Kuwa na laini ya TTCL iwe ni lazima kwa watanzania wote TTCL iimarishwe zaidi

Nizungumze kizalendo kabisa kuhusu hii Ttcl hii ni kampuni ya Serikali inatutosha kabisa katika suala la mawasiliano na ushindani nchini

Uwekezaji wa ttcl ukiangalia walivyosambaza cable kila pahala sio uwekezaji mdogo ni uwekezaji mkubwa sana
Acha ushamba bwana, sasa hivi ni soko huru na kinacho matter ni huduma kwa wateja.
Watu mnasahau haraka, TTCL ndiyo ilikuwa ya kwanza kuwa na huduma ya simu za mkononi kupitia kampuni tanzu yake nafikiri CELTEL miaka ya 90.

Yaliyotokea humo ni ufisadi mkubwa, wizi, na huduma mbove na kuingiliwa na wanasiasa.

Kampuni ikapoteza wateja na yalipoingia makampuni mengine CELTEL ikafa au ikanunuliwa na wabia wengine, na ndiyo sasa kuna mradi wa TTCL simu za mkononi.
Hata leo TTCL simu za mkononi huduma mbovu sana, huduma inaweza katika for days!
Hata ukitia taarifa hakuna anayejali.

Huduma ya TTCL waachiwe viongozi wa serikali.
 
Kizuri cha jiuza mkuu. Ttcl hawako serious, mimi nilishangaa mwaka 2015 nlienda kagrra huko vijijini nikashangaa watu wengi wanatumia halotel ambayo kiukweli haikuwa na muda sokoni.
Ttcl hawako kibiashara. Ukilazimisha watu wanunue line watanunua na hawataitumia unless uyaue makampuni menginr kama walivyofanya kwa fastjet ili airtz ishike soko
Halotel ndio mtandao pekee ambao sehemu mitandao mingine haipatikani wao wanapatikana wako vizuri mno hata uende vijijini vipi halotel inadaka
 
Hao kila siku wanatupandishia bei za vifurushi, nawakataa sio mda.
Kwanza ni urasimu huo.
 
Halotel ndio mtandao pekee ambao sehemu mitandao mingine haipatikani wao wanapatikana wako vizuri mno hata uende vijijini vipi halotel inadaka
Sijajua kwann ttcl hawako serious. Kuna kipindi hata upatikanaji wa vocha ilikuwa shida. Kuna kipindi nilikuwa naishi mivumoni hapo, nikanunua ttcl line, aisee network ilikuwa shida niliacha itumia next day
 
Nizungumze kizalendo kabisa kuhusu hii Ttcl hii ni kampuni ya Serikali inatutosha kabisa katika suala la mawasiliano na ushindani nchini

Uwekezaji wa ttcl ukiangalia walivyosambaza cable kila pahala sio uwekezaji mdogo ni uwekezaji mkubwa sana
Huna akili

Wewe ni kama meko tu
Vipi unadhani sababu gani iliwafanya tigo na voda wakawa na wateja wengi?

Rudi shule
 
Waajili Maguru pale waache kuajili watoto wadogo wa UVCCM na kukumbatia wale wazee kizazi cha Nyerere kinachoamini katika ujamaa.

Hii ni Karne ya ushindani inayohitaji wachapa kazi na vichwa smart ili uone faida na maendeleo ya kampuni yako... TTCL iendeshea kama private entity na scheme za mishahara ziendane na soko la ajira kwenye industry ya telecom, mfumo wa kuajiri uendane na mazingira...
 
Kampuni ya kizalendo lakini huduma za kibepari.
Wakiboresha huduma wateja watawakimbia wenyewe.
 
Nizungumze kizalendo kabisa kuhusu hii Ttcl hii ni kampuni ya Serikali inatutosha kabisa katika suala la mawasiliano na ushindani nchini

Uwekezaji wa ttcl ukiangalia walivyosambaza cable kila pahala sio uwekezaji mdogo ni uwekezaji mkubwa sana
Ni wazo zuri lakini serikali haijawahi kuwa na kitu kizuri angalia mfano TBC uwekezaji ni mkubwa ila huduma zao ni zaidi ya utopolo hamna mtu mwenye akili timamu anaweza kukaa na kuangalia na hao ttcl ndio walewale tu hawana jipya
 
Haya mashirika hayataki siasa na wanasiasa, yanataka watu wa kazi walio smart vichwani na waliozoea kupimwa kulingana na matokeo..
 
Huko ni kutaka kutuingiza jehenama.

Yatajirudia yaleyale ya kuua Fast jet iliyotuonjesha wengi kupanda ndege - sasa tunazisikia redioni.
 
Sijajua kwann ttcl hawako serious. Kuna kipindi hata upatikanaji wa vocha ilikuwa shida. Kuna kipindi nilikuwa naishi mivumoni hapo, nikanunua ttcl line, aisee network ilikuwa shida niliacha itumia next day
Vocha za TTCL mitaani sehemu kubwa hazipo!
 
Nina laini ya ttcl lakn kupata vocha ya jero inanibid nitumie naul ya tsh 5000/- kwenda na kurud

Huon Kama huu mtandao umeniongezea mzigo wa maisha

Na line ya voda na tigo situmii hata shilingi kuifuata vocha

...angalia hapo kipi kinanipa umasikini...
 
Nizungumze kizalendo kabisa kuhusu hii Ttcl hii ni kampuni ya Serikali inatutosha kabisa katika suala la mawasiliano na ushindani nchini

Uwekezaji wa ttcl ukiangalia walivyosambaza cable kila pahala sio uwekezaji mdogo ni uwekezaji mkubwa sana
Hakuna kampuni ya simu inaendeshwa kipuuzi kama hii ya TTCL,,

Huduma kwa wateja mbovu,,vocha mtihani kupata imagine unaeza tafuta vocha ya buku hakuna hadi makao makuu yao unaenda wanakwambia bado hamna,,ukitaka kutumia T pesa majanga zaidi mawakala wachache na hao wachache wenyewe hizo laini za T pesa walipata kwa tabu na mizunguko kibao unaeza isubiria Till mwaka mzima,,kulipa comision mawakala wao imekuwa kero kuu,,wakala anaeza fanya kazi miezi miwili hapati comision

Kiufupi hakuna kampuni hapo
 
Mmekaa kumsema Magufuli alikuwa dikteta kumbe nyinyi ndio madikteta wakubwa sema hamjapata nafasi. Kama ttcl wanataka kuteka soko ni rahisi tu waweke vifurushi vya ushindani na sio pamoja na favor zote wanazopata bado gharama hazipishani na mitandao mingine
 
Si walikuja na process ya kila mtu wa serikalini awe na line ya ttcl imeiishia wap?
Ilisaidia sanaa watu wakanunua line sanaa.
Now wameaanza kulega tenaaa
 
Back
Top Bottom