Kuvuta/kubwia ugoro ni kitendo cha kizalendo??

BRUCE LEE

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
2,097
2,000
Habari zenu ndugu zangu,ktk pita pita zangu nimefanikiwa kugundua kua kiburudisho cha ugoro kimekua kikitumiwa na wazee watu kwa zaidi ya miaka mia,pia bidhaa hiyo imekua ikitengenezwa kiasili kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe tofauti na viburudisho vingine.kumekua na ongezeko la watumiaji hasa vijana na umri wa makamo ukiacha wazee na hali hiyo imepelekea bei ya bidhaa hiyo kukua from kati ya tsh 30 na 50 mwaka 2000 hadi kati ya 200 na 500 kwa sasa. Pendekezo,kama wahindi wamekua wakizalisha kuberi,pariki,tambuu na manikchandi na kuuza sehem mbalimbali je hatuoni kama kuna haja ya ugoro wetu kupelekwa kwa mkemia mkuu,kupimwa na kuwekea stamp za tbs kisha uuzwe huku na serikali ikijipatia kodi yake? Hatuoni kama kitendo hicho kitachangia kutengeneza ajira from wazalishaji,wasambazaji hadi wauzaji?hebu fikiri kenya wanauza mirungi hadi ulaya na serikali inapata kodi yake,Rwanda hadi waendesha boda boda za baiskeli wanalipa kodi ya asilimia 20 ya mapato kwa siku, sasa kwanini serikali yetu ina angalia mambo makubwa tu na kusahau haya ambayo niya kizalendo? Ahsanteni sana kwa heshma na taadhima naomba kuwasilisha hoja hii.
 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
1,195
Ugoro? Unataka vijana wetu waoze meno, sio? Kama kuozesha meno ni uzalendo, mimi simo!
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
18,466
2,000
Kitendo cha kufananisha ugoro na vitu jamii ya madawa ya kulevya, kwa maoni yangu ugoro unaondolewa sifa ya kuwa bidhaa halali kwa walaji.
 

Percival

JF-Expert Member
Mar 23, 2010
2,652
2,000
Ugoro si mzuri kiafya , Nchi nying upo ugoro lakini utengenezaji wake tofauti. US kuna tumbaku ya kutafuna. Tafuta kingine kuendeleza lakini sio ugoro au tumbaku sababu siku hizi kuna muamko unao piga vita hizi bidhaa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom