Kuvunjwa kwa mara ya pili kwa Tawi la CHADEMA la "Ukombozi" Jimbo la Kawe Manispaa ya Kinondoni - Dar es Salaam

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
713
1,241
Leo asubuhi Novemba 6 mwaka 2007 Viongozi wa Vijana wa CHADEMA Jimbo la Kawe Manispaa ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam tulipokea taarifa ya kuvunjwa kwa mara ya pili Tawi la CHADEMA la Ukombozi lililoko katika eneo la Kawe Tanganyika Packers na bendera ya chama chetu kuteremshwa. Tumefika eneo la tukio na kujionea hali hali ya uharibifu uliofanyika. Tunaamini hali hii ni kinyume kabisa na misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kwa vyovyote vile vitendo hivi vikiachwa viendelee vitasababisha uvunjifu wa amani. Tumeona tutoe taarifa hii kwa chama chetu na umma wakati huo huo tunaelekea Kituo cha Polisi Kawe kutoa taarifa, kujua hatma ya jalada letu la awali la uchunguzi baada ya tawi hili kuvunjwa na kama itabidi kufungua jalada la pili kwa ajili ya kitendo cha kuvunjiwa tawi letu kwa mara ya pili. Tumeona tutoe taarifa ya kina kuhusu suala hili kwa kuwa hii ni mara ya pili tukio kama hili linatokea katika kipindi kisichofikia mwezi mmoja.

Ikumbukwe kwamba Oktoba 14, 2007 katika kuhitimisha wiki ya vijana ya Taifa na kuadhimisha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere vijana wa CHADEMA mkoa wa Dar es Salaam waliandaa kongamano la vijana wa Jimbo la Kawe la kumkumbuka Nyerere; uzinduzi wa matawi ya vijana na mkutano wa hadhara.

Wananchi wa maeneo ya Tanganyika Packers hususani vijana waliamua kwa hiyari yao wenyewe kufungua tawi la vijana na kujenga kijiwe cha tawi hilo katika eneo lao. Tawi hilo lilipewa jina la Ukombozi Tawi lingine lililofunguliwa ni Tawi la Wakali wa Maamuzi.

Tawi la Ukombozi lilizinduliwa rasmi kwa bendera kupandishwa na Mh. Chacha Zakayo Wangwe, Mbunge wa Tarime. Akifungua Tawi hilo mbele ya hadhara ya wananchi wa eneo hilo, Mkurugenzi wa vijana Taifa alisema wazi kwamba CHADEMA imepokea taarifa kuwa mjumbe mmoja wa serikali za mitaa kwa tiketi ya CCM hataki kuona tawi la CHADEMA katika mtaa wake. Bwana Mnyika aliwajulisha umma kuwa kila chama kwa mujibu wa sheria kina haki ya kufungua matawi na kupeperusha bendera. Bwana Mnyika aliendelea kumkumbusha mjumbe huyo kuwa Waziri Mkuu Edward Lowasa ametoa kanuni za vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa na kwamba kanuni hizo zinakataza kiongozi yeyote au kiserikali kuteremsha bendera ya chama chochote cha siasa. Hivyo Bwana Mnyika alitangaza kuwa kama mjumbe huyo atatekeleza azma yake ya kushusha bendera hiyo ya CHADEMA atapambana naye mpaka kieleweke. Bwana Mnyika alisisitiza kuwa anafurahi tawi hilo limeitwa Ukombozi na kwamba linazinduliwa siku ya Nyerere ambaye alipigania ukumbozi. Bwana Mnyika alisema kwamba tawi hilo litaunganishwa moja kwa moja na baadhi ya wabunge wa CHADEMA ili kuendelea kupigania maslahi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Tanganyika Packers ambao kiwanda kimeuzwa lakini toka 1992 wanaendelea kutetea maslahi yao mahakamani. Bwana Mnyika alitangaza wazi kuwa kwa kuwa mahakama ilishasisitisha zoezi la kuwahamisha wananchi mpaka kesi yao ya msingi isikilizwe, wananchi wa eneo hilo wana haki ya kuedelea kuishi kama raia wengine ikiwemo kufungua matawi ya vyama katika maeneo yao. Hivyo bwana Mnyika aliwapongeza kwa uamuzi wao wa sasa kwa kumua kufungua Tawi la CHADEMA.

Jumanne Oktoba 16,2007 viongozi wa CHADEMA wa Tawi la ukombozi walipokea taarifa kuwa walinzi wa eneo hilo walishusha bendera ya CHADEMA na kuvunja kijiwe kilichojengwa na kupeleka mligoti wa bendera hiyo polisi.

Kiongozi wa vijana wa CHADEMA jimbo la Kawe Bwana Msabaha alipokwenda polisi alitaarifiwa kuwa walinzi hao walivunja tawi hilo kwa kuwa CHADEMA ilifugua tawi hilo bila kupata kibali. Hata hivyo mkuu wa kituo hicho alisema wazi kuwa walinzi hao walifanya kosa kwa kuvunja tawi hilo bila kibali cha mahakama wala walau kutoa taarifa polisi. Aliwaomba viongozi wa CHADEMA kuzungumza na wahusika hao kulipa na kumaliza tatizo hilo kwa kuwa ni la kisiasa.

Bwana Msabaha alipokwenda kuzungumza na mkuu wa ulinzi Bwana Swai alisema tawi hili limevunjwa kwa kuwa CHADEMA hawajaomba kibali toka kwake.

Kutokana na maelezo hayo viongozi wa vijana waliamua kwenda makao makuu ya CHADEMA kutoa taarifa. Ujumbe kutoka makao makuu ukiongozwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Bwana Erasto Tumbo; Afisa Mwandamizi Idara ya Sheria. Omari Chitanda na Mkurugenzi wa Vijana CHADEMA-John Mnyika walifika eneo la tukio na kujionea hali halisi.

Ujumbe huo ulimua kwenda polisi Kituo cha Polisi Kawe kufungua jalada kwa ajili ya walinzi hao kukamatwa kwa tuhuma zifuatazo:

a) Kushusha bendera ya chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kinyume na sheria ya vyama vya siasa na kanuni za vyama vya siasa.
b) Kesi ya jinai ya kuharibu mali kutokana na kuvunja kijiwe cha CHADEMA.
c) Madai ya kulipwa fidia ya mali iliyoharibika.


Ujumbe huu ulizungumza kwa kirefu na Mkuu wa Kituo mbele ya maofisa wapelelezi wake. Baadaye mkuu wa kituo akaelekeza wapelelezi wake waende pamoja na viongozi wa CHADEMA katika eneo la tukio kupeleleza hali hali ilivyo. Waliporejea mazungumzo yaliendelea na hatimaye Mkuu wa Kituo alimua kufungua jalada la KW/RB/10773/07 kwa ajili ya shitaka la kuvunjwa kwa Tawi la CHADEMA na bendera kungolewa. Viongozi mbalimbali wa CHADEMA waliandikisha maelezo yao akiwemo Mkurugenzi wa Vijana- John Mnyika, Afisa Mwandamizi Idara ya Sheria- Ali Chitanda, Katibu wa Vijana Jimbo la Kawe- Msabaha na viongozi wa Tawi husika. Mkuu wa Kituo aliwajulisha pia wanaweza kufungua tena tawi la chama na kupandisha bendera kama kawaida wakati uchunguzi unaendelea.

Hoja za ziada na maswali ya kujiuliza:

i) Katika eneo hilo kuna matawi/mashina/vijiwe vya Chama cha Mapinduzi ambayo wananchi wanasema havijawahi kuomba vibali ni kwa nini cha CHADEMA kitakiwe kibali?
ii) Kwa nini toka kijiwe kijengwe Jumapili(Oktoba 14) walinzi hao hawajakivunja mpaka wamesubiri siku tatu baadaye (Jumanne-Oktoba 16) na kukivunja wakati ambapo wakazi wengi wapo makazini.
iii) Kwa nini walinzi mmekuwa askari na mahakimu moja kwa moja? Wmetuhukumu kwamba Tawi la CHADEMA limevunja sheria, wamelikamata na kulipa hukumu ya kulivunja? Kama tawi la CHADEMA lingekuwa limevunja sheria; kwa nini hawakwenda polisi na baadaye mahakamani kupata kibali cha kuvunja?
iv) Kiwanja kinamilikiwa na PSRC, na kuna kesi mahakamani hivyo wananchi wampewa haki ya kuendelea na maisha yao katika eneo hil; vipi kibali cha wananchi kufungua tawi leo kiombwe kwa walinzi wa eneo wa kampuni binafsi (ambao si wamiliki wa kiwanja) hilo kama wanavyotaka?
v) Kwanini wahusika waliovunja tawi la kwanza hawajakamatwa mpaka sasa? Je, jalada la uchunguzi limefikia hatua gain?


Taarifa hii imeandaliwa na:

Msabaha(Katibu wa Vijana wa CHADEMA Jimbo la Kawe)- 0773201079


Kwa maelezo zaidi wasiliana na:


Chionda( Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA Jimbo la Kawe)- 0712273240
 
Huu ni uchokozi tu

Ben sidhani kama ni uchokozi bali ni ulevi wa madaraka!

Ile hali ya kudhani kwamba kama wewe ni kiongozi basi uko juu ya sheria na alimradi uko upande wa chama tawala lolote utakalo lifanya ni sawa!

No wonder Jk kakubaliana na hotuba ya mropokaji Makamba kuwaita wapinzani MAPAKA mbele yake na wageni waalikwa hata toka nchi zanje!
 
Duh,Huu ni upuuzi mtupu.ipo siku watajua watanzania million 37 ndio wenye nchi
 
Tatizo polisi inajiona kama idara fulani ndani ya chama cha mapinduzi.

Wananchi wakichukua sheria mikononi Mwema anajifanya kushangaa, wakati chanzo cha matatizo ni vijana wake.

Anyway, Mnyika pambaneni hadi hatua ya mwisho ya kisheria. Ikiwezekana mmpe taarifa IGP aache kushangaa bali awawajibishe vijana wake.
 
sasa Bendera ya CCM imechomwa, na ofisi ya Chadema kuvunjwa.. yote hii ni sehemu ya demokrasia?
 
Mwanakijiji said:
sasa Bendera ya CCM imechomwa, na ofisi ya Chadema kuvunjwa.. yote hii ni sehemu ya demokrasia?

Mwanakijiji,
mimi nilifikiri nikununua bendera ya CCM na kuamua kuichoma moto hadharani ndiyo DEMOKRASIA.

ikiwa nitamnyanganya mwana CCM bendera yake na kuamua kuichoma nadhani huo unakuwa UHUNI.

zaidi kitendo cha kuharibu mali za CCM/CHADEMA tena kwa kijificha ni UWOGA, WIZI, na UHUNI.
 
Nimekuwa nafuatilia matamshi ya wana CCM kuanzia JK na Makamba dhidi ya wapinzani .Matamshi yao yanaonyesha nia ya wazi ya kutoa manyanyaso kwa Vyama pinzani na Mwema na JK they have to come clean kwa kuwa watu wanaweza kuumizana .Haiwezekani mtu achome bedndera ya CCM ama Chadema ile jambo la kisiasa hapana . Hili lina madhara makubwa baadaye kama Unazi wa U CCM hauta achwa.
 
ohh, nyinyi kila kukicha mnafurahia viongozi wa ccm wakumwagiwa mchanga, wakipigwa mawe, bendera ya ccm kuchomwa, lakini na madai yote hayo huwezi kusikia ccm inadai wapinzani ndio wamefanya hivyo ! inakuwaje hapa ?
 
kwanza waliofanya hivyo ni kampuni binfasi, so Mnyika nakushauri ungewaandikia barua hao watu na sio kuleta CONFUSION ndani ya forum !
 
sasa Bendera ya CCM imechomwa, na ofisi ya Chadema kuvunjwa.. yote hii ni sehemu ya demokrasia?

vizuri kwa kuona pande zote mbili, sasa tujiulize kwa kufanya hivi tunamnufanya nani ? Jibu mimi Sifahamu, lakini kama madhara yakitokea watakaohadhirika nani WANANCHI WOTE !
 
hapana babu, it doesnt take much kujua kama ni confusion au sio, halafu ukiangalia MANGAPI HUMU FORUM TUMEJUDGE VIONGOZI ukizingatia hakuna prosecutors, majaji n.k ! Mbaya zaidi hakuna hata siku inayopita bila ya kujudge viongozi wetu na kutoa hukumu !

confusion ni "hali" inayoonekana na sio kitu cha kuamuliwa !
 
Back
Top Bottom