Kuwa msemaji wa CCM kunahitaji moyo

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,305
12,600
CCM ni chama ambacho kinahusika na maendeleo na hali ya maisha ya watanzania tangu mwaka 1961 hadi leo. Hivyo sababu zilizosababisha hali ya maisha ya watu, uchumi, afya, elimu, afya, madeni, kilimo, uvuvi, ufugaji, michezo, ufisadi na mipango miji iwe hivi ilivyo leo sababu na majibu wanayo CCM pekee.

Mazuri wanayo mengi na mabaya wanayo mengi pia. Mfano, msemaji wa CCM hivi sasa anayo kazi ngumu sana ya mujibu ziliko sh. 1.5 trillion, manunuzi yasiyozingatia kanuni, matumizi ya serikali bila ya idhini ya wabunge, na hata ikibidi kuhitajika kutoa majibu ya kwanini wanaume ni rahisi kuwatelekeza watoto wao wa nje ya ndoa.

Msemaji wa CCM ana kazi nguvu sana kuijibia CCM maswali haya yote ambayo wananchi makini wanataka kupata majibu kutoka serikali yao ya CCM. Hivyo, ugomvi, ujanjaujanja, mizengwe, kigugumizi, mbinu na hasira za kati ya watoa majibu na wauliza maswali utanzia hapo.

Kazi ya msemaji wa CCM itakuwa nyepesi kama atasimama kidete kuisimamia serikali yake ifuate sheria na kanuni zote za utawala bora vinginevyo iko siku atakosa jibu sahihi hata moja la mdomo la kuwapa wananchi juu ya maswali yao kwa serikali yao. Kama siku hali ikifikia huko huenda tukashuhudia utawala wa mabavu nchi hii.

Chanzo cha utawala wa mabavu duniani ni pale watawala wanapokosa au wanaposhindwa kutoa majibu sahihi kwa maswali na hoja za wananchi kuhusu matumizi sahihi ya jasho lao na namna ya kugawana pato la ziada (surplus ) linavyotumiwa au kugawanywa na watawala.
 
CCM ni chama ambacho kinahusika na maendeleo na hali ya maisha ya watanzania tangu mwaka 1961 hadi leo. Hivyo sababu zilizosababisha hali ya maisha ya watu, uchumi, afya, elimu, afya, madeni, kilimo, uvuvi, ufugaji, ufisadi na mipango miji iwe hivi ilivyo leo sababu na majibu wanayo CCM pekee.

Mazuri wanayo mengi na mabaya wanayo mengi pia. Mfano, msemaji wa CCM hivi sasa anayo kazi ngumu sana ya mujibu ziliko sh. 1.5 trillion, manunuzi yasiyozingatia kanuni, matumizi ya serikali bila ya idhini ya wabunge, na hata kwanini wanaume ni rahisi kuwatelekeza watoto wao wa nje ya ndoa.

Msemaji wa CCM ana kazi nguvu sana kuijibia CCM maswali haya yote ambayo ambayo wananchi makini wanataka kupata majibu kutoka serikali ya CCM. Hivyo, ugomvi, ujanjaujanja, mizengwe, kigugumizi, mbinu, hasira za kati watoa majibu na wauliza maswali utanzia hapo.

Kazi ya msemaji wa CCM itakuwa nyepesi kama atasimama kidete kuisimamia serikali yake ifuate sheria na kanuni zote za utawala bora.
Kunahitaji akili ugumu unakuja ukiwa kichwa Maji
 
Kitu cha hovyo wanachokifanya ccm ni kuwaona watanzania kama watu wasiojielewa na wao ndio wenye hati miliki na nchi Kitu ambacho si kweli. Mara nyingi wanaendesha nchi kwa akili zao bila kufata katiba ya nchi, kutopenda maendeleo ya watu na kupenda kujigawia ajira wao wenyewe (makada wa chama) wakati wapiga kura ni watu wa itikadi tofauti.
 
Back
Top Bottom