Kuwa nje ya nchi wakati wa tatizo kubwa la umeme ni ishara kuwa bado hatuna kiongozi

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Wandugu,Kwa mtazamo wangu, umeme ni kila kitu kwa maisha ya kisasa. Bila umeme nchi inayumba kiuchumi na katika nyanja zote za maisha ya mwananchi. Kinachonisikitisha ni kuwa katikati ya janga hili la nchi kuwa gizani kutokana na upungufu wa umeme, mkuu wetu wa nchi yupo busy na safari za nje. Mbaya zaidi safari zenyewe ni za kustarehe tu. Nimetafakari sana hali hii na kuhitimisha kuwa nchi yetu bado haijapata kiongozi. Sijui mnasemaje wadau?
 
Aliondoka leo kwenda Pretoria for 2 days. Kuna fununu akirudi atakaa for a week then atanyanyua tena pipa kuelekea China.
Huyu bwana mkubwa nchi imemshinda kabisaa.
Heri mara millioni moja tukaweka robot pale ikulu then tuiprogram ili iweze ku-execute kazi zote za raisi na kazi itafanyika vema tu kuliko kuwa na huyu mheshimiwa ofisini. Hadi akiondoka 2015 atafikisha safari 1500 za nje ya nchi. Atamshinda hata Hillary Clinton kwa mileage. Kazi kwenu mnaomtetea mwanamagamba mwenzenu.
JK Hafai na hana uwezo wa kuongoza hata wilaya
 
Juzi alikuwa ktk harusi ya mdogo wake bagamoyo......nadhani wengi wetu tumeona picha kwenye mitandao. Leo tunaambiwa eti kaenda kwenye birthday ya Mandela Africa Kusini (July 18), mafuta ya ndege na msafara wote huo mamilioni ya pesa yameenda..... Kesho kutwa atakwenda Sheli Sheli /Comoro tena maana alisahau kuagana na mwenyeji wake. Twaaaafa.....
 
Anaonyesha uafrika halisi wa kutokua serious na kuona kila kitu kuwa cha kawaida, hilo suala la umeme kwake ni la kawaida na ndio maana mlimsikia akimtetea Ngeleja kwamba asilaumiwe, ila ukame! What a shame.....! kama vile mvua hazijanyesha miezi mitatu mfululizo kwa mara ya kwanza! Wacha aende penye umeme wa uhakika!
 
Wandugu,Kwa mtazamo wangu, umeme ni kila kitu kwa maisha ya kisasa. Bila umeme nchi inayumba kiuchumi na katika nyanja zote za maisha ya mwananchi. Kinachonisikitisha ni kuwa katikati ya janga hili la nchi kuwa gizani kutokana na upungufu wa umeme, mkuu wetu wa nchi yupo busy na safari za nje. Mbaya zaidi safari zenyewe ni za kustarehe tu. Nimetafakari sana hali hii na kuhitimisha kuwa nchi yetu bado haijapata kiongozi. Sijui mnasemaje wadau?
Akiwa anakamilisha safari yake ya 134 nje ya nchi watanzania tupo kwenye giza totolo. Athari za safari za Kikwete zipo wazi mathalani angekuwepo automatically tungepata majibu juu ya adhabu ya rafiki yake Jairo,lakioi PM anasema subirini Rais afike SA nimshitaki. Mi niungane na mwanakijiji kumtaka Rais kutangaza hali ya hatari ili ku-suspend sheria lakini hilo liende sambamba na kumfuta kazi Ngereja na Malima...
 
Hana akili hata kidogo,kilichotokea jana bungeni hata kama angekuwa kwenye ndege angeweza ama kutoa maamuzi juu ya Jairo ama angetakiwa kurudi jana hiyo hiyo kuja kuwajibika kulingana na bunge lilivyosema,vinginevyo atakuwa anarudia historia ya mabomu ya G.mboto badala ya kusaidia kutatua janga yeye aliendelea na safari za nje huku kazi zote akimwachia Kaimu M.mkoa,Saddick...JK ndo tatizo hapa Tz kwa hivi sasa na si vinginevyo
 
watanzania wote tunaonekana wapumbavu kwa kua na raisi mpuuzi asiyejua priorities,kwa safari ni muhimu kuliko kukaa nchini kwake kutatua mambo magumu yanayokabiki taifa.hakika nimeamini msemo wa watu wanaosema ukioa mzaramo uwe tayari kuachwa ndani na mwenzi wako akienda ngomani.same thing nakiona kwa JK,ijumaa alikua kwenye harusi ya mdogo wake,jumamosi alikua kwenye ngoma kijijini kwao,jumatatu ameenda kwenye birthday ya mandela

Kweli kazi tunayo watanzania wenzangu!!!
 
Uraisi na mdundiko wapi na wapi, makosa ni yetu wenyewe,Mwl (RIP) alisema bado ni kijana mdogo lakini tulidharau, acha tulie kwani kilio ni chetu watz wote.
 
Wandugu,Kwa mtazamo wangu, umeme ni kila kitu kwa maisha ya kisasa. Bila umeme nchi inayumba kiuchumi na katika nyanja zote za maisha ya mwananchi. Kinachonisikitisha ni kuwa katikati ya janga hili la nchi kuwa gizani kutokana na upungufu wa umeme, mkuu wetu wa nchi yupo busy na safari za nje. Mbaya zaidi safari zenyewe ni za kustarehe tu. Nimetafakari sana hali hii na kuhitimisha kuwa nchi yetu bado haijapata kiongozi. Sijui mnasemaje wadau?

Hivi unafikiri yeye anaenda kucheza huko?
 
Inahitaji moyo sana kuvumilia huu upuuzi wa serikali yetu, na watanzania ndo tulivyojengwa toka enzi za mwalimu. Ingekuwa nchi nyingine tayari watu wangekuwa barabarani siku nyingi. Lakini kwa vile wabongo/wananchi wamezoea ujanja ujanja kila kona, basi tunaona sawa tu bora liende. Tumepigwa sijui nini hata sijui haziwezi kuwa kali kiasi hiki.
 
Nadhani kuna upungufu mkubwa kwenye safu ya washauri wa Rais. Haiwezekani Rais aende South Africa mara mbili in less than 4 months. Kama ni kutafuta wawekezeji kwa nini hawakufanya hivyo wakati alipotembelea South Africa majuzi? Hii itawachosha hata Wa-south maana kila kukicha mgeni yule yule anakuja ili mradi anatafuta sababu za kuja! Kingine, hivi kutafuta wawekezeji ni lazima Rais aende? TIC ina mana hawana uwezo wa kutafuta wawekezeja mpaka Rais wa nchi aongee nao? What does that say?

Siamini hata kidogo kuwa mwekezeji ataamua kuwekeza kwa sababu tu kaongea na Rais, kwao cha muhimu ni mazingira mazuri na uhakika wa kupata faida, 'Presidents come and go'. Ni hivi majuzi katoka Malaysia, Pinda naye ameenda Brazil kwa kazi hiyo hiyo, sasa TIC wanafanya nini? Ni party orgnisers. Kichekesho tunaambiwa Rais kaenda Pretoria kwa ajili ya kutafuta wawekezeji lakini WAZIRI WA UWEKEZEJI - Mary Nagu yuko Dodoma Bungeni na hata jana kaongea!
 
wandugu,kwa mtazamo wangu, umeme ni kila kitu kwa maisha ya kisasa. Bila umeme nchi inayumba kiuchumi na katika nyanja zote za maisha ya mwananchi. Kinachonisikitisha ni kuwa katikati ya janga hili la nchi kuwa gizani kutokana na upungufu wa umeme, mkuu wetu wa nchi yupo busy na safari za nje. Mbaya zaidi safari zenyewe ni za kustarehe tu. Nimetafakari sana hali hii na kuhitimisha kuwa nchi yetu bado haijapata kiongozi. Sijui mnasemaje wadau?

kikwete alishasema yeye hawezi kugeuka wingu la mvua pale mtera. Kama yeye ndivyo anafikiri sasa tutegemee nini kutoka kwake. Ina maana hajui cha kufanya. Ten years of tanzania leadership inapotea hivi hivi.
 
Back
Top Bottom