Kuvunja ahadi ya kuoa au kuolewa: Sheria inasemaje?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,197
2,000
Haki ya kudai fidia kwa kuvunjwa ahadi ya kuoa/kuolewa (ndoa (Right to damages for breach of promise of marriage)

Kifungu cha 69 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinatoa haki kwa wapenzi kupeleka shauri mahakamani na kudai fidia kutokana na kuvunjwa ahadi ya ndoa. Suala la msingi kuzingatia ni kwamba, hakuna shauri litakalokubalika kisheria kama mdaawa katika shauri hilo wakati wa ahadi alikua na umri chini ya miaka kumi na nane.

Pia, fidia haziwezi kutolewa zaidi ya hasara ambayo ndio dhahiri kwa upande wa mdai ambayo ilitokana na gharama alizoingia wakati wa ahadi hiyo na mambo mengine kama hayo.

Je, ni muda gani umewekwa kisheria kwa ajili ya kufungua madai ya fidia kutokana na kuvunjwa kwa ahadi ya kuoa/kuolewa (ndoa)?

Kifungu cha 70 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinaweka ukomo wa muda wa kupeleka shauri mahakamani kudai fidia za uvunjifu wa ahadi ya ndoa kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu ahadi hiyo ilipovunjwa.

Zawadi za wachumba (Gifts between engaged couples)

Suala jingine la msingi kuzingatia ni zawadi baina ya wachumba. Katika jambo hili, swali la msingi kabisa kujiuliza ni je, zawadi hio ilitolewa na mchumba kwa mwenzake kama rafiki wa kawaida tu au kwa matarajio ya kuja kuwa mke/mume hapo baadae?

Kama zawadi hio ilitolewa kwa lengo la pili, yaani kwa matarajio ya kuwa mume na mke hapo baadae, basi zawadi hio itakua yenye sharti yaani“conditional”. Ila kama zawadi hio ilitolewa na mmoja kati ya wachumba hao kama mtu wa kawaida tu, pasipo sharti, basi zawadi hio itakua ni mali binafsi ya mchumba huyo aliyepewa zawadi hio na inaweza kurudishwa.

Kifungu cha 71 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kinatoa haki ya kurudishiwa zawadi zilizotolewa na mmoja kati ya wachumba hao kwa matarajio ya kufunga ndoa lakini kwa sababu moja au nyingine ndoa hiyo haikufungwa.

Hivyo mtoa zawadi ana haki ya kufungua shauri mahakamani kudai zawadi alizompa mchumba wake arudishiwe kwa kuithibitishia mahakama kua zawadi hizo alitoa kwa sharti la kufunga ndoa (that the gift(s) was conditional on the marriage being contracted) na sio vinginevyo.

Mahakama lazima ijiridhishe kwamba zawadi hizo zilitolewa kwa sharti kwamba wachumba hao wana nia ya kufunga ndoa.

Sababu za msingi zinazoweza kepelekea uchumba kuvunjika;

1. Kutokuweka bayana masuala ya msingi kwa mchumba wako, hasa masuala yale ambayo kimsingi unatakiwa kuyaweka wazi. Mfano; utofauti wa dini na taifa (difference of religion and nationality), ugonjwa wa ulevi (dipsomania), utasa au ugumba (sterility) na kadhalika.

2. Kuvunja makubaliano. Mfano, kama mmoja kati ya wachumba hao anafanya matendo kinyume na maadili na mtu wa tatu (kama kuchepuka – neno lisilo rasmi) au mmoja kati ya wachumba hao anakataa pendekezo la kufunga ndoa kwa muda mrefu pasipo sababu za msingi.

3. Mabadiliko makubwa kutokea kati ya wachumba baada ya kuingia katika uchumba huo ambayo yanahatarisha kufanikisha kufungwa kwa ndoa rasmi. Mfano; uhanithi “impotence”, wazimu/ukichaa “insanity” baina ya wachumba na kadhalika.
 
Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,197
2,000
Ahadi ya kuoa au kuolewa ni nini?

Kama sheria haijatoa definition ya hili, ni sheria inayohusu kitu ambacho hakijaelezwa rasmi.
Hivi kweli na wewe unaweza kuuliza definition ya ahadi ya kuoa kweli? unapomuahidi mtu kumpa kitu flan unakuwa umetekeleza au, ahadi ni pale unaponogewa na urembo wa mwanamke, unamwambia utamuoa badae unakacha. wengine hutumia gia hii ili ampate msichana akishatembea naye tu basi anamuacha, wasichana wengine hawataki tena mapenzi ya kawaida wanataka waolewe tu sasa ukisema tu ntakuoa anakubali usiposema anaona huyu mdanganyifu.
 
Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,197
2,000
Ukimtongoza mdada anakwambia kama utanioa sawa vinginevyo sitaki maana yake tayari yeye mwenyewe ameshaleta maombi kwako kuwa umuoe sasa ni wewe kukubali au kukataa ikitokea umekubali maana yake maombi yake yamekubaliwa hapo sasa badae akimpata mwingine akabadili mawazo basi akaamua kwenda kwa mwingine sasa ni wewe mwanaume kwenda kumfungulia mashtaka kumbuka hizi ahadi nyingi hazina maandishi.
 
Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,197
2,000
Siku hizi mdada akikwambia umuoe kwanza ndio atakubali kuwa naye mwambie aandike kwa maandishi kuwa amekuomba umuoe na endapo hata tekeleza hilo la kuolewa na wewe sheria ichukue mkondo wake, hapa tutakuwa tumebambana, ikitokea anaenda kwa mwingine unaipeleka karatasi mahakamani kama ushahidi
 
Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,197
2,000
Kina dada siku hizi mwanaume akikwambia anataka akuoe na ukimuona anafaa mpe karatasi akuandikie muandikishiane kuwa kwa hiari amekubali atanioa ili akikataa au akibadili mawazo unafungua kesi kupiti hiyo karatasi ya makubaliano mtakuwa mmebambana
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
56,198

Bado hujatoa definition ya kisheria ya ahadi ya kuoa/ kuolewa.

Kwa mfano, kuna tofauti kati ya mtu anayefanya sherehe na kumvalisha mchumba pete na kutangaza uchumba huo magazetini na kanisani na mtu ambaye amekutana na mwenzake siku ya kwanza, akiwa amelewa, akiwa na mshawasha wa mapenzi ya ghafla, akatamka "wewe mtoto mzuri kweli, nataka kukuoa" kabla hata ya salamu.

Sasa, hapo tuseme kwamba hao wawili wote wameahidi kuoa sawa?
 
Hapana, umekaa na msichana kwa kipindi flani ni wachumba mmeahidiana, sio iyo ya ghafla mnatakiwa pawepo na mashuhuda walio waona mkawatamkia wewe au mdada mkawaambia kuwa Mungu akipenda tutaoana wakajua hivyo. huo ndio ushahidi huwa unaenda mahakamani
 
sagaciR

JF-Expert Member
Jun 17, 2017
646
1,000
Haki ya kudai fidia kwa kuvunjwa ahadi ya kuoa/kuolewa (ndoa (Right to damages for breach of promise of marriage)

Kifungu cha 69 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinatoa haki kwa wapenzi kupeleka shauri mahakamani na kudai fidia kutokana na kuvunjwa ahadi ya ndoa. Suala la msingi kuzingatia ni kwamba, hakuna shauri litakalokubalika kisheria kama mdaawa katika shauri hilo wakati wa ahadi alikua na umri chini ya miaka kumi na nane.

Pia, fidia haziwezi kutolewa zaidi ya hasara ambayo ndio dhahiri kwa upande wa mdai ambayo ilitokana na gharama alizoingia wakati wa ahadi hiyo na mambo mengine kama hayo.

Je, ni muda gani umewekwa kisheria kwa ajili ya kufungua madai ya fidia kutokana na kuvunjwa kwa ahadi ya kuoa/kuolewa (ndoa)?

Kifungu cha 70 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinaweka ukomo wa muda wa kupeleka shauri mahakamani kudai fidia za uvunjifu wa ahadi ya ndoa kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu ahadi hiyo ilipovunjwa.

Zawadi za wachumba (Gifts between engaged couples)

Suala jingine la msingi kuzingatia ni zawadi baina ya wachumba. Katika jambo hili, swali la msingi kabisa kujiuliza ni je, zawadi hio ilitolewa na mchumba kwa mwenzake kama rafiki wa kawaida tu au kwa matarajio ya kuja kuwa mke/mume hapo baadae?

Kama zawadi hio ilitolewa kwa lengo la pili, yaani kwa matarajio ya kuwa mume na mke hapo baadae, basi zawadi hio itakua yenye sharti yaani“conditional”. Ila kama zawadi hio ilitolewa na mmoja kati ya wachumba hao kama mtu wa kawaida tu, pasipo sharti, basi zawadi hio itakua ni mali binafsi ya mchumba huyo aliyepewa zawadi hio na inaweza kurudishwa.

Kifungu cha 71 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kinatoa haki ya kurudishiwa zawadi zilizotolewa na mmoja kati ya wachumba hao kwa matarajio ya kufunga ndoa lakini kwa sababu moja au nyingine ndoa hiyo haikufungwa.

Hivyo mtoa zawadi ana haki ya kufungua shauri mahakamani kudai zawadi alizompa mchumba wake arudishiwe kwa kuithibitishia mahakama kua zawadi hizo alitoa kwa sharti la kufunga ndoa (that the gift(s) was conditional on the marriage being contracted) na sio vinginevyo.

Mahakama lazima ijiridhishe kwamba zawadi hizo zilitolewa kwa sharti kwamba wachumba hao wana nia ya kufunga ndoa.

Sababu za msingi zinazoweza kepelekea uchumba kuvunjika;

1. Kutokuweka bayana masuala ya msingi kwa mchumba wako, hasa masuala yale ambayo kimsingi unatakiwa kuyaweka wazi. Mfano; utofauti wa dini na taifa (difference of religion and nationality), ugonjwa wa ulevi (dipsomania), utasa au ugumba (sterility) na kadhalika.

2. Kuvunja makubaliano. Mfano, kama mmoja kati ya wachumba hao anafanya matendo kinyume na maadili na mtu wa tatu (kama kuchepuka – neno lisilo rasmi) au mmoja kati ya wachumba hao anakataa pendekezo la kufunga ndoa kwa muda mrefu pasipo sababu za msingi.

3. Mabadiliko makubwa kutokea kati ya wachumba baada ya kuingia katika uchumba huo ambayo yanahatarisha kufanikisha kufungwa kwa ndoa rasmi. Mfano; uhanithi “impotence”, wazimu/ukichaa “insanity” baina ya wachumba na kadhalika.
Tupia na CASE LAW mkuu kama rejea kwa Tanzania.
 
Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,197
2,000
Hayo maelezo ya hiyo sheria hayajatanabahisha ahadi ya uchumba ni nini.
We we kama wewe una define vipi ahadi ya uchumba/ kumuahidi kumuoa mdada. kila case lazima iwe na ushahidi bila ushahidi hamna kesi. sasa ahadi ya uchuma ikoje na ushahidi wake ni upi, ujue ni trick ndogo sana mwanamke akiwa tu na evidence ambayo utaulizwa na mahakama kama kweli umekubali mahakama ipokee evidence hiyo maana inaweza ikawa ya maandishi au ya mtu aliyekuwepo mkisema na kuahidiana au kukubaliana. etu toa definition ya ahadi
 
Karma

JF-Expert Member
May 20, 2019
22,919
2,000
Sasa wakati huyo mwanaume anaenda kumfungulia mashitaka huyo mwanamke, anakuwa ana mpango wa kumuoa kweli?
Ukimtongoza mdada anakwambia kama utanioa sawa vinginevyo sitaki maana yake tayari yeye mwenyewe ameshaleta maombi kwako kuwa umuoe sasa ni wewe kukubali au kukataa ikitokea umekubali maana yake maombi yake yamekubaliwa hapo sasa badae akimpata mwingine akabadili mawazo basi akaamua kwenda kwa mwingine sasa ni wewe mwanaume kwenda kumfungulia mashtaka kumbuka hizi ahadi nyingi hazina maandishi.
 
Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,197
2,000
Mwanaume akimfungulia mwanamke mashitaka ujue mwanamke amemkacha tayari hapo hamna tena kuoana mwanamke si ameamua kumuacha mwanaume na ku move on, hapo ndio huwa anaenda mahakamani
Sasa wakati huyo mwanaume anaenda kumfungulia mashitaka huyo mwanamke, anakuwa ana mpango wa kumuoa kweli?
 
Karma

JF-Expert Member
May 20, 2019
22,919
2,000
Siku hizi mdada akikwambia umuoe kwanza ndio atakubali kuwa naye mwambie aandike kwa maandishi kuwa amekuomba umuoe na endapo hata tekeleza hilo la kuolewa na wewe sheria ichukue mkondo wake, hapa tutakuwa tumebambana, ikitokea anaenda kwa mwingine unaipeleka karatasi mahakamani kama ushahidi
Sasa ndiyo nini? Basi kumbe dawa ya wanaume ni kukataliwa tu hadi watakapojiongeza na wasiposema kuwa watawaoa hao wanawake wanaowatongoza basi waendelee kutafuta!
 
Karma

JF-Expert Member
May 20, 2019
22,919
2,000
Duuh
Kina dada siku hizi mwanaume akikwambia anataka akuoe na ukimuona anafaa mpe karatasi akuandikie muandikishiane kuwa kwa hiari amekubali atanioa ili akikataa au akibadili mawazo unafungua kesi kupiti hiyo karatasi ya makubaliano mtakuwa mmebambana
 
Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,197
2,000
Sasa ndiyo nini? Basi kumbe dawa ya wanaume ni kukataliwa tu hadi watakapojiongeza na wasiposema kuwa watawaoa hao wanawake wanaowatongoza basi waendelee kutafuta!
Naye mwanaume ni mjanja ukimkataa kama hana ushahidi wa ahadi yenu eitha kwa maandishi ambayo wengi hawafanyi kama commitment kwa mwenza, au ya watu waliwaona wakiwa pamoja kwa muda mrefu na waliambiwa na wahusika kuwa sisi ni wachumba basi ujue hapo atakupeleka tu mahakamani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom