Kuwa mlinzi wa fedha zako

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
KUWA MLINZI IMARA WA FEDHA ZAKO,

Tunaishi dunia ambayo kila mtu kuna kitu anatafuta. Na kipimo kimoja ambacho kinapima kile ambacho kila mtu anataka ni fedha.
Kama unataka kuwa na maisha yenye hadhi nzuri basi yatapimwa kwa kiwango cha fedha unachotengeneza au ulichonacho.
Hivyo kwa kila wakati kila mmoja wetu anapambana kupata fedha.

Tunafanya kazi na biashara zinazowasaidia wengine ila mwisho wa siku tunataka na sisi kupata fedha ambazo zitatusaidia kwatika mahitaji mengine muhimu.

Katika mchakato huu wa maisha wa kila mtu kutafuta fedha, imefika hatua sasa kila mtu anawinda fedha uliyonayo wewe. Kila mtu anakazana kukushawishi utoe fedha yako ili aipate yeye.

Mtu anayeuza nguzo nzuri na kukushawishi kwamba huwezi kupata nyingine kama hizo anafanya yote hayo ili aipate fedha uliyonayo mfukoni.

Mtu anayeandaa tamasha na kukuambia kwamba ni la kukata na shoka, hutakiwi kulikosa, anatumia mbinu zote hizo kuhakikisha wewe unatoa fedha yako na yeye anufaike kwa kiasi chake.

Jua kwamba kila mtu unayekutana naye katika mazingira ya kazi au biashara anatafuta jinsi ya kuipata fedha yako.

Sio jambo baya kwa kuwa unapata huduma, ila pia kuna somo kubwa sana unatakiwa kujifunza hapa. Kama kila mtu anaiwinda fedha yako, je wewe ni juhudi gani unazofanya kuilinda isichukuliwe hovyo?

Huwezi tu kutoa fedha kwa sababu mtu amekushawishi ufanye hivyo, japo kuna wengi wanafanya hivi, unakutana na muuza nguo, hukuwa na mpango wa kununua nguo ila unajishangaa umenunua na unafika nyumbani nguo yenyewe hujaipenda.

Ni lazima wewe uwe na ulinzi mkubwa kwenye fedha zako, la sivyo utajikuta unampatia kila mtu na wewe mwenyewe unabaki mikono mitupu.

Kuwa mlinzi imara wa fedha zako, hakikisha unatumia kwenye matumizi ambayo ni muhimu sana.

Kesho nitakushirikisha njia nyingine muhimu ya kuzilinda fedha zako na pia
kuhakikisha na wewe unaziwinda fedha zako mwenyewe.

Mshirikishe mtu na utakuwa umefanya jambo zuri sana.
 
Niwe Mlinzi Madhubuti na Nivutie Za wengine Pia Zije Kwangu. Nimeipenda Lugha uliotumia. Na Selection Ya Mifano. Nashukuru Nimejifunza Kitu Fulani hapo.
 
Back
Top Bottom