kuwa kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi wilayani rufiji mkoani pwani sio dawa ya kukomesha mauwaji ya

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Siku zote nachukiwa kwa sababu ya ukweli.

Nisaidie ku-share imfikie mwigulu nchemba waziri wa mambo ya ndani.

Mwambieni waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kuwa kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi wilayani rufiji mkoani pwani sio dawa ya kukomesha mauwaji ya kikatili yanayoendelea wilayani humo.

Muda wa kutumia nguvu nyingi kuliko maarifa kwenye vyombo vyetu vya ulinzi umepitwa na wakati ni muda wa wizara hiyo kuangalia upya sifa za watu wanaoajiliwa kwenye jeshi hilo na kuangalia upya mfumo wa mafunzo na kipelelezi pia uendeshaji wa jeshi hilo.

Kwa mfano jeshi la polisi nchini zambia jirani zetu, jeshi lao linatambulika kama (Zambia Police Service) kwa tafsiri ya haraka ni kwamba jeshi la polisi zambia lipo kwa ajili ya kutoa huduma kwa raia kama zilivyo taasisi zingine za serikali kama mabenk n.k,Asilimia 82% ya askari wote ni wanataaluma katika taaluma za sheria,uchumi na information technology (IT).

ZPS huwapeleka nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo ya udukuzi na upelelezi wanataaluma wa IT na sheria wa ndani ya jeshi hilo kwa muda usiopungua miezi 6 na hufanya kila baada ya miaka miwili.Jeshi hilo lipo karibu sana na wananchi na ni kawaida sana kumkuta askari wa zambia na sale zake za kazi akiwa bar akinywa pombe na kufurahi na raia huku wakipiga picha (selfie) ya pamoja na raia, na ndio maana ni ngumu sana nchini zambia kuyasikia matukio kama haya yanayotokea kwetu eti watu wameuwawa na watu wasiojulikana..Watu wanafanyeje mauwaji halafu wasijulikaNE?

Changamoto ya nchi yetu ni kwamba kwanza jeshi letu huitwa (Tanzania police force) wengi wenu mnafahamu maana ya neno force.Neno force ni nguvu hivyo badala ya kutoa huduma lenyewe linatumia nguvu matokeo yake kumekuwa na gepu kubwa kati ya raia na polisi..Leo askari polisi akiingia kanisani,bar au sehemu yoyote yenye kusanyiko akiwa amevaa sale watu wanaingiwa hofu,,Na waoga zaidi huondoka eneo hilo hata kama hao maafisa wa polisi wana shuguli nyingine eneo hilo.Kitu hicho kimefanya maafisa hao kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi ususani matukio yanayotokea mkoani pwani na maeneo mengine.Ni kazi sana kuwajua wahalifu kama jeshi lenyewe halina ushirikiano mzuri na wananchi.

Na kitu hiki cha polisi kutokuwa na mahusiano mazuri au mashirikiano mazuri na wananchi kimepelekea jeshi hili kufanya kazi kwa kukisia na kupiga ramli ya wahalifu waliofanya matukio kuwauwa au kuwakamata na kuwafikisha mahakamani mwisho wa siku jeshi hilo linaenda kushindwa mahakamani kitendo kinachofanya gepu kuongezeka kati ya polisi na raia

Naishauri wizara ya mambo ya ndani kufanya yafuatayo ili kuboresha jeshi letu la polisi na kulifanya liwe la kisasa.

1)kuweka mahusiano mazuri zaidi na ukaribu kati jeshi hilo na wananchi (polisi jamii) hii itasaidia hata jeshi hilo kupata ushirikiano wa kufanya upelelezi wa matukio tata mfano ya kibiti rufiji na maeneo mengine ambayo watuhumiwa hawajulikani.

2)Kutumia mabavu na nguvu nyingi kupunguzwe na badala yake yatumike maarifa mengi na saikolojia namna ya kuwakamata wahalifu na kutawanya makusanyiko yasiyo halali au mikutano ya kisiasa.

3)kutengenezwe sheria ambayo itawadhibiti na kuwaadhibu askari wote wanaobambikiza watu kesi kwa chuki zao binafsi zikiwemo za mapenzi,biashara au kingine.

4)Jeshi la polisi liangalie upya mfumo wa upelelezi ikiwezekana kuufumua na kuunda upya kitaalamu na kisasa,

5)Kama itawezekana wale wanaoomba nafasi katika jeshi hilo angalau asilia 80% wawe wanataaluma wa IT information technology na sheria yani kati ya 1000 ,mia nane wawe wanataaluma wa fani hizo.

6)Ili kukomesha waharifu wasiojulikana wizara itengeneze utaratibu wa kuwapeleka nje ya nchi ususani ulaya askari wapelelezi kwa ajili ya mafunzo maalumu ya matukio ya mauwaji na mengineyo angalau mafunzo ya miezi 6 kwa miaka miwili mara moja.

7)Jeshi letu lijitenge na siasa kabisa na badala yake lijikite kufanya kazi kitaalamu

Nadhani haya yanaweza kupunguza au kumaliza kabisa matukio ya kiuhalifu ususani mauwaji yanayotokea nchini kwetu.

Mwisho kabisa natoa pole kwa familia ya mwanasiasa mwezetu katibu wa ccm aliyeuwawa juzi huko kibiti mkoani pwani kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMEN.

mdude nyagali
sumu ya nyigu.
 
Jeshi polisi likiwa la watu kwa ajili ya watu na likajiepusha kutumika kisiasa, litafanya kazi nzuri sana.

Pia Jeshi linahitaji " analysts" walioenda shule au wenye uzoefu, wenye uwezo wa kusoma trend za mabadiriko ya jamii na kuandaa strategy zenye kuwa updated jinsi ya kudeal na populations time to time. Watanzania wanaokuja watakuwa wengi wenye elimu na wabishi wa haki zao, kwa hiyo huwezi kuwahandle kama ilivyokuwa enzi za Kambarage.

Jeshi litumie tekinolojia sasa, Vijana kwenye vyuo wapo wenye uwezo wa kutengeneza mifumo ya ICT kusaidia kurahisisha utendaji wa jeshi la polisi, Polisi wapunguze Matumizi ya Makaratasi kwenye kutunza kumbukumbu zao za kikazi, Watumie sasa Computer systems ambazo mtandao wake utakuwa umeunganishwa nchi nzima, kiasi kwamba kwa mfano mtu aliyepoteza kitambulisho let say cha mpiga kura, kikiokotwa na taarifa zake kuingizwa kwenye system, mtu akienda kituo chochote cha polisi nchini, anaweza kuelezwa kimeokotwa wapi na kipo kituo gani cha polisi!

Haya ndo miongoni mwa mapinduzi yanayotakiwa kufanywa katika jeshi la polisi.

Mwigulu, Computerise the Police force as a part of reforming the force, itasaidia kutatua mambo mengi sana.
 
Back
Top Bottom