Jaffary
JF-Expert Member
- Oct 29, 2011
- 806
- 385
Wewe utakuwa na tatizo kwenye ubongo wako. Mwanasheria ni mhitimu wa shahada ya sheria kutoka kwenye chuo kilichosajiliwa na serikali. Wakili ni mhitimu wa shahada ya sheria plus aliyefaulu Bar Exams au Law School.Mnaokosoa wote naona mnashindwa kuelewa tofauti ya MWANASHERIA na WAKILI.
Mwanasheria ni mtu yeyote ambaye amejifunza na anaijua sheria.
Wakili ni mtu aliyepewa idhini ya kuwakilisha watu kwenye kesi Mahakamani. Ili kuwa Wakili ndo inabidi usome degree na ufaulu Law School. Lakini Mwanasheria sio lazima kupitia kote huko.
Nifafanue tu kwamba kozi hii haitakufanya uwe Wakili, ila itakufanya uwe Mwanasheria.
Jambo la Muhimu kwa mnaotaka kujifunza kufahamu ni kwamba MAHAKAMA ZIKO WAZI KWA KILA MTU. SIO KWA MAWAKILI TU. MTU YEYOTE ANAKARIBISHWA KUFUNGUA KESI YAKE MAHAKAMANI AU KUJITETEA KWENYE MASHTAKA DHIDI YAKE MAHAKAMANI. SIO LAZIMA ATETEWE NA WAKILI.
Kwa hiyo kozi hii ndo imelenga hapo. Kukuwezesha uweze kuitumia Mahakama vizuri kwenye ishu zako za Kisheria.
Natumai mpaka hapo tumeelewana.
Wacha utapeli kijana, tafuta pesa kihalali vinginevyo utajuta!