Kama ni michango ya harusi- sote tunalipa
Kama ni michango ya ujenzi wa shule- tunalipa
Kaka sina Ada- tunalipa
Dada sina karo ya shule-tunalipa
Mama mwaka huu mvua haikunyesha- tunalipa
Mwanangu nikakufa na njaa- tunalipa
Mwanangu nyumba inaniangukia- tunalipa
Kaka sina viatu vya shule wala uniform – tunalipa
Kaka board ya mikopo inataka lazima uwe na kiasi Fulani ndio ukopeshwe- tunalipa
Kaka tuma hela za kiwanja- tunalipa
Dada bado kidogo tu tufukuzwe kwenye pango- tunalipa
Baba niongezee mchano wa karo- tunalipa
Mama nina deni la Saccos – tunalipa
Na mengineyo mengi,
sasa kwa nini mnatunyanyasa na mnaendelea kututumia ? Mirija lazima ifungwe mpaka akili zenu ziamke zianze kung'amua mambo kwamba sote tuko sawa, watoto wa tumbo moja, baba mmoja na nchi yetu sote moja , ndugu wa damu kuzaliwa Tanzania na ni katika kutafuta tu maisha ndio maana wengine tuko huku ngambo ya mbali, wengine Dar es salaam toka mikoani mianka nenda rudi bila mtu kurudi kwao hata kusalimia tu; sote twajua huku ulaya na marekani kwamba fainali uzeeni na hili tunalijua sana tu . Acheni kutubagua wakatu sote ni wamoja , wachina , wapakistani na wengineo munawapa uraia na sisi munasuasua , maana yake nini… hamuna mapenzi ya dhati kwetu ili hali michango yetu munaiomba kwa udi na uvumba na mchana pia usiku ni kupanga namna ya kutuchoma fedha tu huku.
Hakuna tofauti yeyote kati yetu na ndugu zetu wa Arusha wenye asili ya musoma na kwingineko wanochukua masaa 12 kusafiri kwa basi mbugani serengiti au hata miaka kenda bila kwenda salimia makwao toka Dar Es Salaam ili hali sisi ni masaa 8 tu… haijalishi kama tuko huku au la na tunakuja kila likizo na wake na watoto zetu.
Haki yetu ya Urai isiwe mpira wa miguu kupigwa huku na kule , haki tunaitaka na msitulazimishe kuwakana wazazi wetu na uraia wetu maana kukaana uraia maana yake ni kuwakana wazazi wako waliokupa uraia huo na hakuna kitu kama hicho huku ulaya na marekani…na ndio maana hata serikali hizi za huku hawakuambii uukane uraia wako… wanakutumia tu na wewe unawatumia tu… mtumikie kafiri upate mradi wako.
Vinginevyo kama hamtaki kututambua acheni kutufanya kitega uchumi na kuja na madili mengi tu ya ufisadi kifamilia ili muweze kutubomu fedha, mipango yenu ya kutufanya vitega uchumi tunaijua na sio kwamba kuishi huku hatujui kinachoendelea huko na habari za huko tunazisoma ili hali asilimia sabini bado wako usingizini tu… kama hamtutaki achezi kuja na vijisababu vya chehechea ili hali mna madeni ya kulipa kwenye board ya mikopo.. kwa nini basi mlienda kukopa wakati shule hamkuilewa?
Eti usalama, eti Uzalendo , upuumzi mtu, hivi mkiruhusini huo uraia pacha maana yake ni ndio mtaanza tena madili ya kuwagiwia akina awilo longomba kama njugu huo uraia wa Tanzania? Mtawapa tu bila masharti? Mnatupa tu kichefu chefu kwa jinsi mnavyo tufanyia sisi ndugezeni wa huku, jifunzeni kisa cha mwana mpotevu, kaka yake na baba yake