MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Inafahamika katika duru za kisiasa, hofu ya kupinduliwa ilipelekea Abeid Amani Karume ambaye alikuwa kiongozi chama cha A.S.P. kuamua kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika iliyokuwa chini ya chama cha TANU ambacho kiliongozwa na Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Inafahamika kabla ya kuungana, kuna wanajeshi zaidi ya 300 wa Tanganyika walikuwa Zanzibar wakiilinda serikali ya Karume ili isipinduliwe. Mpaka sasa Tanganyika imeendelea kuilinda Serikali ya CCM Zanzibar sio kijeshi pekee bali pia kiuchumi na kisiasa.
Muungano huu ulijenga kile kinachoitwa buffer zone ambacho mpaka leo kinawalinda CCM Zanzibar, no matter what.
Kama CUF wanataka kutawala Zanzibar, ni lazima kwanza wafanye kila linalowezekana Muungano uvunjike au udhoofu sana ili kuondoa buffer zone ambayo ni kikwazo kikuu katika harakati zao.
Muungano huu ni kama nyumba yenye watoto ndani ambayo mwenye ufunguo ni Tanganyika. Uimara wa Tanganyika kisiasa na kiuchumi ndiyo afya ya Muungano lakini pia udhoofu wa Tanganyika kisiasa na kiuchumi ndio kiama cha Muungano. Tanganyika kwa sasa ndio inaamua nani aingie ndani ya nyumba au la.
Jumuiya ya kimataifa hata kama ikiweka vikwazo vya kiuchumi kwa Zanzibar itakuwa ni kupoteza muda as long as buffer zone is alive and kicking while in Tanganyika, Its political and economy is flourishing.
Ieleweke pia, Jumuiya ya kimataifa haiwezi kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Tanganyika wakati chaguzi zake na uchumi wake unakubarika katika ofisi za mabepari wa nchi za Magharibi.
Tuliona mwaka 1995 na 2000 ambapo Jumuiya ya Kimataifa iliamua kuweka vikwazo vya kiuchumi Zanzibar baada ya kutokea matatizo kwenye Uchaguzi wa Rais na wawakilishi wa Zanzibar. Vikwazo havikufanikiwa na CCM Zanzibar chini ya Rais Salmin Amour waliendelea kudunda kwa sababu Tanganyika ilibeba jukumu la kuisaidia kiuchumi na kisiasa.
Kwa mazingira ya kisiasa na kiuchumi yalivyo, watakaovunja muungano au kuudhoofisha sana siyo Wazanzibari bali Watanganyika. Kelele za CUF kwa CCM Zanzibar ni kama debe tupu!
Kama CUF wanataka kutawala Zanzibar, wanapaswa kwanza wawashawishi Watanganyika ili wauvunje Muungano au waudhoofishe sana. Kinyume cha hivyo, wataendelea kuiona kwa mbali Ikulu ya Zanzibar.
Mwandishi wa Kimarekani, Monica Johnson aliwahi kuandika, ‘’You recognize the truth because sometimes it's hard to swallow, but if you hold it in your mouth, refusing to eat it, you are going to choke’’.