Kuwa Balozi ni lazima uwe kada wa chama tawala?

Balozi ni mwakilishi wa rais nje ya nchi. Ubalozi wa Tanzania nje ya nchi ni sehemu ya nchi yetu huko nje.

Huwezi kuwa rais unayetoka chama cha CCM halafu mwakilishi wa sera zako na mipango yako ya muda mfupi na mrefu huko nje, awe eti anatoka CUF au CHADEMA.
 
ni lazima au si lazima ndiyo majibu mawili pekee katika swali lako.....
Uuu lazima wa jambo mara nyingi ni swala la kisheria, tena kukiuka inaweza kuwa ni kosa kwa mujibu wa sheria husika...!!!
mimi sijaona hilo swala kwenye katiba yetu ijapokuwa sijasoma kurasa 1/1 tokea uchweo mpaka mawio...labda wanasheria waje kutuambia hata, kama mada hii, si moja ya mada kwenye mitaala yao....

Mimi nadhani hili ni swala lenye Sura ya kihistoria hapa kwetu , na kama wengine wanavyosema juu ya interest (who you going to save/ who you going to represent) ni maswali hata mtu wa kawaida lazima ujiulize kbla ujachagua wa kukuwakilisha..

kifupi sio lazima ndugu, kwa mfano aliyekuwa Madhimu mkuu wa Jeshi, IBRAHIM SHIMBO kama sijakosee jina , amepewa ubalozi baada ya kustaafu kazi....
kwa sheria za nchi yetu hakustahili kuwa mfuasi wa chama chochote cha kisiasa,,, hivyo nadhani hupewa yoyote mwenye uwezo wa kuiwakilisha nchi na atakae fata matakwa ya yeye aliyemchagua...
 
Mkuu ww kasomee masuala ya diplomasia mpk uzeeke lkn kama akina Bulembo (darasa la 7) ambao ni ccm damu hawaja kupatia ithibati huwezi kuwa balozi ng'o!.

Badala kuhangaika kusomea diplomasia chukua kadi ya ccm ukiwa darasa la 3, ili unapo maliza la saba upewe ubalozi.
 
Hii Nchi ya Matamko kama ulizania Raisi huyu alipowaambia ni Raisi wa CDM,CUF,NRA,ACT na Vyama vingine na Watanzania wote zile ni Siasa huyu ni Raisi wa CCM pekee nyie si bado Mnaimani na Lowassa....! mkaneni Mle Matunda ya Nchi maana yeye ndie Shida
 
Back
Top Bottom