Victoire
JF-Expert Member
- Jul 4, 2008
- 24,137
- 56,590
duh, you can't teach somebody irony!
oooh sure!
duh, you can't teach somebody irony!
oooh sure!
Mkkj kumbe ndo ulivyo!kumbe mkurungezi wa NSSF awajibike why wakati kuna kina;;;;;;;;;;!Pia why tusisubiri uchunguzi kabla ya kumuhukumu Bwana mkubwa wa NSSF?
Wajiuzulu then what?Hata wakijiuzulu hili suala la kuvuja paper halita settle down!Every year paper linavuja ila suala linakuja pale ambapo tunasema to what extent paper limevuja?
Wakijiuzulu watakuja wapuuzi wengine ambao watafanya paper li leak!
Masuala kama haya yanapaswa yashughulikiwe kwa watu kuadhibhiwa vikali sana ili iwe fundisho!
Kila leo viongozi wanajiuzulu and then hamna kitu hii imeshakuwa fasheni
Umesema kweli Kevo, kwa suala kama hili kujiuzulu tu haitoshi......inabidi watu wapelekwe mahakamani na kufungwa. Lakini suala jingine la kujiuliza hawa watu wa baraza la mitihani/wizara wanajua kweli tatizo liko wapi?...manake inawezekana ikawa 'year in year out' tatizo ni lile lile kwa sababu hawajui wapi penye tatizo. Hivi waziri au mkurugenzi wa NECTA wakiulizwa wanaweza kutuambia tatizo liko wapi .....na wanahitaji nini ili kuliondoa isije ikawa hawapewi nyenzo zote wanazohitaji kufanikisha kazi.
Leo imeripotiwa kuwa mtihani wa Mathematics kwa Form IV umehairishwa kufanyika leo kwa sababu umevuja na utafanyika jumatatu ijayo. Hii ni habari mbaya kwa vijana waliojiandaa kufanya mtihani leo kutokana na uzembe wa wizara ya elimu na baraza la mitihani kushindwa kutimiza wajibu wao wa kulinda mitihani.
Hii sio poa na waziri wa elimu anawajibika kujiuzulu akifuatiwa na uongozi wa baraza ili kuruhusu uchunguzi zaidi kwa nini hawa jamaa bado wanatoa mitihani. Utaratibu wa huu wa mithani una walostisha sana vijana ambao wasingeweza kupata hata huo mtihani fake wenyewe.
Inawezekana pia ushindani wa shule uliopo sasa unaweza kuwa ndio kichocheo zaidi kila mtu anataka mtoto wake au shule yake iwe ya kwanza hata kama haina uwezo ukizingatia wasimamizi wa mitihani wako corrupted lazima mtihani uvuje. Lakini hii sio sababu pekee manake na walimu pia wanahusika kuvujisha.
Miaka yote paper inavuja na business as usual sio poa.
You nailed it buddy!Hao wahusika wakuu hawataki tu, kudhibiti hiyo hali. Serikali kama ikitaka jambo lake lifanyike litafanyika tu bila mizengwe wala kupoteza muda.
Hao watayarishaji wa mitihani wanajulikana, wanaoingiza Data kwenye Computer wanajulikana, wachapishaji wanajulikana, wanao hifadhi hiyo mitihani pia wanajulikana. Sasa tatizo liko wapi?
Mbona hatujawahi kusikia kuwa PESA mpya zinazo chapishwa zimepotea?
Siku Serikali itakapo amuwa kuwaadhibu wale wote wanao husika na UFISADI huu, tena kwa adhabu ya kupigiwa mfano, watakao fuwata watatia akili.
Angalieni mfano wa nchi ya China, mafisadi wanawafanya nini. Serikali ijifunze kutoka kwao.
Watoto kuwafutia matokeo ni sawa na kuangalia tulipoangukia, badala ya tulipojikwa. Kwanini tusiannze na Waziri wa wizara husika,baraza la mitiani na ngazi zingine zinazofuatia mpaka kuja kumfikia mtoto ambaye ndio chanzo chetu cha kuwapata hao mafisadi wetu wa elimu.Huu uvujaji wa mitihani uliokithiri lazima wizara itafute namna ya kukomesha nayo ni kuwaadhibu Wale wote wanaosababisha hili litokee,kuwafutia wanafunzi mitihani siyo dawa ktk hili badala yake ni uonevu na kuwanyima haki kwa sababu hana uwezo sana wa kupigania haki yake.nionavyo mimi namna nzuri ya kukomesha hili ni kupata chanzo cha wapi ilikopatikana hii mitihani na kuwawajibisha Wahusika ambao pengine ni walimu ama wasimamizi ama watunga mitihani lakini tukiwa tumedhamiria kuwafahamu inawezekana kabisa kupitia haohao wanafunzi ambao ni watoto waliopotoshwa na watu wazima pengine kwa tamaa ya pesa pamoja na kukosa uadilifu wafutwe kazi pamoja na kushitakiwa ndiyo namna ya kukomesha hii tabia, ukiwafutia watoto mitihani na kuwaacha hawa watu ambao wameshafanya ya kuwa huu ni mradi mwakani wataendelea na mradi wao kama kawaida na kusababisha tena wengine kufutiwa mitihani lakini kwao kwa sababu wako salama zoezi litakuwa endelevu miaka yote...