Kuwa Makini, Msimu Wa Wewe Kufilisika Na Wenzako Kutajirika Umefika!!

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,830
23,135
Habari Wana Jamii Forums,.

Simaanishi kitu kingine ila wengi wetu tunafahamu mashindano ya kombe la Dunia yanatarajiwa kuanza rasmi hivi leo!

Tunajua watu wengi ni mashabiki wa damu kabisa na baadhi ya timu zilizofuzu kuingia katika mashindano haya,.

Wengi wao wanafikia hatua ya kuweka rehani mali zao za thamani kama vile magari, nyumba, mashamba au asset yoyote ile yenye thamani kubwa kana kwamba timu yake ikishindwa basi yeye apoteze izo mali au timu yake ikishinda basi yeye achukue mali ya mwenzake waliyowekeana rehani.

Kwa kifupi hii ni kamari kwani kuna kupata na kukosa, kuna watu wengi wameishia kufilisika au kujiua kabisa baada ya kuingia katika mchezo huu wa kamari katika masuala ya michezo.

Wakuu Kombe la Dunia lisitufanye tukapoteza mali zetu au kusambaratisha familia baada ya kupoteza mali nyingi katika mchezo huu wa kamari!!

Nawasilisha,..
 
Back
Top Bottom