Kuwa na Uwezo wa Kufanya Maamuzi Magumu ni Kipaji au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa na Uwezo wa Kufanya Maamuzi Magumu ni Kipaji au?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mawaiba, Apr 26, 2012.

 1. Mawaiba

  Mawaiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 420
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Najaribu kukumbuka jinsi Mwl. J.K. Nyerere alivyokuwa na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi magumu. Nina imani kabisa kutokana na uwezo mkubwa wa J.K. Nyerere katika kusoma alama za nyakati na kufanya maamuzi magumu accordingly, kama leo hii angekuwa hai Nyerere angeshauri muungano wa Bara na Visiwani uvunjwe. Miongoni mwa maamuzi magumu ambayo viongozi wetu wa sasa hawana uwezo wa kuyafanya kwa hiyari ni "kung'atuka" kutoka madarakani kama alivyofanya Nyerere. Hebu tukumbushane baadhi ya maamuzi magumu ambayo Mwalimu aliyafanya wakati wa uhai wake, ili liwe somo kwa viongozi wetu wa sasa. Karibuni....
   
 2. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Mkiwabagua mkasema wao waunguja ss watanganyika...........hotuba hii inaonyesha asingeweza kupendekeza muungano kuvunjwa!
  So jipange upya kisha urudi.
   
 3. Mawaiba

  Mawaiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 420
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiyo kauli aliyoitoa wakati huo haiendani na hali tuliyo nayo hivi sasa. Hali tete ya muungano wa Bara na Visiwani inaashiria kuvunjika kwa amani. Inatakiwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi magumu kuweza kufanya hivyo. "Uzanzi-bara" na "Uzanzi-bari" unamaslahi gani kwa jamii inayopingana na hali hiyo. Kwa kuwa huna uwezo wa kutafakari kwa undani kaa pembeni. Watu mnaokumbatia muungano mnafanya hivyo eti kwa sababu Nyerere alisema muungano ulindwe, lakini kaeni mkijua Nyerere alikuwa flexible. Ndio maana pamoja na kuitawala Tanzania chini ya chama kimoja, lakini mwisho wa siku alishauri mfumo wa vyama vingi, mfumo ambao hivi sasa unapelekea kukua kwa demokrasia Tanzania. Na hii imetokana na uwezo mkubwa wa Nyerere katika kusoma alama za Nyakati. Ndio maana nasema hata issue ya kuvunja muungano ingekuwa simple sana kwa Nyerere.
   
Loading...