Kuvunja kwa sanamu za waliotenda ukatili zidi ya watu weusi kuna saidia kufuta machungu au kujifunza?

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
Baada ya kifo cha George Foyd nchini Marekani kumezua maandamo katika majimbo mbali nchini Marekani. Huku maelfu kwa maelfu wakiandamana kupinga vitendo hivyo nchini Marekani.

Mwitikio kufuatia tukio Hilo nchi mbali za ulaya zikiwa zimeguswa na hatimae kuanza maandamo na zenyewe.

Maandamo maana hayo yakihusishwa na jumbe mbali kama BLACK LIVES MATTER, kauli ya black lives matter inatumia logo hi.
images (44).jpeg


Maandamo haya yamehusishwa na uvunjaji na uondoaji wa sanamu mbali ambazo za watu mashuhuri waliohusika moja kwa moja maonezi ya mtu mweusi, mauaji ya mtu mweusi na ukatili zidi ya watu weusi.

Mfano wa sanamu zilizopata kuondolewa Ni : These confederate statues have been removed since George Floyd's death

images (45).jpeg

Moja ya sanamu hizo Ni pamoja za wakoloni waliotawala Afrika, mfano Ni sanamu iliyo-ondolewa ni Ile ya Mfalme Leopold wa pili aliyetawala DRC Congo na Toka aitawale Congo DRC hakuwahi kufika nchini Congo mpaka anakufa.
Pichani chini sanamu ya Leopold wa pili ikiondolewa.
images (46).jpeg

Pia na sanamu nyinginezo za wakoloni waliotawala Afrika nazo zimepata kutolewa Kama wakina Cecil Rhodes.

Swali la msingi, licha ya kuwepo maandamo haya na utoaji wa sanamu hizi lengo ni Nini haswa?
1: Kukomesha vitendo (Ukatili, utumwa,mauaji, utumwa, ubaguzi) hizi?
2:Kufuta Historia zidi ya watu walioshiriki katika vitendo na kufanya vitendo hivi?
3: Kujifunza zidi ya pandikizi za kale zilizochangia mpaka vitendo hivi kuwepo Hadi Karne ya leo?
4: Au ni namna ya kupoza machungu kwa watu weusi?
 
Back
Top Bottom