Kuwa na laini ya TTCL iwe ni lazima kwa watanzania wote TTCL iimarishwe zaidi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,887
Nizungumze kizalendo kabisa kuhusu hii Ttcl hii ni kampuni ya Serikali inatutosha kabisa katika suala la mawasiliano na ushindani nchini

Uwekezaji wa ttcl ukiangalia walivyosambaza cable kila pahala sio uwekezaji mdogo ni uwekezaji mkubwa sana

Kiukweli sasa hivi ttcl inapatikana naweza kusema ni nchi nzima almost maeneo mengi niliyotembelea ipo

Cha ajabu na kinachoniliza ni watumiaji wachache, hawa jamaa wana ofisi za kutosha, kila kitu yaani, wanauhakika wa kufanya kazi zao na ulinzi nzuri wa kisera maana serikali inalea hili shirika

Ttcl waboreshe network zao,,,,wasambaze 4g zaidi....Ikiwezekana waje na 5g.....Iwe ni lazima kila mtanzania kumiliki line ya TTCL ...naam isiwe ni lazima kutumia lakini walau iwe ni lazima kila mtu kusajili line ya Ttcl

Faida ya hii ni kwamba

1.Ttcl itapata mamilioni ya wateja

2.Mapato yataongezeka maradufu

3.Mabando yatashuka na yatakua bei chee

4.Italeta ushindani na makampuni mengine nayo itabidi waanze kuwaza mbinu za kuendelea kushindana ikiwemo kutazama vifurushi upya nk...

Ttcl ikiwa imara na inayotengeneza kipato ikiwa na usimamizi nzuri, serikali inaweza kuvuna na kupata matrilioni ya pesa kutoka kwenye hili shirika....nawaambia ttcl inaweza ikafanya tukapunguza kutegemea misaada kwa kiasi fulani maana tutapata mapato makubwa sana kupitia ttcl

Halafu hili litaenda sambamba na kushusha vifurushi viwe bei chee zaidi...yakifanyika haya tutarajie Ttcl pesa zikizagaa kila mahali hadi vijijini

Mfano sasahv ukienda vijijin huko wilayani inakamata vizuri tu tena inasoma 3G na H+ yenye speed balaa,ofisi zipo,minara ipo lakini cha ajabu unakuta watumiaji kwa wilaya husika hawafiki hata watu 400 hili linaumiza sana, na hapo serikali imewekeza sana huku ttcl, fedha nyingi sana zimetumika,mikongo ya taifa inajengwa ya mabilioni

Inabidi tuvae roho ngumu tu kuhusu kuinyanyua ttcl kuwa na line ya ttcl iwe ni lazima kwa kila mtanzania kwa manufaa ya nchi yetu
 
Mimi sikumbuki mara ya mwisho niliwaona lini hawa TTCL mitaani hata masokoni.

Kila siku hasubuhi ukitembea tu barabarani masomoni, hukosi kukutana na watu wanasajili laini za voda, tigo lakini hawa ttcl, labda kam ndotoni wanapatikana kwa wengi hapo tutakubali.

Bado ttcl wamezubaa sana.
 
mimi sikumbuki mara ya mwisho niliwaona lini hawa TTCL mitaani hata masokoni
Kila siku hasubuhi ukitembea tu barabarani masomoni, hukosi kukutana na watu wanasajili laini za voda, tigo lakini hawa ttcl, labda kam ndotoni wanapatikana kwa wengi hapo tutakubali.
Bado ttcl wamezubaa sana.
Kuna haja ya ttcl kuimarishwa maana faida za makampuni ya vodacom mathalani zinaenda kujenga london na Washington
 
Kundi la Vodafone, ambalo linajulikana kwa jina la Global Partnership for Ethiopia, linajumuisha kampuni za Vodafone, Safaricom, Vodacom Group, Sumitomo Corporation, CDC Group (inamilikiwa na serikali ya Uingereza), na US Development Finance Corporation (inamilikiwa na serikali ya Marekani).
 
Biashara wala sio nguvu, na amri za kijinga kijinga, bali ni mikakati imara tu, licha ya ATCL, kuifanyia figisu figisu fastjet , je ilifanikiwa kutawala soko la anga nchini na kutengeneza faida?

Usione makampuni binafsi ya simu yanafanikiwa ukafikiria wanakaa tu, ofisini, na kuwaza kuandaa makongamano, warsha, na mikutano ya bodi ili kupiga pesa, kama makampuni ya serikali yanayotegemea ruzuku tu!!

waangalie tigo ni mtandao ambao ki ukweli zamani ulionekana kama wa wanafunzi tu, lakini walipokuja na promotions nzuri, walifanikiwa kuteka wateja wengi sana, hasa wa maeneo ya mjini.
 
Unasema italeta ushindan sasa huo ushindan utakujaje wakati kampuni moja inapendelewa kwa kulazimisha watu waumie huduma zake kwa lazima?
 
Nizungumze kizalendo kabisa kuhusu hii Ttcl hii ni kampuni ya Serikali inatutosha kabisa katika suala la mawasiliano na ushindani nchini...
Ulazima wa kila Mtz kuwa mteja wao, utaletwa na hayo uliyoorodhesha, yaani huduma zilizowazidi wengine, slo uzalendo.
 
Uchumi haiwezi inuliwa kwa kanuni za kifashisti ivo asee. Hizo akili za jiwe zilitumika kuua FAST JET na kuifufua ATC ila hakuna alilofanikiwa.

Wao kama TTCL waboreshe huduma. Mm ni mteja wa TTCL ila vijiji vingi nilivyotembea hakuna NETWORK ya TTCL unategemea hata kupiga kutuma sms au kutumia internet ingekuwa huduma ya bure nani angetumia lain ambayo ukitoka mjini 8km network haikamati
 
Hakuna haja ya kulazimisha kila mtanzania kutumia laini ya TTCL,ni suala la wao tu kuja na strategy nzuri za ku acquire new customers wa kutosha while wakiendelea ku retain existing customers,so ni issue ya wao kuwa serious tu..
 
ATCL imeachiwa soko lote la ndani ,haina mpinzani na bado inapata hasara
Biashara ni mbinu , sio nguvu za kulazimisha
 
Nizungumze kizalendo kabisa kuhusu hii Ttcl hii ni kampuni ya Serikali inatutosha kabisa katika suala la mawasiliano na ushindani nchini

Uwekezaji wa ttcl ukiangalia walivyosambaza cable kila pahala sio uwekezaji mdogo ni uwekezaji mkubwa sana
TTCL wapunguze rates na wahakikishe mtandao upo stable! Huwezi kuuza mabando kwa hela ya kukomoa na huduma zao mbovu halafu utegemee watu waende huko!

Kama kuna mda mzuri wa kupiga hela ni sasa. Waji organize waweke bundle za internet bei rahisi! Unlimited plan za nyumbani pia waanzishe!
 
Nizungumze kizalendo kabisa kuhusu hii Ttcl hii ni kampuni ya Serikali inatutosha kabisa katika suala la mawasiliano na ushindani nchini

Uwekezaji wa ttcl ukiangalia walivyosambaza cable kila pahala sio uwekezaji mdogo ni uwekezaji mkubwa sana

Kiukweli sasa hivi ttcl inapatikana naweza kusema ni nchi nzima almost maeneo mengi niliyotembelea ipo
Hizi akili hizi,hii ni Sawa na kulazimisha kila mtu aende hospitari kulipua dozi ya malaria kila mwezi hata kama haumwi.
Boda,Tigo,Airtel,walimlazimisha nani kutumia mitandao yao?
Baada ya kuwaza kisayansi,unawaza kama mganga wa kienyeji.
Rushwa,Rushwa,uongozi wa hovyo ndio uneiua TTCL.
Serikali iige kilichofanywa TBL,NMB,TCC,
 
Nizungumze kizalendo kabisa kuhusu hii Ttcl hii ni kampuni ya Serikali inatutosha kabisa katika suala la mawasiliano na ushindani nchini

Uwekezaji wa ttcl ukiangalia walivyosambaza cable kila pahala sio uwekezaji mdogo ni uwekezaji mkubwa sana
Kizuri cha jiuza mkuu. Ttcl hawako serious, mimi nilishangaa mwaka 2015 nlienda kagrra huko vijijini nikashangaa watu wengi wanatumia halotel ambayo kiukweli haikuwa na muda sokoni.

Ttcl hawako kibiashara. Ukilazimisha watu wanunue line watanunua na hawataitumia unless uyaue makampuni menginr kama walivyofanya kwa fastjet ili airtz ishike soko
 
Back
Top Bottom