Kuwa mtu wa malalamiko sana ni dalili ya kukata tamaa

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
Nimeishi nimejionea watu wa namna hii maongezi yao asilimia kubwa ni kulaumu na kulalamika. Hii ni dalili mbovu na ni mbaya mno kwani huonyesha mtu husika kuwa ni mtu ambae ameshakata tamaa na kilichobaki ni kulaumu na kulalamika kwa mambo mengine ambayo hayana nyuma wala mbele!

Inawezakuwa ni tatizo la kisaikolojia na mtu anahitaji ushauri na nasaha,maana wengine mambo ya maisha huwafanya kuwa hivyo.

Lkn binafsi tabia hii mtu wa hivi hunikera mno! Sipendi mtu ambae asilimia kubwa ya maongezi yake ni kulalamika tu na anavyolalamikia vingine anaweza kuviepuka maana vipo chini ya uwezo wake na kwakuwa haivitekelezi basi anajikuta vinamzonga na kwakuwa alishakata tamaa basi amekuwa mtu wa kulalamika tu.

Nashauri watu wengine mjiepushe na aina hii ya watu! Maana hii ni kama tabia na unaweza kuirithi! Maana muda mwengine ubongo unamtindo wa kuenenda kwa kujifananisha Kama fulani (kuiga tabia).

Yangu ni hayo, kama utaona unahili tatizo anza kufikiri chimbuko la tatizo hilo na utatue inaweza kuwa ni swala lolote aidha elimu,uchumi au Imani za kipuuzi tu au familia n.k

Ukishindwa jitahidi kutafuta wanasaikolojia wakusaidie.

Am out.
 
green rajab

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
2,459
2,000
Unamaanisha kulaumu tumbo haliridhiki na msosi kila wakati njaa wakati unaweza kuepuka tatizo kwa kujiua tu.
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
Unamaanisha kulaumu tumbo haliridhiki na msosi kila wakati njaa wakati unaweza kuepuka tatizo kwa kujiua tu.
Inategemea na unataka nini! Kama unaona uhai hauna umuhimu kwako basi jiue tu! Lkn Kama unaweza kupanda ardhi na ukalima ukapata chakula cha kukutosha Basi fanya hivyo..

Muda mwengine unahitaji kubadili hali yako moja tu ili ubadili hali nyengine nyingi mfano ukiweza kubadili hali yako ya uchumi ukawa stable basi utaweza kula utakavyo,utasoma utakavyo,utaendesha gari utakayo,utaishi hata nchi utakayo n.k

kazi inakuja unapofanya vitu kuwa complicated hapo lazima udate.. mkuu maisha ni kujua unalenga wapi mshale wako.
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
Sasa mbona na wewe mwenyewe unatulalamikia sisi tunao lalamika kwa kila jambo? Tofauti ya wewe na sisi iko wapi sasa!!!

Ulitakiwa ukae kimya!!!!
Sijalalamika hapa.. Soma vizuri na uelewe!.
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
pia ni vyema ukiona mtu wa malalamiko umwambie hapohapo.
Ananishinda ubavu nikimuambia nitaambulia kipigo! Laita ingalikuwa nammudu ningemuambia tena face to face!
Kwa malalamiko aliyonayo nikimuambia tu ataanza kunirushia ngumi! Sijui utafurahi kunikosa au vipi nikiwa na minundu..🤣😅
 
chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
3,149
2,000
Nimeishi nimejionea watu wa namna hii maongezi yao asilimia kubwa ni kulaumu na kulalamika. Hii ni dalili mbovu na ni mbaya mno kwani huonyesha mtu husika kuwa ni mtu ambae ameshakata tamaa na kilichobaki ni kulaumu na kulalamika kwa mambo mengine ambayo hayana nyuma wala mbele!

Inawezakuwa ni tatizo la kisaikolojia na mtu anahitaji ushauri na nasaha,maana wengine mambo ya maisha huwafanya kuwa hivyo.

Lkn binafsi tabia hii mtu wa hivi hunikera mno! Sipendi mtu ambae asilimia kubwa ya maongezi yake ni kulalamika tu na anavyolalamikia vingine anaweza kuviepuka maana vipo chini ya uwezo wake na kwakuwa haivitekelezi basi anajikuta vinamzonga na kwakuwa alishakata tamaa basi amekuwa mtu wa kulalamika tu.

Nashauri watu wengine mjiepushe na aina hii ya watu! Maana hii ni kama tabia na unaweza kuirithi! Maana muda mwengine ubongo unamtindo wa kuenenda kwa kujifananisha Kama fulani (kuiga tabia).

Yangu ni hayo, kama utaona unahili tatizo anza kufikiri chimbuko la tatizo hilo na utatue inaweza kuwa ni swala lolote aidha elimu,uchumi au Imani za kipuuzi tu au familia n.k

Ukishindwa jitahidi kutafuta wanasaikolojia wakusaidie.

Am out.

Watu wana kwambia matatizo ya sikie kwa mwenzako.unajua walikuwa wanamaanisha nini !
Yaki kupata utabadilisha mada
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
Watu wana kwambia matatizo ya sikie kwa mwenzako.unajua walikuwa wanamaanisha nini !
Yaki kupata utabadilisha mada
Umeandika hata bila kufikiri mkuu!.

Mkuu huijui historia yangu hata punje!.
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
10,994
2,000
Kuna jamaa angu mmoja ana ilo tatizo.

Yaan hajawai kuridhika Wala kupongeza,

Mwanae juz kafaulu kapata division One ya 12 shule ya kata, watu tunampongeza yeye analalamika Tena mbele ya mwanae
Eti
" hamna kitu mle, ulkua mwaka wa uchaguzi ule. matokeo yamekuja kisiasa aya"

Hadi mwanae amebaki anamshangaa baba ake.
 
chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
3,149
2,000
Umeandika hata bila kufikiri mkuu!.

Mkuu huijui historia yangu hata punje!.

Kwa sasa hayaja kufika.unaweza kuona na kukejeli ukiwa hupo sawa na unamatatizo unaweza kuona wengine wamerukwa na akili au wanashindwa kufanya kama wewe.
Rahaa ya ngoma ingia ucheze na mashabiki ndio wanajua mpira kuliko wachezaji wenyeji
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
Kuna jamaa angu mmoja ana ilo tatizo.

Yaan hajawai kuridhika Wala kupongeza,

Mwanae juz kafaulu kapata division One ya 12 shule ya kata, watu tunampongeza yeye analalamika Tena mbele ya mwanae
Eti
" hamna kitu mle, ulkua mwaka wa uchaguzi ule. matokeo yamekuja kisiasa aya"

Hadi mwanae amebaki anamshangaa baba ake.
Mkuu haya mambo yapo japo watu wanachukulia poa!
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
Kwa sasa hayaja kufika.unaweza kuona na kukejeli ukiwa hupo sawa na unamatatizo unaweza kuona wengine wamerukwa na akili au wanashindwa kufanya kama wewe.
Rahaa ya ngoma ingia ucheze na mashabiki ndio wanajua mpira kuliko wachezaji wenyeji
Mkuu naomba tu niishie hapa! Kuwa na siku njema tu.
 
lliedie

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
1,179
2,000
Ananishinda ubavu nikimuambia nitaambulia kipigo! Laita ingalikuwa nammudu ningemuambia tena face to face!
Kwa malalamiko aliyonayo nikimuambia tu ataanza kunirushia ngumi! Sijui utafurahi kunikosa au vipi nikiwa na minundu..🤣😅
niambie Ni Nani nikamwambie huenda naweza kummudu Mimi pia useme na jinsia yake ili nijue namwendea vipi
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,509
2,000
Mtu anaelalamika mara nyingi anatafuta suluhu ya jambo linalo tesa akili yake,na hilo jambo inaonesha kuwa linajirudia,kwahiyo kama ni mtu wako wa karibu simply jaribu kubadilika na uende na mapigo yake uone kama ataendelea kulalamika...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom