Kuvunja soko la Kariakoo ni upumbavu kabisa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuvunja soko la Kariakoo ni upumbavu kabisa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Boss, Apr 17, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Nimeshangazwa sana na habari hiii.

  Nnimesoma kwenye gazeti la tafakari kuwa soko la Kariakoo limepata mchina anaetaka kulivunja na kujenga jengo lingine hapo hapo la ghorofa 15..........

  Nafahamu hii nchi tumeishiwa viongozi wenye akili but this is too much..........

  Hivi kuna jengo maarufu Tanzania zaidi ya soko la Kariakoo? Hivi sisi hatuna policy ya ku protect historical sites na historical buildings? Hakuna sheria ya kuzuia upuuzi kama huu? Hivi hawa watu wanamjua hata bj amuli?

  Aliye design soko la Kariakoo na Nyerere Airport na jengo la Ushirika (CRDB Lumumba)? Hivi wanajua hata historia ya majengo hayo? Na hivi huo msongamano wa katikati ya jiji watau address vipi wakiongeza ukubwa wa soko? Mara kumi na tano?

  Kama kuna mwana JF ambaye ana contacts zenye nguvu anaeweza ku put stop on this non sense naomba please afanye hivyo......

  Hivi unaweza vunja 'Empire State Building' kwa sababu ya kujenga jengo lingine refu zaidi? Au unaweza vunja 'The Eifel Tower' kwa sababu unataka jenga mnara mwingine mkubwa zaidi?

  Hivi sisi hatujui how history is priceless? Hivi hatuna kabisa viongozi wenye kutumia common sense hapa Tanzania?
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  ina maana wamekosa sehemu zingine za kujenga soko? waende huko tandika kama vipi!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Wapumbavu hawa.
  Kuna boko,mbagala tegeta kimara ote huko kuna shida ya masoko.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  nasikia hata Ikulu wachina wanataka kujenga mpya pale iwe kama The Forbidden City.. !
   
 5. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  mmmmmmh!
   
 6. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kazi ipooooo
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hii ndo bongo, hakuna viongozi kabisa.hatujakuja endelea chini ya mafisadi ccm
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  jamni kama wantaka kujenga jengo la kisasa wasifanye hivyo?hebu waacheni wajenge jengo la kisasa zaidi.jamani acheni kuwa conservative
   
 9. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  masoko makubwa ya katikati ya majiji yapaswa kuwa ardhini na juu kunafanyika shughuli nyingine tofauti na barabara zinapita na majumba yanajengwa............. hii itasababisha wafanyabiashara wengi wa kutoonekana juu ya ardhi hasa wamachinga n.k. ....................nafikiri hao wachina wakifanikiwa kutujengea jengo moja la aina hiyo hapo kariakoo ndio mtajua kuwa dar hakuna watu! kwa maana litameza, machinga complex zote, wahindi wote, mchikichini yote, manzese yote..............nk.

  amini usiamini kuna majiji hapa duniani unaweza kutembea umbali mrefu sana na ukiambiwa kuwa chini eneo lote hilo kuna maghorofa ya kwenda chini hadi gorofa sita ama zaidi na kuna maduka matupu makubwa kwa madogo, kuanzia ya jumla mpaka madogo, mama ntilie mpaka watembeza pweza, washona viatu mpaka kumbi za snema..............


  yaani karibu theluthi moja ya wakazi wa jiji watakuwa wanafanya shughuli zao chini ya ardhi............ na wakimaliza shughuli zao wanakutana na sub-way/metro, inawachukua chini kwa chini hadi huko kimara, sijui gongo la mboto nk na kuacha daladala juu ya ardhi zikiwa nyeupe 24/7 .............. na hii ingepunguza sana msongamano juu ya ardhi............. kama ni mawazo kama hayo, mi naunga mkono ujenzi huo mia kwa mia..............
   
 10. T

  Tom JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama soko linalojengwa ni kuongeza idadi kubwa ya wafanyabiashara (ajira) na pia kuwa jengo bora lenye miundombinu muhimu basi bora Wachina wafanye hivyo. Ukitembelea hiyo sehemu, kweli utaona umuhimu wa kujenga soko la kisasa lenye barabara bora za kuingizia biadhaa na watu.

  Tatizo ni je tunauwezo wa kusimamia hicho kitu kweli WACHINA wakakijenga? Mchina ni mchuuzi vile vile, usipombana toka mwanzo anaweza akabomoa na akajenga ghorofa moja tu na usijue uwafanye nini maana mikataba ulishasaini. Ukiwauliza watakwambia watajenga tokana na mapato ya soko.

  Naamini mfanyabiashara yeyote toka China akiwa na mkataba wa kujenga upya Kariakoo, basi serikali yake itampa mkopo kiurahisi tu, lakini si lazima kua hizo pesa kweli atazitumia ktk huo mradi.
   
 11. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Si wangebomoa yale majengo ya kariakoo ambayo mengi ni sub standard?
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Tumewachagua sisi wenyewe, na tutawarudisha sisi wenyewe madarakani.
   
 13. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Akili kichwani unachokisema ni sawa lakini kwa nini tuvunje kariakoo? kwa nini lisijengwe jengo jingine mbadala wa kariakoo? mbona katika nchi nyingine duniani miji yote ya kale imeachwa na kujengwa miji mipya kabisa. Kwa mtindo huu hakuna historia itakayohifadhiwa dar hasa kama tukianza kuvunja hadi majengo ya serikali. The idea is good but not for demolition of the current kariakoo structure
   
 14. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wapumbavu haswa? huu msongamano unaoongezeka kila siku katikati ya jiji hawauoni kabisa. Labda kwa kuwa wenyewe wanapita na ving'ora.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hii ndio brand ya leaders tulio nao leo. Hawa ndio viongozi wetu.
  Hivi kwani kujenga lazima uvunje cha zamani?
  Ninaijua Dar ina maeneo mengi ya kujenga kwa nini wavunje soko la kariakoo?
   
 16. kuti kavu

  kuti kavu Member

  #16
  Apr 18, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ni jambo la kushangaza kwa sababu wengi wanaotumia soko la kariakoo sio wakazi wa kariakoo...kwa hiyo ni wazi kama watumiaji wanao ishi maeneo yaliyo mbali na kariakoo wakijengewa masoko huko waliko hawatakuwa na uhitaji wa kufunga safari kuja kujazana hapo kariakoo. Na hivyo tutakuwa tumetatua tatizo la msongamano na pia kulinda heshima ya majengo yetu ya ukumbusho.

  Lakini swali linabaki,huyo alietoa 'mawazo mtindi' kama hayo ya kubomoa soko la kariakoo halifahamu hili wazo la kuwasogezea huduma wana nchi huko waliko ili kupunguza msongamano hapo sokoni kariakoo????

  Au ndo ile wanatengeneza naman nyingine ya ulaji....tunakumbuka ni juzi juzi tu tuliambiwa bora tufe njaa lakini lazima ndege ya raisi na rada zinunuliwe, matokeo yake tumeyaona watu walipiga mamilioni ya hela wakatia mfukoni....nhi yetu bwana,kama kajishamba ka bibi!!
   
 17. C

  Chuma JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  DUH ...ama kweli tumekosa ma"thinkers".....Hizi kelele wadau zinawafikia?
   
 18. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya ni matokeo ya kuwa na viongozi wenye Tamaa, Waongo, wasiowajali Wananchi waliowachagua, na pia....wenye akili za Ki-Taahira. Soko la Kariakoo ni "Historical site"....na pia ni "Land-mark" kwa watu wengi....Hao waChina labda wafanye "renovations" katika soko...lakini sio kulivunja.

  Ndio nakubali panahitajika juhudi kubwa za Usafi pale sokoni Kariakoo....lakini sio kulivunja.
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  hatuna viongozi kabisa............
   
 20. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hakuna haja ya kuvunja Kariakoo...

  Tunachotakiwa kufanya ni kujenga Masoko 6 kama Kariakoo kila Wilaya ya Dar es salaam. Kila Wilaya iwe na Masoko 2....
   
Loading...