mpasta
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 917
- 1,997
Kuna siku nilikuwa nasafiri na ndege ya Alfajiri pamoja na Bosi wangu, sasa pale Airport ghafla tupo foleni kajitokeza jamaa ana kifurushi chake anasema ni magazeti anataka nimsaidie kumbebea mpaka MWANZA kuna mtu atapokea. Nataka kukipokea Bosi akaniambia "Kuwa makini huruma zikizidi zitakuponza". Ikabidi nikatae, baadae akaniambia "binadamu sasa sio wazuri unaweza kubebeshwa mihadarati bure kidagaa kikakuozea". Basi toka siku hiyo nipo makini kweli kweli na huruma za kipumbavu sitaki kabisa.
Sasa leo Stendi ya Mbezi, tupo kwenye foleni ya MWENDOKASI Tunakata tiketi, nimeshuhudia kaja mkaka mmoja amevaa kizibao kama waendesha bodaboda, Kamuomba dada wa mbele yangu kwenye foleni achukue elfu 10 yake akatie tiketi ili apate chenji. Dada ikabidi aweke pembeni elfu 1 yake mkononi akachukua elfu 10 ya jamaa yule.
Wakaka wa kule kibanda cha tiketi walipopokea pesa wakaiangalia wakamwambia hatuna chenji. Ikabidi dada arudishe elfu 10 kwa yule bodaboda akatoa elfu 1 yake. Wale wakaka wakamwambia yule dada ile Pesa uliyotoa mwanzoni ni pesa bandia,tumekuonea huruma tu vinginevyo sasa hivi tungekutia mbaroni.
Dada wa watu akatahayari macho yamemtoka kwa hofu. Nikakumbuka msemo wa BOSI wangu "Huruma zikizidi zitakuponza"