KijanaHuru
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 1,822
- 2,290
Habari ya mchana
Poleni na mapambano dhidi ya cov19, tuendelee kujihami nakutumia wakati tulionao kujiwekea kinga zaidi.
Sasa acha niende katika hoja moja kwa moja,
Tumekuwa ni watu ambao tunaishi kwa kuota ndoto, mbalimbali zakutisha kufurahisha kuhuzunisha napia za kuchekesha.
Huenda ndoto nyingi huwa nikweli katika maisha ya kawaida pia yaweza kuwa kweli katika maisha ya kiroho, yaweza kuwa ni jambo lililopita ama pia ni jambo lijalo.
Leo hii nimeona niandike haya nikutokana na kuwepo wimbi kubwa sana la watu ambao kila leo huweza kutoa tafasiri za ndoto kwa namna zao mbalimbali kwa kadri wanavyojua na kuelewa, lakini katika asilimia 100 za maisha ya ndoto za mwanadamu mara nyingi ni asilimia ndogo sana huwa tunapata ukweli wa kile ambacho tumeweza kukiota.
Jambo la msingi na kubwa nivyema kujua yakuwa Ndoto ni lugha, ya mawasiliano katika ulimwengu wa kiroho, maana huwezi ota ndoto ukiwa upo macho zaidi zaidi yawe ni maono(nitaongelea mbele juu ya maono)
Sasa suala linakuja hivi je Mimi ni Mngoni huyu mkinga kaweze kuelewa maana ya lugha yangu?
Je una uhakika anayekupa hiyo maana anaelewa fika lugha yako ilivyo?
Polepole tu tutaelewana ndugu zangu, ngoja ninawe kujikinga na corona.
Haya naendelea.
Kwanini ujihadhari na wanaotoa tafasiri za ndoto? nikwasababu wengi wao wanajua kusoma hali ya mwongeaji wala sio kujua maana ya kile kimeongelewa
Kwanini nasema hivyo?
Mfano; Mtu yeyote wa lugha yoyote ile duniani akiwa anaongea kwa ukali utajua kabisa anakukalipia ama anakatazia kitu kufuatana na lile utaliona mbele yako, lakini hautaelewa nini anaongea.
Hivyo anayetoa tafasiri ya ndoto atasema unakataziwa ama kuonywa kama jambo ni baya ama atasema unaambiwa fanya haraka kama jambo ni zuri ila hataongea nini maana sahihi ya kile kimeongelewa,, sijui mnanielewa hapo?
Mfano wapili: katika ndoto kuna zile ndoto za ta wanyama wadudu nk ka ulimwengu wa kiroho kila mnyama ama mdudu anakuwa na maana yake ama anakuwa na kitu anachokiwakirisha. Mfano Nyoka mara nyingi huwakirisha mambo kama haya:
1. Mapenzi
2. Usaliti
3. Huruma
4. Upole
5.Subira
6.Usikivu nk
Hayo ni mambo vbaadhi tu ambayo watafasiri wengi wa ndoto huweza kuyachukua na kuyaweka katika uhalisia wa ndoto kitu ambacho ni tofauti na ni kinyume kabisa japo kinaweza kuwiana kwa asilimia ndogo sana.
Sasa leo unaweza ota unang'atwa na nyoka lakini mtoa tafasiri akakuambia kuna mchawi anakuwinda ama kuna jambo linakuja utafeli nk
Mwingine anaweza kukuambia jihadhari na mtu uliyenaye katika mahusiano maana anaweza akakusaliti ama kukufanyia jambo lolote jema
Pia unaweza ukaota labda labda nyoka wa kijani anapita mbele yako. Wanaotoa tafasiri kuna mmoja anaweza akakuambia kwamba kuna jambo unataka kulifanya unapaswa kuwa makini au vuta subira kwanza usianze kulifanya nk
Najaribu kutoa kidogo ufafanuzi juu ya misingi ya wanaotoa tafasiri ya ndoto, kwa njia na namna ambayo nitofauti kabisa.
Pia unaweza kutana ana watu ambao wanakupa tafasiri ya ndoto mapema kabisa kabla haujaota ndoto anakuambia ukiota hivi ujue kuna hili nk
Sasa mambo kama hayo inakuwa ni uongo na upotoshaji kwa hali ya juu sana kuliko uhalisia.
Anawezaje kujua lugha yako na maana yake na kabla haujaongea?
NIliwahi kutana na mtoa tafasiri mmoja maarufu sana nikamwambia bibi yangu(Alikwisha fariki mwaka 2008)anaota sana gari(Ambulance) linagonga nyumba, inamtokea mara mbili hata tatu kwa mwaka,
je maana yake nini?
Alichoniambia nilitamani kucheka japo nilikuwa najifunza ikabidi niwe mpole tu,
Lakini yeye bibi aliweza kujua maana ama tafasiri ya ndoto hiyo, Yeye kila akiota gari ya wagonjwa imegonga nyumba basi katika nyumba husika au ndugu wa nyumba husika kunakuwa na msiba ndani ya siku tatu zijazo, aliweza kujua maana ya ndoto hii sababu ya ile kujirudia mara kwa mara.
Lakini pia ukiachilia mbali huyu Bibi yangu jaribu kuangaia katika vitabu vya dini watu walioweza kuota ndoto zilizoandikwa na wakawepo wale wakufasiri ndoto husika,
Unakuta ni ndoto na maana ni vitu viwili tofauti kabisa yaani unapopata maana ndio unaona vinaendana ila pasipo maana hauiwezi kufikiria kabisa kama itakuwa ni hiii ndio maana yake.
Angalia mfano wa ile .......ndoto nyota na mwezi na jua vinanisujudia...... kuna ile ya sanamu pia kuna ile ya miaka saba ya njaa na miaka saba ya shibe.
Ukiangalia hizo ndoto na maana zake nikwamba utaona kuna wimbi kubwa sana lakudanganywa juu ya maana na tafasiri za ndoto kuliko kile ulipaswa kukijua katika uhalisia.
Kwamiaka ya sasa unaambiwa ng'ombe ni ishara ya pepo au roho chafu katika ulimwengu wa ndoto, lakini je ng'ombe anaashiria nini ulimwengu wa roho? yule aliota ng'ombe wanavuka mto mbona hatujaona tafasiri kama ni roho chafu au mapepo?
Sijui tunaelewana hapo kidogo?Usisite kuuliza
Kwahiyo najaribu kwanza kukupa uelewa uone kwamba uwiano wa ndoto na maana haswa tunazotolewa na watu wengi wasio sahihi haswa hawa wanajiita manabii,wachungajii,masheik,waganga wanajimu nk huwa wanapotosha maana.
Sasa utawezaje kujua maana sahihi ya ndoto? Pasipo kudanganywa na kupotoshwa?
Jambo La kwanza na msingi lakujua nikuwa wewe pekee ndie wakwanza unaijua na kuielewa lugha yako, Hakuna mwingine anayejua nini ulichosikia au nini unataka kuongea niwewe wakwanza binafsi unayejua ukweli na uhalisia.
Jambo la pili na la msingi niwewe kuziandika ndoto zako, weka kumbukumbu yakile unachokuwa unakiota andika kumbukumbu zako kwa kile unakuwa unakiota kila siku. Hii itakusaidia kujua na kukumbuka na kuielewa lugha yako ya ndoto
Jambo la tatu hakikisha unajifunza maana yake kiroho yakile unachokuwa umekiona katika ndoto(Main character) mfano umeota nyoka anakukimbiza basi mjue nyoka maana yake kiroho, umeota mbuzi kaingia ndani basi mjue mbuzi maana yake kiroho, umeota nyasi zinaungua basi jua maana ya moto au nyasi kiroho nini humaanisha, (Ukiingia google utapata maana ya viumbe na vitu vingi maana yake kiroho)
Hatua Ya NNE
hapa sasa utaenda kujua maana ya ndoto yako
Ukishamaliza hatua ya tatu unarudi katika uhalisia wa maisha yako kutokana na maana ya mhusika mkuu katika ndoto yako angalia sasa anahusianaje katika maisha yako kwa kuangalia maana husika,
Kaa tulia tafakari polepole ndipo unaichukua na ndoto yako katika maisha yako ya kawaida inaweza kukaa kwa namna gani?
Hiii njia ndio husaidia watu wengi sana kujua m,aana halisi na zikawa kweli katika maisha yao ya kila siku kuliko zile za wale wanaojiita mafundi. Nikweli wapo watu wenye karama zao, lakini huwezi kuwakuta google ama katika mitandao ni kwa nadra sana zaidi zaidi huko utawakuta wanaojua kuhesabu nyota tu.
Ukiwa na swali usisite kuuliza pia kumbuka kujua maana ya ndoto sio lazima uijue kwa siku moja zingine unaweza jua baada ya miaka ama siku kadhaa maana vingine unaandaliwa mambo ya mbele vingine ni mambo yaliyopita ndio maana ni muhimu kuweza kuandika ndoto ili uwe na kumbukumbu sahihi.................
Over