Kuwa makini na unachoilisha akili yako

chief1

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,415
1,409
Hello all,

Natoa maada kwa lengo mahsusi la kuwapa mbinu ya kuepuka baadhi ya mambo au tabia ambazo wengi zinawatumikisha unwillingly na kuwasaidia kupata mafanikio kwenye mambo mbalimbali.

Kuna hiki kitu, unapokuwa unailisha akili yako umbea kila siku kwenye mitandao ya kijamii na sehemu nyingine yaani wewe lazima uwe mmbeya, roho ya umbea inakuvaa kwa kusoma, kufikiria na kusikiliza umbea kila mara.

Roho kama za uzinzi, ukahaba, ushoga nk zinaweza kukuvaa kwa kupenda kufatilia habari za watu wanaofanya hayo, kumbuka kila kitu unachokiona mwilini kimeanzia rohoni, kila kitu.

Pia kwa upande mwingine unaweza kufanikiwa maishani kwa kusoma au kusikiliza documentary za watu waliofanikiwa kwenye jambo unalotaka kufanya, ile roho iliyowafanya wao wafanikiwe inaweza kukuvaa na wewe

Be careful with what you feed your mind, ukipanda mchicha utavuna mchicha tu.

C.E.O
 
Ndio maana wakristo tunatakiwa kushiba kwa neno la Mungu. neno likikukaa sawasawa hutawaza uzinzi na dhambi. Hutawaza kushindwa wala kufeli na wale ambao wamezoea kusoma biblia kwaajili ya kutafuta tupoint twa kuuponda ukristo, mwisho wa siku hua hua wanakuja kuokoka kwasababu Ile Roho na pumnzi iliyoko kwenye Bible inawalisha kuanzia rohoni. Kwa hiyo kina Fulani waendelee kusoma biblia kumbe wanapanda mbegu pasipo wao kujua
 
This's called spiritual impartation. Kile unachopenda kukifuatilia/kukisikiliza/kukiangalia Mara kwa mara roho yake huja na kukuvamia baada ya muda ile roho inaanza kukuendesha kwa kufanya yale matendo ya kile kitu ulichikuwa ukikifuatilia.
First its becoming as a thought in your mind then after a certain period of time it becomes an action with effect.
 
Inabidi kuwa makini sana na tuna holiday ilia mara kwa mara
Hata kwa watoto wetu, kuwazuilia mambo mengine mfano access ya internet ni muhimu inawasaidia kuwaepushia tabia tofautitofauti
 
Back
Top Bottom