Kuvunja Kanuni ili Kusimamia Kanuni: Sitta, Mwakyembe na Chikawe

Kuna Mtu mmoja alikuwa anaoga mtoni, wakati amevua nguo zote na kuzitundika mahala akaja kichaa mmoja akachukua zile nguo na kukimbia nazo, jamaa aliyekua anaoga akamkimbilia akiwa uchi ili azichukue nguo zake toka kwa kichaa huyo, watu wengi waliomwona huko njiani anakimbia uchi wakaenda kuwasimulia jamaa wengine kuwa yule jamaa (alikuwa anaoga) amepata kichaa na anakimbia uchi barabarani. Nadhani ndicho alicho kifanya huyu chikawe hana nia nzuri, lakini Tunisia ni Afrika wala sio zamani na pia Tunisia ina askari kama sisi tu na si ajabu askari wengi kuliko askari wa CCM. Chikawe naye kavunja kanuni kama anataka awaandikie barua ya kuwaonya basi lakini sio kwenye vyombo vya habari hapa anatikisa kiberiti kilichajaa.
 
Back
Top Bottom