Kuvuja kwa sauti ya Said Kubenea na Komu na sakata la Viti Maalum CHADEMA

CCM msiwapangie Chadema nini cha kufanya!Mbona mnawataka sana hao wabunge wawepo bungeni?Si mlitaka bunge lenu peke yenu!
Mimi nilijua mtafurahi zaidi kama wakifukuzwa ili mbaki peke yenu!
 
CHADEMA ndiyo madikteta wa kuzuia watu kutumia haki yao ya kikatiba
Katika hotuba zake zote za kampeni, Jiwe hakutaja neno haki wala demokrasia. Kwake yeye havina nafasi kama ilivyo kwa madikteta.
Unaonaje ukiacha unafiki.
 
Usaliti, forgery na kutoheshimu maamuzi halali ya chama havistahili kuvumiliwa.
Chadema ifukuze wasaliti wote kama ilivyofanya kwa akina Silinde, Lijualikali na Lwakatare
 
Habari.

Mwaka jana kulivuja sauti ya wabunge wa CHADEMA Said Kubenea na Anthony Komu wakipanga njama za kumdhuru Boniface Jacob ili hatimae wafanikishe adhima yao ya kumng'oa Freeman Mbowe kwenye uenyekiti wa chama.

Baada ya sauti hizo kuvuja mara moja chama kilitangaza kikao cha dharura cha kamati kuu kuwahoji ili waweze kuchukuliwa hatua kali sana ikiwa pamoja na kufukuzwa CHADEMA.

Matokeo yake baada ya kikao cha kamati kuu hao wabunge walisamehewa na kutakiwa kuomba radhi tu!!!

Kama hali ni hiyo, wabunge wa viti maalum CHADEMA si wauaji na wala hawajatishia kumuuwa mtu yeyote ila wanajaribu tu kutumia haki yao ya kikatiba iweje wafukuzwe CHADEMA?

Kweli kuwa mwanamke CHADEMA ni dhambi kubwa kuliko wapanga mauaji waliosamehewa??

Tusubiri na kuona kesho kikao cha kamati kuu chadema kitaamua nini ,bila shaka Mbowe is going to be tested again na maamuzi tofauti na kufukuza yatamwimalisha ,na maamuzi ya kufukuza hao wanawake itakuwa ni kiss of death kwa Mbowe na CHADEMA kwa ujumla.
Tumia Akili haki ya kikatiba ni pamoja na kufuata Sheria na kuheshimu hiyo Katiba ambayo inakupa Haki Waheshimu Chama chao kwanza
 
Back
Top Bottom