Kuwa na mwanamke wa aina hii ni raha sana

The patriot man

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
1,025
1,173
Unakuta uko na mchumba/demu/mke wako anakuambia beib kule Kisarawe kuna viwanja vinauzwa ekari moja laki 4 tu nenda kanunue ekari 5 tukajenge huko tuweke na mifugo, kama kuku wa nyama, na mayai ng"ombe wa maziwa na nguruwe.

Beib kuliko uninunulie iPhone 6 bora ata hiyo hela umlipie wifi yangu ada ya chuo mi nokia Obama inanitoshaa kabisaa au tuongezee na hela nyingine kukanunue kiwanja.

Beib kuna kaka mmoja hivi ananisumbuaga sana yaani king"ang"anizi mpaka kero naomba umfuate umkanye umwambie asinizoee. Ukiwa na mwanamke wa aina hii kamwe usimwache ana focus life syo kukuchuna mwishowe akupige chini.

Sasa unakuta una demu/mke/mchumba wa aina hii beib lini utaninunulia gari la kutembelea coz rafiki yangu Rose kanunulia gari. Beib naomba uninunulie iPhone 6 rafiki yangu Rose kanunuliwa na mchumba wake
Beib naomba laki 3 ya kwenda kufanya shopping ya kununua nguo zangu.

Beib weekend nataka unipeleke Serena hoteli tukaenjoy. Ukiwa na mwanamke wa aina hii mkimbie faster kabla haijakula kwako coz kamwe huwezi kuendelea.Take care mwanaume mwenzangu na hawa viumbe ke.

Wewe mwanamke wako ana sifa zipi kati ya hizi apo juu.
 
Tchaaaaaa lanyeee! Dunia hii ya .com au kwenye ile sayari iliyo karibu ma jua?
 
Back
Top Bottom