Kuwa na mpenzi kunahitaji makubaliano au umri unaofanana?

usiendesema

Member
Feb 5, 2019
10
45
Habari ya majukumu wana jamvi ?
Nimekuja mbele yenu na makala yenye kichwa cha habari hapo juu.

Nimekuwa nilisoma na kufuatilia makala mbalimbali za mapenzi na mahusiano, lakini mpaka sasa bado ninamkanganyiko wa mawazo kuuna wakati nilisoma mapenzi mazuri yanahitaji kufanana au kukaribiana kwa umri.

Bado pia nimekosa uhakika wa wazi juu ya hilo, wakati mwingine pia nilisoma nikaona yanahitaji makubaliano nilichokigundua ni kwamba watu wengi huliendea jambo hili kwa kurithishwa kutoka katika tamaduni au historia za koo mbalimbali.

Lakini niwaombe wana jamvi,mara nyingi tumekua tukizikosea nafsi zetu kwa kukariri mambo ambayo yanaweza kuwa na madhara waweza kumpoteza mtu mwenye mapenzi ya kweli eti kwa kuona aibu kwakua hamfanani umri.

Kwa uzoefu nilionao nimewahi ona wapenzi wenye umri unaofanana wanaishi kwa shida na taabu sana katika mapenzi yao.

Vivyo hivyo niliona wapenzi wenye umri uliotofautiana lakini walifurahia mahusiano yao, hivyo basi niwakaribishe wana jamvi tushirikiane pamoja ili tuelimishane juu ya nafasi ya kuwa na mpenzi au mwenza ili tusinyimane nafasi na raha za mahusiano (mapenzi) kwa kuweka matabaka yasiyo na nguvu za hoja na sidhani kama kuna madhara yoyote katika uhuru wa mahusiano ya kimapenzi.
Asante ...Karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
4,366
2,000
Unaweza date na mzee freshy tu all is abot love


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Televoco

Member
Jan 21, 2019
19
45
Nimegundua tatzo lako "unasoma sana"! , mkuu hakuna cheti kwenye mapenzi eti, kuwa na mtu ambae roho yako kwanza inajiskia vizuri kuwa nae , sio waloandika sifa zake huko unakosoma maana huyo aloandikwa ni mapenzi ya mwandishi ambayo ni tofauti na yako! mfano mimi huwa napenda mapokezi(sura nzuri) na msambwanda mengine tunavumiliana ila kwa wengine tofauti.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom