Kuwa Tajili katika ardhi ya watu maskini ni sawa na kula embe ndani ya choo cha shule

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Jamii yenye idadi kubwa ya watu maskini huzalisha viongozi wenye fikra za kimaskini!

Hata kama wakisoma; tabia zao zinakuwa zimeathiliwa na historia ya umasikini.
Hata ufanyeje kila kitu ni tabu tupu!
  • Ukiwa Tajiri ni tabu, na usipokuwa nacho ni tabu
  • Ukipata ajira ni tabu, Usipokuwa na ajira ni tabu
  • Ukiwa na Gari binafsi huko barabaran ni tabu, na ukipanda daladala ni kero tupu
  • Ukipanda UDART ni msongamano tupu, na ukipanda Uber ni foleni tupu
  • Ukiwa mwanasiasa ni tabu, na Ukiwa mpiga kura ni kero tupu
  • Anayepuliza vuvuzera la chama anathaminiwa zaidi kuliko mlipa kodi
  • Ukitoa msaada ni lawama na usipotoa unaambiwa unaringa
  • Ukifuata sheria ni kero na ukivunja sheria ni kero pia
Kiufupi kuwa Tajiri katikati ya kundi la maskini yataka moyo sana!!
 
Kula Embe kwenye Choo cha Shule ya IST ni mazingira wezeshi kuliko kula Embe kwenye Ofisi za Mtendaji Kata

Specify Shule na Shule bana

Sema Shule za Wazalendo
 
Back
Top Bottom