Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?

Hata kichaa hudhani watu wenye akili timamu ni vichaa huku yeye akidhani ana akili timamu.

Mtu unatafuta usingizi unagoma halafu unaanza kuwaza matamko ya wanasiasa badala ya kuwaza afya yako. Mbaya zaidi hao unaowaza matamko yao wamelala na wake/waume zao wakifurahia maisha.

First priority ni afya yako.
Second priority ni familia yako.
Third priority ni ndugu zako.
Fourth Priority ni taifa lako.
Fifth priority ni dunia yako.
Wewe Unazungumza Kuhusu watu kukosa Usingizi, Inaonyesha unakisiakisia tu Kana kwamba Dunia ni Meza na Time zone ni moja. Sio kwamba Kila anayechangia hapa JF awe katika Time zone Moja na wewe, Mimi Unayeniambia Nikalale Nipo Venezuela na Bado sasa ni Mapema Kabisa. Na Ni uhakika gani ulionao Kuwa wewe Priority model yako ndio unit ya Kufuatwa na Kila Mmoja, Je Kama sina Familia, Je Kama sina Ndugu. Na Kama Priority yako ya Kwanza ni Afya yako hebu Kuwa Mkweli Tueleze hapa Ratio ya Uzito wako vs Urefu, Tujue kweli Unajali Afya yako! Au kwa Maneno Mengine Kama kweli wewe Ni Msemaji Ukweli na Unafuata Unachonihubiri? Weka Picha yako hapa Kama haupo Obese, Ntakupa $ 5000 hapa hapa Naapa Mbele za Mungu. Hiyo ni changamoto nakupa thibitisha Usemaji Ukweli wako beste wangu!
Wanadamu Jamani!
 
Hata kichaa hudhani watu wenye akili timamu ni vichaa huku yeye akidhani ana akili timamu.

Mtu unatafuta usingizi unagoma halafu unaanza kuwaza matamko ya wanasiasa badala ya kuwaza afya yako. Mbaya zaidi hao unaowaza matamko yao wamelala na wake/waume zao wakifurahia maisha.

First priority ni afya yako.
Second priority ni familia yako.
Third priority ni ndugu zako.
Fourth Priority ni taifa lako.
Fifth priority ni dunia yako.
Kichaa kimekupanda mpk unampangia cha kuwaza.
 
Wanabodi,
Saa hizi natafuta usingizi unagoma, hivyo nimeshuka jf, tutafakari pamoja, hivi sisi Watanzania tuu wazima kweli? !.

Huu ni uzi wa swali, kuwa
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Mtu Aokote Makopo!. Jee Kuna Uwezekano Tanzania Tuna Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.

Kuna msemo usemao kuwa kichaa sio lazima mtu mpaka aokote makopo, ila kwa maneno na matendo ya baadhi ya sisi Watanzania wakiwemo baadhi ya viongozi wetu, nashawishika kabisa kuamini, kuna uwezekano wengine sio wazima kabisa kichwani ila pia sio vichaa kwa sababu hawaokoti makopo! .

Hoja hii imetokana na kutafakari kwa makini baadhi ya kauli, maagizo, na maamuzi yetu sisi kama Watanzania na viongozi wetu accross the section, na baadhi ya matendo yao yakiwemo maamuzi yao ,amri zao na hatua ambazo wanachukua kudeal na situations mbali mbali zinanithibitishia kuwa badhi ya wenzetu sio wazima kabisa kichwani na na mimi nikiwemo, hivyo wanahitaji kusaidiwa kujitafakari badala ya kushangiliwa tuu kwa kila wanachokifanya, hata wakifanya ndivyo sivyo, watashangiliwa tuu na kupongezwa! .


Vichaa Viongozi.
Kwa muktadha huo wa ukichaa, ukiwasikiliza matamko ya baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali, na ukafuatilia matendo yao,amri zao na maamuzi yao, utakubaliana na mimi sisi Watanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyo jidhania.

What to do to help out.
Mtu kichaa hajijui kama kichaa mpaka atakapojulishwa ukichaa wake, na kujitafakari, ndipo atajigundua na kubadilika. Namna ya kuwasaidia viongozi wetu kujitambua, ni pale wanapotamka matamshi ya kiendawazimu, au kutoa maamuzi ya kiendawazimu, badala ya kuwashangilia wazomeeni ili wajitambue.

Kitendo cha viongozi hawa kutoa matamshi ya kiendawazimu na maamuzi ya kiajabu ajabu na sisi tukiwashangilia badala ya kuwakemea au kuwazomea, kunapelekea wote kuonekana ni vichaa!.

Hivi kweli Tanzania tumefika hapa kuwaacha vichaa hawa kufanya ukichaa wao huku sote tukishangilia tuu bila kukemea, jee sote ni vichaa au kuna wenzetu wanaona tofauti na wanaweza kusaidia tubadilike?.

Paskali
Pasco Nakukubali sana!
 
NIMEKUELEWA PASKALI nami nitoe oni langu.... kichaa anapochekewa bila kukemewa ukichaa hukua na hiongezeka maradufu.. hivyo shime uonapo/usikiapo tendo lolote la ukichaa tulilaani na kulikemea papo kwa hapo ; kwa njia hiyo tunaweza kumpunguzia hali yake ya ukichaa au matendo ya ukichaa ya muhusika.
Utamkemea na kulaan kichaa itasidia nn??

Kichaa ni tayar mgonjwa anahitaji matibabu na sio kukemewa..

Km mdau alivyo sema juu tushaur ktk familia zetu kupima ugonjwa wa akili aisee
 
93dabf10a9a1ea1c5395c14deb0a409c.jpg
Umenena iliyo kweli.
 
Ni mada nzuri sana iliyoletwa na Pasco,ingawa nina mashaka kama itaweza kusurvive hadi kuchao Kabla haijanyofolewa...........

Hata hivyo watu wa kubebeshwa lawama kwa hii dhahama iliyolikumba Taifa hivi sasa kwa kuongozwa na watu 'punguani' ni wale jamaa zetu wa Kitengo......

Wao ndiyo wenye jukumu kubwa kabisa la kupekua background kwa maana ya kufanya vetting ya kila anayestahili kupata nafasi ya juu ya uongozi wa nchi yetu.

Sasa inashangaza mno kuona ilikuwaje jina la huyo jamaa yetu likawa limepitishwa na Kitengo hiko nyeti kinachoaminiwa na Umma wa watanzania kwa weledi wa utendaji kazi wake, wakati dalili zote zinaonyesha kuwa jamaa yetu huyo hayuko sawa upstairs?
 
Tangu tulipopigiwa push ups jukwaani, nilijua kabisa pana tatizo hapako salama lazima dish limeyumba lakini waliamua huyu ndiye, acha tuyashuhudie na mengine mengi yatakayo kuja, alipiga push kanda hiyo hiyo akatamka mambo ya aibu tena mbele ya watoto kanda hiyo hiyo, anaonesha ubabe zaidi akiwa huko na anajua kuwa huko ndipo ashangiliwapo acha awaoneshe wameweza kuzaa na kulea ipasavyo.
 
yule jamaa ambae alisema kuwa "mayalla" maana yake "njaa" ni kichaa namba 1,hasa kwa kauli zake tu utamjua jinsi kiwango cha ukichaa kilivyokuwa kikubwa tanzania
 
48 Reactions
Reply
Back
Top Bottom