Kuvunjika kwa Mo’Hits: Vita vya maneno kati ya D’Banj na Don Jazzy vyapamba moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuvunjika kwa Mo’Hits: Vita vya maneno kati ya D’Banj na Don Jazzy vyapamba moto

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Kabota, Apr 18, 2012.

 1. Kabota

  Kabota Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 15, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  • [FONT=&amp]Madeni ya Mo’Hits utayalipa mwenyewe! – Don Jazzy[/FONT]
  • [FONT=&amp]Utarudisha ile Bentley niliyokununulia?—D’Banj[/FONT]

  [FONT=&amp]Waanzilishi wa lebo ya Mo’Hits ya nchini Nigeria, Don Jazzy na D’banj, wanarushiana maneno ya moto wakati ambao wapo katika mchakato wa kugawana kitega uchumi chao na matunda waliyoyachuma kwa muda mrefu katika lebo hiyo. Barua pepe yenye majibizano baina ya nguli hao wa muziki barani Afrika imenaswa na kufunua yote yanayoendelea kutokana na kuvunjika kwa uhusiano wao.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kama wewe ni miongoni mwa wale watu ambao bado wanadhani kuwa kuvunjika kwa fungate kati ya wahasisi wa Mo’Hits D’banj na Don Jazzy, ni uzushi basi huenda bado unaishi katika muda uliopita. Na tena ili kuufanya muskabali kuwa salama dhidi ya muda uliopita, mafahari hao wawili tayari wameanza kuweka sawa taratibu za kugawana mali zao hasa katika masuala ya umiliki wa lundo la kazi zinazoweza kukufanya utokwe na udenda zikiwemo album za D’banj (No Long Thing, Rundown Funk U Up na The Entertainer), album ya Wande Coal Mushin to Mo’Hits na albam ya nyota wote wa Mo’Hits Curriculum Vitae na nyingine nyingi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hivyo wakati unaendelea kusoma Mo’Hits inasubiri tu uamuzi wa Mahakama kabla haijatangazwa rasmi kuwa imekufa. Na wabebaji wa jeneza tayari wanasubiri katika mstari ili kuyabeba mabaki ya lebo hiyo pendwa nchini Nigeria na kuyapeleka katika makazi yake ya mwisho, hali inayoashiria maliziko liumizalo la lebo hiyo iliyokuwa imefanikiwa sana.[/FONT]
  [FONT=&amp]

  [/FONT] Don-Jazzy-and-Dbanj1.jpg [FONT=&amp]
  [/FONT]

  [FONT=&amp]Wakati huo huo, timu ya Mo’Hits imekuwa ikijigawa wakati ambao nguli wawili wahusikao kwenye mtanange huu wakigawana wafuasi. Mdogo wake na D’banj, K-Switch bila shaka ilikuwa lazima aondoke naye wakati Wande Coal, Dr Sid na D’Prince wakisalia kwenye kambi ya Don Jazzy. Mustakabali wa meneja wa wasanii katika lebo hiyo Sunday Are, haujulikani. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kitambo kabla ya utengano huu kuwa bayana kwa umma, D’banj na Don Jazzy walikuwa hawasemeshani tena[/FONT]

  [FONT=&amp]Hawaonani tena uso kwa uso. Tena, katika tamasha la February mwaka mjini New York walikutana kwenye steji kwasababu kila mmoja alikuwa ana kijichumba chake ndani ya steji moja. Vinginevyo, hawa jamaa huwasiliana kwa e-mail pekee na tena panapokuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Katika email ya siri kati ya marafiki hao wa zamani ambayo ilinaswa na mtandao wa nigeriafilms.com, ukweli usiopendeza na ambao huenda ndio uliosababisha kuvunjika kwa uhusiano wao haujawa bayana lakini mazungumzo yanayohusiana na kudai umiliki wa mali za Mo’Hits husasan kazi za wasanii wote yamewekwa wazi.[/FONT]

  [FONT=&amp]D’BANJ ANAPASWA KULIPA MADENI YOTE YA MO’HITS—DON JAZZY[/FONT]

  [FONT=&amp]Kutokana na dai la D’banj la kutaka umiliki wa asilimia 100 ya nyimbo zote zilizorekodiwa chini ya lebo ya Mo’Hits, producer huyo (Don Jazzy) aliyejizolea sifa barani Africa, katika email iliyotumwa March 17, anasema: [/FONT]

  [FONT=&amp]“Kwamba Mo’Hits Records haimiliki asilimia 100 ya nyimbo. Tambua kuwa Mo’Hits Records inamiliki asilimia 60 pekee ya nyimbo na asilimia 40 zinamilikuwa na wasanii wenyewe. Hivyo, asilimia 40 ya nyimbo si zangu kuweza kuzitoa.[/FONT]
  [FONT=&amp]Anaendelea, [/FONT]
  [FONT=&amp]“Kwamba mimi kumpa yeye (D’banj) share za kazi hakujumuishi na kamwe hakutajumuisha yeye kuwa na haki ya kuwazuia wao (wasanii) kuzitumbuiza nyimbo hizo ama kumpa haki ya kudai pesa zinazopatikana kutokana na kutumbuiza katika matamasha kwa kutumia nyimbo hizi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Na mkopo ama deni lolote linalodaiwa kwa Mo’Hits litalipwa na Bwana D’banj kwakuwa mimi sitambui deni lolote lile .”[/FONT]

  [FONT=&amp]Don Jazzy anaeleza zaidi kuwa kazi anazoziachia kwa partner wake wa zamani zinajumuisha tu nyimbo ambazo zimeshachiwa katika albam na si nyimbo mpya ama nyimbo ambazo hazikuwahi kutoka.[/FONT]
  [FONT=&amp]“Hivyo, nyimbo kama za Wande Coal ambazo ni Go Low na Been Long You Saw Me si sehemu ya kazi hizi anazozipokea. Pia, msanii kama D’Prince, si tu kwamba hajawahi kuachia albam, bali pia hajasaini mkataba wowote ule na Mo’Hits Records. [/FONT]
  [FONT=&amp]“Kwamba hana haki ya kudai pesa zozote kutokana na deal ambazo zimeshazungumzwa na zinazohusu kazi hizo ama kuzuia utumikaji wake”[/FONT]

  [FONT=&amp]Ni muhimu kutambua kuwa nyimbo zozote ambazo hazijatoka na ambazo zimefanywa na msanii yoyote akiwemo D’banj na K-Switch hazitakiwi kuachiwa na si sehemu ya mkusanyiko wa kazi ninazompa”[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Anaongeza,

  [/FONT]

  [FONT=&amp]“Kwa pointi hizi chache, Ninaamini kuwa utatambua kwamba nimekuwa mwema vya kutosha kuwezesha mwisho wa muda wa “D’banj & Don Jazzy kama timu. Baada ya deal hii mpya kusainiwa na kufungwa sitegemei kuona email yoyote ama kusikia jambo kutoka kwa DKM (D’banj, K-Switch, Mo’Hits) na yote yatakuwa heri tena.[/FONT]

  [FONT=&amp]UTARUDISHA ILE BENTLEY NILIYOKUNUNULIA?—D’BANJ[/FONT]

  [FONT=&amp]Siku hiyo hiyo D’banj aliijibu email hiyo na kudai, “Kama amesahau (Don Jazzy) huu ndo utaratibu! 50/50—mwandishi wa wimbo/ utayarishaji, ina maana kuwa kwa wimbo X wa msanii Y, asilimia 75 ya utayarishaji inamilikiwa na Mo’Hits na uandishi unagawanwa 25/25 na ushiriki wa uandishi wa msanii mwenyewe. Hivyo ndo ilivyo. Hivyo anaposema asilimia 40 si zake kuzitoa ni kama asilimia 75 kwangu mimi na asilimia 25 kwa kila msanii”[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Anauliza tena,

  [/FONT]

  [FONT=&amp]“Unamaanisha nini kwa kudai kuwa bili yoyote ama mkopo utalipwa na Bwana D’banj? Hilo halitatokea kamwe kwasababu niliiongoza kampuni vizuri. Hivyo kama nikimpa share zangu atakuwa na asilimia 100 ya wajibu wa kulipa deni. Kazi zangu ndo kila kitu kilichofanywa kupitia mfumo wa Mo’Hits na kwa makubaliano ya kawaida tuliyonayo, hiyo inamaanisha kuwa kila kitu nilichorekodi kiwe kipya ama cha zamani ama hata kikiwa classic, iwe beat iliyo na wazo ama wazo bila beats, chochote tulichofanya kama timu na kudhaminiwa na mimi muda wote, basi ni changu.[/FONT]


  [FONT=&amp]Akiendelea, D’banj anaandika,

  [/FONT]

  [FONT=&amp]“Na sasa nataka kuweka sawa kuhusiana nah ii deal ya Samsung! Ningetegemea mpaka sasa kwamba unaelewa kuwa kitendo cha mimi kukaa kimya ni cha wema tu sababu hii ni deal iliyopatikana chini ya Mo’Hits Records, (na ndivyo ilivyo) na ni deal na kipato cha kwanza ulichowahi kuleta kwenye kampuni katika miaka minane.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tuligawana Dola laki moja na nusu za kwanza (karibu shilingi milioni 228 za Tanzania). Lakini baada ya kuchukua dola laki moja na thelathini zingine (karibu milioni 197) na sikusema kitu, hicho ni na kinaweza kuelezewa kama ni wizi! Nilikataa kuwasiliana nao (Samsung) moja kwa moja kwasababu ya heshima yako. Lakini tafadhari usiniite mimi mjinga na acha tuone yupi ni mwema! ” [/FONT]
  [FONT=&amp]
  D’banj anaandika zaidi, [/FONT]


  [FONT=&amp]“Chonde, chonde, ataweza (Don Jazzy) kurudisha ile Bentley (gari) kwasababu nilimnunulia kwa naira milioni 5.2 (milioni 50 na zaidi za kitanzania) zaidi ya gari langu? [/FONT]

  [FONT=&amp]“Na Prince kwamba hakuwa amesaini mkataba lakini amekuwa akifanya kazi na kusainishwa kutokana na alichofanya – nina haki ya kumiliki kazi zake pia – zote zilizorekodiwa, ziwe zimetoka ama la! Hii ni kwasababu hakuna mtu aliyeniuliza kipindi nimemnunulia gari D’Prince kwa Naira milioni 11(LR3/Range) (zaidi ya shilingi milioni 105 za Tanzania) bila kutoa albam yoyote ili tu kuongeza jina la kijana huyu na hiyo imemsaidia! Hivyo, tuseme ukweli, mimi ni mwema zaidi hapa.”[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] dbanj-don-jazzy.jpg [FONT=&amp]
  [/FONT]

  [FONT=&amp]DEAL YA GOOD MUSIC NA MAMBO MENGINE[/FONT]

  [FONT=&amp]Baada ya deal ya GOOD Music kupatikana Don Jazzy alisainishwa kama producer huku D’banj akichukuliwa kama msanii. Kwa jinsi mfumo wa muziki nchini Marekani ulivyo, watayarishaji wa muziki wanatakiwa kusikika tu na si kuonekana. Hivyo inasemakana kwamba Kanye na D’banj na jamaa wengine walikuwa wanatoka na kuwaacha maproducer akiwemo Don Jazzy, jambo ambalo halikumfurahisha.[/FONT]


  [FONT=&amp]Baada ya muda D’banj aliligundua hili na kuamua kumliwaza kwa kumnunulia Bentley na yeye kununua ya kwake. Zaidi ya hapo alinunua nyumba huko Atlanta, kisha akaiwekea vifaa vikali vya studio ili Don Jazzy aweze kufanya kazi zaidi akiwa hapo lakini hilo pia lilimuumiza kwakuwa aliona amezidiwa sana kimafanikio na D’banj.”

  [/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa upande mwingine, inadaiwa kuwa Don Jazzy aliwaambia watu wake wa karibu kuwa sababu ya yeye kutengana na D’Banj ni kutokana na kibuli chake ambacho kilikuwa na madhara kwa wasanii wengine.

  [/FONT]

  [FONT=&amp]Kitambo sana kabla ya kuanzishwa kwa Mo’Hits, Don Jazzy na D’Banj walikuwa marafiki kabla ya kuwa partners na kuvumiliana kutokana na makosa yao lakini umaarufu na pesa vimeufunika uvumilivu wao. Source (Nigeriafilms.com)[/FONT]  Fredrick Bundala aka Skywalker

  Tone Radio-Tz Intends To Connect You To The People Of Sub Saharan Africa And Across The World |Tone Radio-Tz Anywhere You re
   
 2. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Mkuu Don Jazzy huyo jamaa ana hela chafu,nadhani D banj ni kama bwana mdogo tu,,,,,,pamoja na hivo d'banj alikuwa anapata support ya hela kwa don jazzy ili atoke kimziki
   
Loading...