Kuvunja soko la Kariakoo ni upumbavu kabisa...

kama wameweza haribu markiti ya zenj ya zaidi ya miaka 100,sembuse kkoo.........
Hatuna viongozi wenye akili..Yes I said it
 
Ninavyokumbuka mimi ni kwamba, nilivyokuwa mdogo nilisikia habari kwamba soko la Kariakoo lilivyojengwa lilijengwa na "lifespan" ya miaka kadhaa (either that or some technical malfunctions were being spun to that effect), na linaweza kuanguka katika miaka ya 2000's, enzi hizo in the eighties tunaona the year 2000 ni mbali sana.

Katika kujadili swala hili, ningefurahi kuhakikishiwa kwamba kubomolewa kwa jengo hakuhusiani na "lifespan"/ security factor. Kama jengo lina hatari ya kubomoka then it is only sensible to demolish it. Kama tunaweza kubomoa na kutumia space effectively kwa kuweka kikwangua anga hapo, more power, as long as hawatufisadi wananchi.

Good point Kiranga, public building kama lile codes zinasema ' it should last longer' not from economical point of view but also safety. Factor of safety ni kubwa mno.However kama kuna severe corrosion ambazo kwa kweli sijui kama zipo, then life span inapungua kwa kasi sana. generally life span ya jengo kama lile sawa kabisa na common public building zilizojengwa kwa cement ni miaka 100. Mengi kutokana na poor services, violation of use yana drop mpaka miaka 70, still yanakuwa katika status ya kuweza kuwa regenerated (kufufuliwa) na kuongeza tena life span. So is not an issue hapa, I can tell you that jengo liko kwenye order.

mkuu mimi
sio engineer wa majengo but huwa
nakwenda kariakoo almost kila wiki........

Nalijua vizuri hilo jengo ni imara tena imara sana.......
Naaamini linaweza kuishi hata 200 years na zaidi.......

Na usisahau design na teknolojia ya soko la kariakoo ndo hiyo hiyo
ya airport ya mwalimu nyerere.........kwani architect ni huyohuyo.....

Bj amuli alikuwa ana design majengo ambayo ni built to last.......

Kama kariakoo imefikia muda wake,je jengo la crdb lumumba?na mengineyo mengi aliyo design????

Mimi mzazi wangu mmoja ni architect na alishafanya kazi na bj amuli.
From what i know kariakoo ilijengwa mwaka 74.....unaweza
we mwenyewe tazama maghorofa mengi ya town ambayo yalijengwa kwa teknolijia
duni zadi na yamesha last zaidi ya miaka mia moja.....sembuse miaka 30 ya kariakoo????????????

Mr. Boss niko upande wako lakini sijaelewa hoja ni lisivinjwe kwa nini? so far nimeona point chache za traffic jam, na historical sites. unaweza kueleza au kuongeza point nyingine nyingi ili titile ya thread yako iwe imekaa kihoja zaidi na sio kulaizmisha zaidi. I will certainly add points
 
wazee, poleni kama mlikuwa na vibanda kule shimoni, au kama kulikuwa na biashara yoyote mmewaweka wadogo zenu wawafanyie. kwa upande wangu mimi nasapoti asilimia mia moja, wacha tu wavunje, wajenge jengo jipya zuri, habari ya kusema kuwa watu wapumbavu, hii si halali, unawatukana tu kumbe pengine wewe haujaelewa dhamira yao, na kwasababu hauelewei wewe mwenyewe ukawa ndo mpumbavu. kama jengo watakalojenga pale litakuwa bora kuliko jengo la lile soko, au kama litakuwa linaingiza pato au huduma kwa wananchi zaidi ya lile lililopo sasahivi, ni bora wafanye hivyo tu. ila kama wanataka kujenga hotel ya mtu binafsi, au jengo lolote ambalo wananchi hawatafaidika, hapo ndo ningepinga. pamoja na yote, sitawaita wapumbavu, kwasababu sijafanyia utafiti mradi huo.
 
Dhamira ya wao kuvunja soko inaweza ikawa nzuril lakini uzuri wa dhamira hii lazima uwe sensible na acceptable at least kwa common sense ya watu wote.

Je kwa mtazamo wako weka faida za uvunjwaji wa soko la kariakoo kwa Tanzania yetu ya sasa na ya baadae, zungumza in such a way of debating , you may think bila ata kujua wao waliamua nini au walifikiria nini, then I think we will be in a good track, nimemuuliza swali hili hata mtoa maada! jenga hoja!
 
masoko makubwa ya katikati ya majiji yapaswa kuwa ardhini na juu kunafanyika shughuli nyingine tofauti na barabara zinapita na majumba yanajengwa............. hii itasababisha wafanyabiashara wengi wa kutoonekana juu ya ardhi hasa wamachinga n.k. ....................nafikiri hao wachina wakifanikiwa kutujengea jengo moja la aina hiyo hapo kariakoo ndio mtajua kuwa dar hakuna watu! kwa maana litameza, machinga complex zote, wahindi wote, mchikichini yote, manzese yote..............nk.
amini usiamini kuna majiji hapa duniani unaweza kutembea umbali mrefu sana na ukiambiwa kuwa chini eneo lote hilo kuna maghorofa ya kwenda chini hadi gorofa sita ama zaidi na kuna maduka matupu makubwa kwa madogo, kuanzia ya jumla mpaka madogo, mama ntilie mpaka watembeza pweza, washona viatu mpaka kumbi za snema..............

yaani karibu theluthi moja ya wakazi wa jiji watakuwa wanafanya shughuli zao chini ya ardhi............ na wakimaliza shughuli zao wanakutana na sub-way/metro, inawachukua chini kwa chini hadi huko kimara, sijui gongo la mboto nk na kuacha daladala juu ya ardhi zikiwa nyeupe 24/7 .............. na hii ingepunguza sana msongamano juu ya ardhi............. kama ni mawazo kama hayo, mi naunga mkono ujenzi huo mia kwa mia..............
Ni kweli kuwa kama watajenga jengo kubwa la kuweza ku-accommodate watu wengi zaidi, watapunguza tatizo la mahitaji ya sehemu za kufanyia biashara. Japokuwa sio lazima kubomoa soko la Kariakoo.

Vile vile, kama watalijenga katikati ya Jiji, matatizo mengine makubwa zaidi yataongezeka. Nayo ni sehemu za kuegesha magari pamoja na msongamano wa watu na magari. Matatizo hayo mawili ni makubwa, na hakuna miundo mbinu iliyopo inayoweza kuhimili ongezeko hilo.

Vile vile sioni sababu ya kubomoa jengo la soko la Kariakoo na kujenga jingine, sehemu hiyo. Kama wanataka kujenga soko kubwa, ni vyema kutafuta majengo mengine (kama ya NHC) na kuyabomoa ili kuweza kulijenga.

Soko la Kariakoo linachohitaji kwa sasa ni kuwa modernized na sio kulibomoa kabisa. Wanaweza kulikarabati likawa soko la kisasa zaidi na kuongeza uwezo wake wa kuchukua biashara nyingi zaidi, kwa urahisi zaidi na bila kubadili sura yake.

Waliache soko liendelee kuwepo na walipe usasa unaoendana na hali ya kibiashara ya miji mikubwa.
 
Asante mkuu! umegusia hoja ya parking na miundo mbinu mingine. Kwa haraka kama tutahitaji parking then tunatakiwa kuvunja majengo mengine mengi sana, likiwamo kituo cha polisi msimbazi,

barabara za kuingilia hilo soko inabidi ziwe expanded na hii ni bara bara ya msimbazi, Lumumba na uhuru.

sewage systems inabidi ziwe safi kabisa na kuweza ku-accomodate population na activities zote za kisoko, sewage systems mpya ni wazi itabidi iunganishwe na za zamani, which is wrong, haiwezekani ukajenga sewage sytems kubwa ukaenda ku-conncect na zile za zamani ambazo nyingi ni ndogo.

so they will need kujenga separate sewage system kutoka kariakoo mpaka baharini which is not a joke.

So miundo mbinu is the great barrier of this project.

From your point of modernised I could say (just mawazo) wampe mwekezaji atakayeweza ku-pastimulate mahali pale pawe modern kama ilivyo mlimani city. The jengo la soko la public liwe mbali na city center.

Kujengwa kwa soko hili mbali na mji kuta simulate maendeleo ya hilo eneo husika na kuugawa mji katika activities mbali mbali hivyo kupunguza hata misongamano na mji kuwa attractive na msafi
 
Kabisa Mkuu.

Wanatakiwa kuangalia project nzima kwa mapana yanayostahili. Kwasasa barabara ulizozitaja haziwezi hata kuhimili mahitaji yaliyopo. Hivyo ni lazima zipanuliwe kabla hata soko halijapanuliwa na kuwa kama wanavyotaka liwe.

Nina uhakika suala la sewage system mpya na ya kutosha kukidhi mahitaji ya muda mrefu ya soko hilo, lenye uwezo mkubwa zaidi ni tatizo kubwa kuliko hata kulijenga soko lenyewe. Vinginevyo, soko litashindwa kutumika kwa kukosa matoleo ya uchafu.
 
The Boss Unaposema nchi yetu inaviongozi ni matusi nchi yetu hasa katika awamu hii ya mwisho HATUNA VIONGOZI Inabidi tutafute jina lingine kwani ata kuwahita watawala halifahi labda tuwaite Mamluki kwani kuna MAFISADI ingawa wao pia ni MAFISADI WAKO NYUMA YAO HAO NDIO WANAOTOA MAAMUZI KWA MAMLUKI HAWA TEGEMEA LOLOTE KWANI KWAO MUHIMU NI MASLAHI
Nimeshangazwa sana na habari hiii.

Nnimesoma kwenye gazeti la tafakari kuwa soko la Kariakoo limepata mchina anaetaka kulivunja na kujenga jengo lingine hapo hapo la ghorofa 15..........

Nafahamu hii nchi tumeishiwa viongozi wenye akili but this is too much..........

Hivi kuna jengo maarufu Tanzania zaidi ya soko la Kariakoo? Hivi sisi hatuna policy ya ku protect historical sites na historical buildings? Hakuna sheria ya kuzuia upuuzi kama huu? Hivi hawa watu wanamjua hata bj amuli?

Aliye design soko la Kariakoo na Nyerere Airport na jengo la Ushirika (CRDB Lumumba)? Hivi wanajua hata historia ya majengo hayo? Na hivi huo msongamano wa katikati ya jiji watau address vipi wakiongeza ukubwa wa soko? Mara kumi na tano?

Kama kuna mwana JF ambaye ana contacts zenye nguvu anaeweza ku put stop on this non sense naomba please afanye hivyo......

Hivi unaweza vunja 'Empire State Building' kwa sababu ya kujenga jengo lingine refu zaidi? Au unaweza vunja 'The Eifel Tower' kwa sababu unataka jenga mnara mwingine mkubwa zaidi?

Hivi sisi hatujui how history is priceless? Hivi hatuna kabisa viongozi wenye kutumia common sense hapa Tanzania?
 
Kujengwa kwa soko hili mbali na mji kuta simulate maendeleo ya hilo eneo husika na kuugawa mji katika activities mbali mbali hivyo kupunguza hata misongamano na mji kuwa attractive na msafi

Mkuu Wabeloya,
Hili ndilo la maana. Kuvunja hakutapunguza matatizo. Kujenga sehemu nyingine kutachochea maendeleo ya maeneo mengine.
 
Kujenga soko la kisasa ni suala jema kabisa. Lakini siafiki na replacement ya soko la sasa la K'Koo.

Tanzania tunayo ardhi ya kutosha, nafikiri ni vyema wakatafuta eneo jingine kwa ajili la soko la kisasa.
Litatusaidia sana na kupunguza msongamano wa magari kuelekea K'Koo, haitaharibu utaratibu wa soko kuendelea kutoa service au wauzaji kujipatia rizki zao.

Kupandiana magorofa ni kuzuri lakini kunatokana zaidi na uhaba wa ardhi ambao kwetu sisi hatuna shida hiyo.
Naomba Tanzania iheshimu historia. Ijenge miji mipya ktk maeneo ambayo hayajaendelezwa, na kwa mpangilio unayotarajiwa na technologia za kisasa.

Nimeshangazwa sana na habari hiii.

Nnimesoma kwenye gazeti la tafakari kuwa soko la Kariakoo limepata mchina anaetaka kulivunja na kujenga jengo lingine hapo hapo la ghorofa 15..........

Nafahamu hii nchi tumeishiwa viongozi wenye akili but this is too much..........

Hivi kuna jengo maarufu Tanzania zaidi ya soko la Kariakoo? Hivi sisi hatuna policy ya ku protect historical sites na historical buildings? Hakuna sheria ya kuzuia upuuzi kama huu? Hivi hawa watu wanamjua hata bj amuli?

Aliye design soko la Kariakoo na Nyerere Airport na jengo la Ushirika (CRDB Lumumba)? Hivi wanajua hata historia ya majengo hayo? Na hivi huo msongamano wa katikati ya jiji watau address vipi wakiongeza ukubwa wa soko? Mara kumi na tano?

Kama kuna mwana JF ambaye ana contacts zenye nguvu anaeweza ku put stop on this non sense naomba please afanye hivyo......

Hivi unaweza vunja 'Empire State Building' kwa sababu ya kujenga jengo lingine refu zaidi? Au unaweza vunja 'The Eifel Tower' kwa sababu unataka jenga mnara mwingine mkubwa zaidi?

Hivi sisi hatujui how history is priceless? Hivi hatuna kabisa viongozi wenye kutumia common sense hapa Tanzania?

Pamoja na nia njema lakini B.J. Amuli haja-design Nyerere Airport. Hiyo ilikuwa designed na wafaransa ( Aeroport de Paris kama sikosei). Pamoja na haya cha msingi ni kuwa ni ujinga kukazania kujenga maghorofa kariakoo wakati infrastructure imeishelemewa. Tunalalamika foleni lakini tunashindwa kuelewa mchango wa haya maghorofa kwenye tatizo hilo! Ni wakati muafaka umefika kujenga na/au kuboresha centre nyingine badala ya kung'angania kurundika pale alipotuachia mkoloni. Kwa kufanya hivi tunauharibu mji wetu, kuanzia Kariakoo, City Centre, Upanga, Oyster-bay n.k. Tunashindwa nini kujenga cha kwetu ambacho kitapunguza mzigo wa hii CBD yetu iliyochoka?

Amandla........
 
Kwa kuongezea. Si suala la infrastructure peke yake. Kariakoo ilivyo sasa iko accessible na mwananchi wa kawaida aidha kama mchuuzi au mnunuzi. Hiyo Mall wanayotaka kujenga ni waswahili wangapi wataona ndani? This is another nail in the coffin of the mswahili wa Kariakoo. Kuna wakati wakina mama walikuwa wakiuza samaki wa kukaanga sebuleni, leo Kariakoo itabaki kuwa ya wenye fweza na mateja. Street laif baada ya kuingia kiza inakufa. Na usalama wa watu hivyo hivyo.

Amandla......
 
Nadhani THE BOSS ameshindwa kueleweka, tatizo siyo kuongeza ajira au ufanisi wa soko. Tatizo hapa ni tatizo la watanzania kulinda na kujivunia HISTORICAL ARTIFACTS zetu. Soko la kariakoo ni la kipekeee siyo Tanzania tu hata Afrika mzima, na kama soko hili lingekuwa katika nchi zilizoendelea lingekuwa ni LISTED BUILDING, as a historical site. soko hili ni ICON, na si sahihi kulivunja naunga mkono mzee.

haya ni matatizo ya wanasiasa wabovu, warafi na washamba. Binafsi nilisikitishwa hata pale niliposikia DAR ES SALAAM INTERNATIONAL AIRPORT inabadilishwa jina na kuitwa MWALIMU NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT, hakukuwa na hii sababu kabisa, kwa sababu DIA ni BRAND NAME iliyokuwa tayari imeshajizatiti katika hadhi ya kimataifa. leo ni rahisi kwa mtalii au mzawa kununua SOUVENIR yenye nembo ya DIA kuliko hili jina la sasa. kwa sababu it's nonsense to believe that mwalimu appeals to everyone's taste, but DIA was a non-partizan brand name. Jina hili limekuwa pale kwa miaka mingi sana. lakini JUST ONE IDIOT, na eti anaitwa msomi anakuja kuliua hili jina, hawaeleweki wamesoma wapi hawa, wanashindwa hata kutathmini BRAND NAMES. Could anyone estimate the monetary value of DIA as a brand name? kwa upande wangu sijawahi kujua the most popular brand name in tanzania than DIA, U TELL ME.

Na kuongeza tu nyerere ni mwanasiasa pekee wa kitanzania ambaye ameandikwa kuliko mwanasiasa mwingine yeyote yule katika historia ya tanzania. pia maeneo mbalimbali na majengo mengi tu yameitwa jina lake zaidi ya mwanasiasa yeyote yule, hivyo ni vigumu kusahaulika kihistoria. na inashangaza kuona bado tunatoa majengo na tunaua ESTABLISHED BRAND NAMES kama hizi.

Matatizo kama haya yanaua historia, na kuirudisha nchi nyuma, kwani tunapopoteza historical artifacts tunaua sekta muhimu ya utalii. angalia kilichotokea pale serikali yetu iliposhindwa kutunza magofu ya kale kama kumbukumbu ya biashara ya utumwa kule KILWA, BAGAMOYO, PANGANI, MIKINDANI, TABORA, zenji na maeneo mengine. ukiulizwa na mtalii nini kivutio cha utalii ndani ya tanzania tunabakiwa na mbuga za wanyama tu. leo senegal, gambia, ghana na nchi nyingine za west africa zinaingiza watalii wengi kwa sababu ya vitu hivyo, wabongo tunajivunia tembo na panya tu waliopo mikumi. tunasahau kuwa ni vitu kama SOKO LA KARIAKOO ambavyo in years to come, ndivyo vitakuwa vivutio. matatizo tunachagua viongozi washamba, DAMN IT, IT'S A SHAME
 
Naamini uamuzi wa kuvunja na kujenga upya ulifikiwa baada ya kukutanisha vichwa vya wataalam, kufanya utafiti na kufikia muafaka. Jambo kubwa kama hili haliwezi kufanywa hivi hivi bila kuangalia mizani inaelekea upande gani.
 
Ni kweli kunahitajika soko jipya Dar. Lakini itakuwa bora likajengwa Mbezi kunakoyakiwa kujengwa mji mpya kwa sababu kuna barabara zinazojengwa kuelekezwa barabara ya Morogoro tokea Kisarawe na Bagamoyo. Itapunguza pia msongamano wa magari katikati ya jiji. Kariakoo lisivunjwe kwani kihistoria limesanifiwa na Msanifu majengo Mtanzania." Kipende Chako" waliimba western jazz
 
masoko makubwa ya katikati ya majiji yapaswa kuwa ardhini na juu kunafanyika shughuli nyingine tofauti na barabara zinapita na majumba yanajengwa............. hii itasababisha wafanyabiashara wengi wa kutoonekana juu ya ardhi hasa wamachinga n.k. ....................nafikiri hao wachina wakifanikiwa kutujengea jengo moja la aina hiyo hapo kariakoo ndio mtajua kuwa dar hakuna watu! kwa maana litameza, machinga complex zote, wahindi wote, mchikichini yote, manzese yote..............nk.

amini usiamini kuna majiji hapa duniani unaweza kutembea umbali mrefu sana na ukiambiwa kuwa chini eneo lote hilo kuna maghorofa ya kwenda chini hadi gorofa sita ama zaidi na kuna maduka matupu makubwa kwa madogo, kuanzia ya jumla mpaka madogo, mama ntilie mpaka watembeza pweza, washona viatu mpaka kumbi za snema..............

yaani karibu theluthi moja ya wakazi wa jiji watakuwa wanafanya shughuli zao chini ya ardhi............ na wakimaliza shughuli zao wanakutana na sub-way/metro, inawachukua chini kwa chini hadi huko kimara, sijui gongo la mboto nk na kuacha daladala juu ya ardhi zikiwa nyeupe 24/7 .............. na hii ingepunguza sana msongamano juu ya ardhi............. kama ni mawazo kama hayo, mi naunga mkono ujenzi huo mia kwa mia..............
Unachokisema ni sawa lakini UMESHAWAHI KUJIULIZA KWA NINI ASILIMIA KUBWA YA FOLENI ZA MAGARI ASUBUHI ZINAELEKEA POSTA NA KARIAKOO.......???? KWANI TATIZO NI FOLENI JUU YA ARDHI TUU.....??? HATA UKIHAMISHIA FOLENI HUKO CHINI YA ARDHI SHIDA ITAKUWA PALE PALE TU......... CHA MSINGI NI KUTAWANYA MASOKO MJI MZIMA. KAMA KILA MTU MAHALA ALIPO ANAPATA MAHITAJI YAKE YOTE, HATAKUWA NA SABABU YA KUINGIA KATI KATI YA MJI............. WAKAJENGE KINYEREZI-KIFURU.....KUPO WAZI...............
 
Zinavunjwa stadiums itakuwa jengo chafu & poor architects la Kariakoo? sioni landmark yeyote pale zaidi ya uchafu tuu...sehemu ile kuwa na structure kama ya sasa ni waste of space.
 
Huyo aliyeamua amesahau kuwa vitu vyote vinavyouzwa kariakoo vinatoka mikoani na hatuna barabara za kuingia kariakoo? hayo malori yatapita wapi? Kuna kiwanja kimenunuliwa kwa ajili ya kujenga soko kule mbezi luis; kwa nini kisitumike tukapunguza malori yanayoingia mjini?
 
Back
Top Bottom