Kuwa mfanyakazi kwenye Serikali hii ni zaidi ya mateso

LadyAJ

JF-Expert Member
Oct 21, 2015
7,173
9,631
Hakika nimepatwa na hali ya kukata tamaa isiyo kifani, TAREHE 24/10/2017 tulipata safari ya kikazi kwenda Zanzibar Ku campaign juu ya Bio gas,namna ya kuandaa na kuitumia

1. Baada ya kipindi kirefu cha mkauko wa safari,kwa kweli hii niliifurahia maana nilijua ukame unaanza kupungua

2. Ni Mara ya 2 kwenda Zenji,Mara ya kwanza ilikua ni nyakati za JK tulifikia hotel safi kabisa na starehe kibao + fuko la pesa bank limeshatunishwa

Kimbembe safari hii, fedha za kujikimu unaambiwa utapewa check tena ukirudi eti unakabidhiwa bahasha ya nauli na malazi unaambiwa umeshaandaliwa,haya tukajisemea ngoja twende cha ajabu tunapelekwa kwenda kulala kwenye ki gest kighorofa cha hovyo sana Masingini mkoa wa kaskazini Unguja!?

Kwa kweli kazi ile ya siku 10 ilikua ni zaidi ya ngumu maana hakukua na maana kwetu. Mpaka hii Leo sitamani hata kutia mguu kazini maana sijui nitamuangaliaje msimamizi wangu kwa chuki na ghadhabu nilizonazo.

Hebu serikali ibadilike sasa na kuthamini watumishi maana matokeo mazuri ya kiuchumi huanza na watumishi wa vitengo vyote kufanyakazi kwa moyo na si kwa manung'uniko,ilinibidi nitumie gharama zangu kwenda kulala mjini badala ya kulala kule Amani maana hakukufanana na Mimi
 
hiyo gesti na nyumbani kwako wapi kuzuri???

maana usije iponda gesti mbovu huku unakaa chanika nyumba ambayo haijaisha sakafu vumbi...

hela ya serikali ni ela ya walipa kodi wote hadi maskini vijijini... lazima itumike kwa nidhamu...

sio ya kugawa gawa posho kwa kundi la watu wachache kisa wanaitwa watumishi
 
Mbona kama wewe ni mtu wa kujivuna mkuu?

Mara ooh kule hakufanani nawewe!?
Kwa hadhi yako au sio?

Ulipaswa kusema mazingira yalikua mabaya ila usianze kusema mazingira hayaendani nawewe, hiyo ni lugha ya kujivuna kwamba wewe ni classic sana.

Yangu ni hayo tu, samahani kama nimekukwaza
 
hiyo gesti na nyumbani kwako wapi kuzuri???

maana usije iponda gesti mbovu huku unakaa chanika nyumba ambayo haijaisha sakafu vumbi...

hela ya serikali ni ela ya walipa kodi wote hadi maskini vijijini... lazima itumike kwa nidhamu...

sio ya kugawa gawa posho kwa kundi la watu wachache kisa wanaitwa watumishi
Nyumbani ni nyumbani hata kama vichakani! Elewa kitu kimoja unapomtuma mtumishi kuna stahiki zake lazima umpe ,enyi watanzania msio na mbele wala nyuma acheni mawazo ya wanywa matapu tapu nyie
 
Poleni sana watumishi, binafsi nilishajiapiza ni bora nikaenda vigwaza kukata mkaa kuliko kua mtumishi wa serikali katika ngazi yeyote.
Huijui kesho yako pengine unaweza usiweze nyanyua hata hiyo shoka
 
hiyo gesti na nyumbani kwako wapi kuzuri???

maana usije iponda gesti mbovu huku unakaa chanika nyumba ambayo haijaisha sakafu vumbi...

hela ya serikali ni ela ya walipa kodi wote hadi maskini vijijini... lazima itumike kwa nidhamu...

sio ya kugawa gawa posho kwa kundi la watu wachache kisa wanaitwa watumishi
Jibu mujarabu, walafi kama hawa wanajua pesa ni kwa ajili yao na hawaelewi kuwa ni kwa matumizi ya watanzania wote.
 
Si bora hata unapata safari ya kutalii. Huku kwetu hata mia hupati zaidi yakutumiwa na vitisho vya hali ya juu.
 
Back
Top Bottom