Kuwa Balozi ni lazima uwe kada wa chama tawala?

Cheque Number

Member
Nov 1, 2016
25
18
Wakuu salaam!

Kuna jambo ambalo linanitatiza and I real need to know it. Hivi kuwa balozi wa nchi ni lazima uwe kada wa chama kitakachokuwa madarakani? Kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja wa majukumu ya kibalozi na pengine utekelezaji wa ilani ya chama tawala?

Ninauliza hivi kwa kuwa, ingawa sijui/sina experience kwa nchi zingine ila imekuwa ni kawaida kwa huku kwetu kuwa makada wa chama tawala ndio huchaguliwa kuwa balozi ili kuwakilisha nchi katika mataifa mbalimbali.

Nawasilisha
 
Kwa mtazamo wangu na mifano ya nchi zingine kama Marekani nk. Balozi ni LAZIMA akubaliane na SERA na UONGOZI wa ANAYEMWAKILISHA.

Kila nchi ina vigezo vyake.Tuchukulie kama rais Trump sasa baada ya ushindi wake amekuwa na KIBARUA kikubwa kujaza nafasi MUHIMU 4,000 miongoni mwao ni kuchagua mabalozi kati ya wale waliomuuga mkono wakati wa uchaguzi.

Hata kwetu pia si lazima awe KADA ila at least awe mwanachama wa chama kilichoko madarakani.
Maana ni vigumu mtu kuiwakilisha serikali USIOIPENDA.
Maana unaweza KUHARIBU mambo!
Haya ni mawazo yangu binafsi.
 
Ufafanuzi please mkuu...
Balozi ni kama muwakilishi sio tu wa nchi bali pia mtetezi wa sera ya serikali ya Nchi, . ana mamlaka ya kuisemea Nchi hukooo abroad. sasa kwa mfano unamteau LEMA kuwa Balozi wako umoja wa mataifa , halafu aulizwe kuhusu mchakato wa katiba.je atautetea msimamo na sera ya serikal yetu ambayo katiba sio kipaumbele au atatoa povu kwa kuiponda nchi mbele ya wageni kwa kutetea sera za chama chake.
 
Asanteni sana, nimeipenda mfano wako mkuu hahahaaa
 
Asante boss, nimekupata vema

Kwa mtazamo wangu na mifano ya nchi zingine kama Marekani nk. Balozi ni LAZIMA akubaliane na SERA na UONGOZI wa ANAYEMWAKILISHA.

Kila nchi ina vigezo vyake.Tuchukulie kama rais Trump sasa baada ya ushindi wake amekuwa na KIBARUA kikubwa kujaza nafasi MUHIMU 4,000 miongoni mwao ni kuchagua mabalozi kati ya wale waliomuuga mkono wakati wa uchaguzi.

Hata kwetu pia si lazima awe KADA ila at least awe mwanachama wa chama kilichoko madarakani.
Maana ni vigumu mtu kuiwakilisha serikali USIOIPENDA.
Maana unaweza KUHARIBU mambo!
Haya ni mawazo yangu binafsi.
 
Balozi ni kama muwakilishi sio tu wa nchi bali pia mtetezi wa sera ya serikali ya Nchi, . ana mamlaka ya kuisemea Nchi hukooo abroad. sasa kwa mfano unamteau LEMA kuwa Balozi wako umoja wa mataifa , halafu aulizwe kuhusu mchakato wa katiba.je atautetea msimamo na sera ya serikal yetu ambayo katiba sio kipaumbele au atatoa povu kwa kuiponda nchi mbele ya wageni kwa kutetea sera za chama chake.
Umemaliza mkuu.!
 
Balozi hawezi kuwa mtu wa hovyo hovyo
Unamteua mtu kama lema atakwenda kufoka na kupiga piga meza mapokezi katika wizara ya mambo ya nje ya nchi aliopelekwa,kisa kwa nini mmewasiliana na waziri nyumbani,wakati mie ndio nilietafuta watalii
 
Obvious, maana anaenda kuwakilisha serikali iliyopo madarakani na serikalibnibya ccm. Labda katiba ibadilishwe ili kutaja sifa za kuwa balozi.
 
Tanzania tunao majuha wengi sana. Balozi wa nchi hawakilishi serikali anawakilisha nchi. Sasa wanaodhani ukada ni sifa wameteleza kwa upotofu wa fikra zao.
 
Kwa uelewa wangu mdogo, Sio lazima awe kada japo kuwa kada hakumzuii mtu kuwa balozi. Mara nyingi kama sio zote huwa watu wa system. Wenzetu wanatuletea majasusi tena waliokubuhu, angalia Balozi wa Marekani alikuwa Deputy Chief of Staffs Ikulu Marekani, Balozi mstaafu wa UK Diana Melrose naskiaa Spy nguli M16. Hata sisi huwa hivyo, kwa sababu ndio wawakilishi wa Nchi, kila kitu kinachohusu serikali yetu kinaanzia ofisini kwao. Pia ubalozi inakuwa ni namna ya kuwapoza watu waliokuwa katika nafasi za juu ambao hutaki kufanya nao kazi, au wametokea si katika watu utakaofanya nao kazi huku bado wakiwa na nguvu ya kutumika. Wengine pia hutaka kuwaweka watu nje ya influence katika mambo ya kisiasa na pia ni sehemu ya kuwapoza wale waliokosa nafasi mbalimbali ndani ya siasa zetu.
 
Asante mkuu, imekaa vizuri hii
 
Wakuu salaam!

Kuna jambo ambalo linanitatiza and I real need to know it. Hivi kuwa balozi wa nchi ni lazima uwe kada wa chama kitakachokuwa madarakani? Kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja wa majukumu ya kibalozi na pengine utekelezaji wa ilani ya chama tawala?

Ninauliza hivi kwa kuwa, ingawa sijui/sina experience kwa nchi zingine ila imekuwa ni kawaida kwa huku kwetu kuwa makada wa chama tawala ndio huchaguliwa kuwa balozi ili kuwakilisha nchi katika mataifa mbalimbali.

Nawasilisha
Ulitaka wampeleke Lema ili akafanye nini?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom