Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?

Wanabodi,

Saa hizi natafuta usingizi unagoma, hivyo nimeshuka jf, tutafakari pamoja kuhusu huu utafiti uliowahi kufanywa na kubaini kuwa kwenye kila Watanzania 4, mmoja ni kichaa!. Jee katika hizo sampling, inawezekana pia kukawa na baadhi ya viongozi wetu wa vyama, taasisi, mashirika, na serikali na taasisi zake?. Huu utafiti ulipotoka sikuuamini niliuona kama umekuwa exaggerated, lakini kadri siku zinavyokwenda na mambo yanavyokuwa, mwenzenu nimeanza kuuamini kwa kujifanyia self diognosis na kukuta ni kweli!. Wewe jiulize jee wewe ni mzima?, na kisha jiulize hivi sisi Watanzania tuu wazima kweli? !. Tufanyeje kuondokana na hali hii?.

93dabf10a9a1ea1c5395c14deb0a409c.jpg

Huu ni uzi wa swali..
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Mtu Aokote Makopo!. Jee Kuna Uwezekano Tanzania Tunao Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.

Kuna msemo usemao kuwa kichaa sio lazima mtu mpaka aokote makopo, ila kwa maneno na matendo ya baadhi ya sisi Watanzania wakiwemo baadhi ya viongozi wetu, wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa vyama vya kijamii, viongozi wa bunge letu, badhi ya waheshimiwa Wabunge, madiwani na viongozi wa serikali za mitaa, nashawishika kabisa kuamini, kuna uwezekano mkubwa, baadhi yao au wengine wetu sio wazima hata kidogo!, kichwani hawana kitu kabisa bali ni vichaa kabisa, ila kwa vile hawaokoti makopo, then hatuwezi kuwajua kuwa ni vichaa!. Kuwa kichaa jameni sio lazima mpaka mtu aokote makopo!.

Hoja hii imetokana na kutafakari kwa makini baadhi ya kauli, maagizo, na maamuzi yetu sisi kama Watanzania na viongozi wetu accross the section, na baadhi kauli na matendo yao yakiwemo maamuzi yao ,amri zao na hatua ambazo wanachukua kudeal na situations mbali mbali zinanithibitishia kuwa badhi ya viongozi wetu sio wazima kabisa upstairs, (kichwani) na mimi mwenyewe mwandishi wa bandiko hili nikiwa not exeptional!, hivyo wanahitaji kusaidiwa kujitafakari badala ya kushangiliwa tuu kwa kila wanachosema na wanachokifanya, hata wakifanya ndivyo sivyo, watashangiliwa tu na kupongezwa! .

Vichaa Viongozi.
Kwa muktadha huo wa ukichaa, ukiwasikiliza matamko wanayotoa baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali, vyama na taasisi hata wa mihimili, na ukafuatilia matendo yao,amri zao na maamuzi yao, utakubaliana na mimi kuwa, sisi Watanzania tuna vichaa wengi zaidi kuliko tunavyo jidhania.

Jee Vichaa Hawa, Wako Katika Makundi Mangapi?.
Vichaa hawa wako katika makundi 5.
Kundi la Kwanza- Hawa ni vichaa wa temporary insanity, au pseudo insanity, ambacho ni kile kichaa watu wengi wanacho hii huletwa na stress na hasira, au kuchanganyikiwa tuu kwa muda mfupi, ukitulia kinakwisha.
Kundi la Pili- ni la lunatics ambao hawa wanaenda na mwezi, au unaitwa wazimu, mwezi ukiwa nchanga, kinapanda, mwezi mpevu kinatulia, kama maji kuja na kupwaa, au good moods na bad mood, akiwa kwenye bad mood ni kichaa ni kama kichaa lakini kikawaida yuko completely sane.
Kundi la Tatu -ni la wale wanaojitoa ufahamu, hili lina wanaume wachache sana, majority ni wanawake waliokwisha pita menopause. Hawa huwa wanajisemea chochote kile bila aibu. Kundi hili pia linawahusisha watu wote wenye msongo wa mawazo, depression, na wote wanaoamua kujiua.
Kundi la Nne -ni la wasema hovyo, wapayukaji, watenda vitendo vya kiajabu ajabu na wale wasiofunzwa na wazazi wao, hili ndilo kundi kubwa kabisa, hadi humu jukwaa, wako wengi kibao, wao ni matusi tu, hata ukiuliza kitu simple kwa nidhamu ya hali ya juu, subiria matusi yatakayoporomoshwa, walio bungeni wanaropoka, waliserikali wanafanya maamuzi ya ajabu, etc.
Kundi la Tano- ni la wale ambao ni certified mental case, hawa ni wagonjwa kabisa na ukichaa wao ni ugonjwa kabisa, hawa sio kosa lao, ugonjwa wa kichaa ni kama ugonjwa mwingine wowotw, tusicheke ugonjwa.

What to do to help out.
Mtu kichaa kwa kawaida huwa hajitambui, wala hajijui kuwa yeye ni kichaa mpaka atakapojulishwa ukichaa wake, na kujitafakari, ndipo atajigundua na kubadilika. Namna ya kuwasaidia viongozi wetu hawa vichaa kujitambua, ni pale wanapotamka matamshi ya kiendawazimu, au kutoa maamuzi ya kiendawazimu, badala ya kuwashangilia wazomeeni ili wazinduke na wajitambue.

Kitendo cha viongozi hawa kutoa matamshi ya kiendawazimu na maamuzi ya kiajabu ajabu na sisi tukiwashangilia badala ya kuwakemea au kuwazomea, hakuwasaidd, na hakutusaidii, na badala yake, kunapelekea wote kuonekana ni vichaa!.

Hivi kweli Tanzania tumefika hapa kuwaacha vichaa hawa kufanya ukichaa wao huku sote tukishangilia tuu bila kukemea, jee sote ni vichaa au kuna wenzetu wameisha jitambua, na wanaona tofauti na wanaweza kusaidia ili tubadilike?. Kama moja ya sifa za kuwa kiongozi wa kuchaguliwa, ni pamoja na kuwa na akili timamu, hivi huu utimamu unapimwajwe wakati tukiwashuhudia na maneno na matendo ya kiendawazimu, au ili kuwapima, au iwekwe kabisa kwenye sheria, taratibu na kanuni, moja ya vigezo wa kuwa kiongozi wa ofisi za umma ni pamoja na kupimwa afya ya akili, ili kuepuka kuwa na viongozi vichaa?.

Paskali
Rejea
Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu?

Hivi Kweli Kuna Mtanzania, Mwenye Akili Zake Timamu, Anaweza Kuichagua Tena CCM?!. Kwa Lipi?!.

Escrow: Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!.Tuache Cherry Picking Kutafuta Mbuzi Wa Kafara!.

Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance?
Tuko wengi mimi ni mmoja wapo 'Every body is mad and that the Degree of Madness is measured when Angly'
 
Kuwapata wenye utimamu Wa akili Tanzania ni jambo gumu sana,muundo wa maisha tunayoishi yanapelekea tuzidi kuwa vichaa.
Unaweza kuwa timamu kwny suala A na ukawa kichaa kwny suala B.
 
Mkuu Britanica, pole!. Nimemsikiliza the man is insane!, you can just tell by look, ila kwa sisi ambao tumefanya money transfer, hakuna malipo yoyote ya bima yoyote ku withdraw fedha zako kutoka benki yoyote, Zaidi ya kukatwa tax na kulipia bank charges ambazo zote zinakatwa, toka kwenye hiyo hiyo fedha yako!. Jamaa kasema anatakiwa kulipa bima ya us $ 150 ndipo alipwe.

Insane anatambulika just by look, the way he dresses, and his mode of life.
Dr Shika anahitaji msaada wa kusaidiwa na sio kubezwa.
Pascal.
Hilo halina ubishi Dr shika ni kichaa tena ni kichaa alie ktk hatua mbaya sana.
Inaonekana ana mambo mengi sana yaliyoharibu akili yake na kuwa punguani.
Anahitaji msaada mkubwa wa kisaikolojia kumuweka sawa ili aweze kukubaliana na ukweli.
 
Kichaa utamjuwa kwa matendo yake,yaani huwa hapendi kufata utaratibu uliopangwa isipokuwa hufata hisia zake na huwa anapenda kusifiwa na aongeapo hupenda kutumia nafsi ya kwanza umoja,pia huongeaa jambo Leo then kesho hulikataa.
 
Acha kumuita Mwehu Mtu ambaye humjui! Usije onekana mwehu mwenyewe! Kwanza kwa Elimu yake tu na yako, tayari Mwehu keshajulikana!
Mkuu Pharaoh, hakika wewe uu mmoja wao!. Nimesema, insane, na kusisitiza sio lazima awe kichaa au mwehu. Kama uwehu unapimwa kwa kiwango cha elimu, then for sure hiyo ni dalili!.

Pole.

Paskali
 
Mkuu Pharaoh, hakika wewe uu mmoja wao!. Nimesema, insane, na kusisitiza sio lazima awe kichaa au mwehu. Kama uwehu unapimwa kwa kiwango cha elimu, then for sure hiyo ni dalili!.

Pole.

Paskali
Hapana mzee Pascal, mambo huwa hayaendi hivyo! eti kwa sababu wewe ni mwandishi wa habari, uzungumze kila tukio linalotokea mbele yako! Suala la Huyu Shika lina utata bado, hivyo najua waandishi wengine wengi bado wapo kimya kuandika makala za huyu jamaa kwa sababu kila siku linazuka jipya juu yake!, hivyo bado wanasoma matukio yake na maisha yake ili wafanye judgement na kumuingiza kwenye makala! Kumuita Insane umemaanisha Mwehu, kichaa, Punguani!. Moyo wa Mtu ni kichaka, hivyo tunajua machache mno kuhusu yule jamaa so ni kheri tunyamaze kwanza mpaka mambo yatakapokuwa wazi maana lazima itakuja ijulikane! So usitulazimishe tuamini kitu unachokiamini wewe kwa hizi siku tatu nne tu ulizomjua Mr Shika, unaanza kumtangaza kuwa ni insane, Subira yavuta kheri,
 
Nakubaliana na wewe, tofauti yetu, ni muda, mimi nimeishafanya conclusion hivyo the motive behind ya bandiko lile ni Dr. Shika, asaidiwe. Msaada wa kwanza ni kulindwa dhidi ya over exposure na hadi kuingilia his right to privacy, watu wameingilia hadi chumba chake kikoje.

Wewe unaona it's too soon to judge, tumpe muda atalipa hivyo it's right kuendelea kuitwa bilionea, by now ameisha fanya media interviews 3, hivyo media waendelee?.

Insane anahitaji msaada kusaidiwa, anahitaji msaada toka kwenye jamii zetu na kuwa protected asizidi kuwa exposed.

Media should stay away.

Paskali
 
Kuna msemo usemao kuwa kichaa sio lazima mtu mpaka aokote makopo, ila kwa maneno na matendo ya baadhi ya sisi Watanzania wakiwemo baadhi ya viongozi wetu, wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa vyama vya kijamii, viongozi wa bunge letu, badhi ya waheshimiwa Wabunge, madiwani na viongozi wa serikali za mitaa, nashawishika kabisa kuamini, kuna uwezekano mkubwa, baadhi yao au wengine wetu sio wazima hata kidogo!, kichwani hawana kitu kabisa bali ni vichaa kabisa, ila kwa vile hawaokoti makopo, then hatuwezi kuwajua kuwa ni vichaa!. Kuwa kichaa jameni sio lazima mpaka mtu aokote makopo!.

Hoja hii imetokana na kutafakari kwa makini baadhi ya kauli, maagizo, na maamuzi yetu sisi kama Watanzania na viongozi wetu accross the section, na baadhi kauli na matendo yao yakiwemo maamuzi yao ,amri zao na hatua ambazo wanachukua kudeal na situations mbali mbali zinanithibitishia kuwa badhi ya viongozi wetu sio wazima kabisa upstairs, (kichwani) na mimi mwenyewe mwandishi wa bandiko hili nikiwa not exeptional!, hivyo wanahitaji kusaidiwa kujitafakari badala ya kushangiliwa tuu kwa kila wanachosema na wanachokifanya, hata wakifanya ndivyo sivyo, watashangiliwa tu na kupongezwa! .

Vichaa Viongozi.
Kwa muktadha huo wa ukichaa, ukiwasikiliza matamko wanayotoa baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali, vyama na taasisi hata wa mihimili, na ukafuatilia matendo yao,amri zao na maamuzi yao, utakubaliana na mimi kuwa, sisi Watanzania tuna vichaa wengi zaidi kuliko tunavyo jidhania.

Paskali
Wanabodi,

Kupitia bandiko hili,
Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Naendelea kuuthibitisha ukweli wa bandiko hili,
Kama Habari imeandikwa "Bunge Linajipendekeza?", halafu akaibuka Mhe. Mbunge na kusema mwandishi na gazeti limeandika "Bunge Linajipendekeza". Naomba kuuliza, hivi Mbunge wa aina hii, kweli ni mzima?.

P.

Pascal
 
Mimi nakuombea tu wasikutumie watu wasiojulikana, ila kama watataka hoja utawashinda asubuhi na mapema.....
 
Back
Top Bottom