Kuwa na mambo mengi yaliyo sahihi kisheria lakini yasiyo halali ni dalili ya ufisadi

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Katika nchi inayoendeshwa kifisadi watu waliopewa dhamana za uongozi utumia nafasi hizo kujineemesha wao wenyewe kwa maamuzi yasiokuwa halali. Hata hivyo ingawa maamuzi hayo yanakuwa hayakuzingatia taratibu, lakini kwakuwa ndio wenye mamlaka, yakishatolewa nao yanakuwa na nguvu za kisheria. Kwa mfano kama taratibu zinahitaji mtu kabla hajamilikishwa kiwanja apate kwanza baraka za kikao husika, lakini mtu mwenye madaraka akatumia wadhifa wake kutoa miliki bila ya kupitia kwenye kikao husika, mmiliki hiyo itakuwa sahihi kisheria, ingawaje siyo halali. Hiyo ndiyo hali atakayokumbana nayo Prof. Tibahijuka katika vita yake na wavamizi wa viwanja vya wazi. Huko nyuma, ambapo vitendo vya rushwa vilikuwa havivumiliki, ili kitu kiwe sahihi kisheria kilitakiwa pia kiwe halali. Hayo yalikuwa katika miaka ya tisini, ambapo cheo kilichukuliwa kuwa dhamana. Lakini kuanzia kipindi cha pili cha rais Mkapa usahihi wa kitu kisheria na uhalali wake viko mbali sana kama uwingu na dunia. Si mnajua, siku hizi mambo yanaendeshwa kwa kauli mbiu ya mbuzi anakula kulingana na urefu wa kamba yake.
 
Back
Top Bottom