Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,954
- 8,093
Kuvuja damu baada ya kujifungua ni nini?
Kuvuja damu baada ya kujifungua ni hali ya kuvuja damu kupita kiasi kutoka kwenye njia ya mfumo wa uzazi wakati wowote baada ya kuzaa hadi wiki sita baadaye. Takriban asilimia 70-90 ya matukio ya hali hii hutokea wakati wowote katika saa 24 za kwanza baada ya kuzaa. Matukio haya hutokea kwa sababu kizazi (uterus) hakikujikaza vyema baada ya kondo la nyuma (placenta) kutengeka. Mikazo dhabiti ni muhimu ili kuziba mishipa ya damu kwenye shina la kondo la nyuma.
Kuvuja damu baada ya kuzaa ni hali isiyotabirika na ya kasi inayosababisha vifo vya kina mama. Hali hii haitabiriki kwa sababu theluti mbili ya wanawake waliokabiliwa na tatizo hili hawana visababishi vinavyojulikana. (Kiwango hatari cha hali hii hujulikana na madaktari kama hali idiopathiki (idiopathic) ikiwa kisababishi chake hakijulikani.) Katika matukio mengine, wanawake wanaovuja damu baada ya kuzaa huwa na mojawapo au zaidi ya vipengele vya hatari vinavyojulikana.
Takribani wanawake 127,000 kote duniani hufa kila mwaka kutokana na kuvuja damu baada ya leba na kuzaa. Hali hii hujulikana kama kuvuja damu baada ya kuzaa. Hali hii ni kisababishi kikuu cha vifo vya kina mama vinavyohusiana na kuzaa, nayo husababisha robo ya vifo vyote vya kina mama vinavyohusiana na kuzaa. Kila mwaka, visa milioni 14 vya kuvuja damu hutokea wakati wa ujauzito na kuzaa. Hali hii hutokea mara nyingi kwa sababu uterasi haikujikaza vyema baada ya plasenta kutoka.
Kuvuja damu baada ya kuzaa ni hali hatari zaidi inayohitaji matibabu ya dharura, kuvuja damu kupita kiasi kabla ya uchungu kuanza kunaweza kuhatarisha maisha ya mama na mtoto.
Visababishi viwili ambavyo mara nyingi husababisha kuvuja damu katika kipindi cha mwisho wa ujauzito ni privia ya kondo la nyuma (placenta previa)na kutengeka kwa kondo la nyuma(abruptio placenta).
Privia ya kondo la nyuma ni hali ya kondo la nyuma kuwa limeota karibu sana na mlango wa kizazi (cervix) au kuufunikam kabisa mlango wa kizazi. Kwa kawaida, kondo la nyuma hutakiwa kuota mbali kabisa na mlango wa kizazi.
Kondo la nyuma hujitenga mlango wa kizazi(cervix) unapoanza kupanuka wakati uchungu unapoanza. Kutengeka kwa kondo la nyuma (abruptio pacenta) hutokea kondo la nyuma linapokuwa katika pahali pake pa kawaida katika theluthi mbili za juu ya kizazi, lakini imetengeka kabla ya mtoto kuzaliwa.
Visababishi hivi viwili vya kuvuja damu kupita kiasi, humuweka mwanamke mjamzito katika uwezwkano mkubwa wa kuvuja damu kupita kiasi baada ya kujifungua.
Ni kiwango gani cha kuvuja damu kilicho cha “kupita kiasi”?
Kwa kawaida, mama hupoteza kiwango kidogo cha damu wakati wa kuzaa. Mama kwa kawaida hupoteza takriban mililita 150 (kikombe 1), za damu wakati wa kuzaa na baada ya kondo la nyuma kutolewa. Ikiwa kiwango hiki kitazidi mililita 300 (vikombe 2), hali hii inaaminiwa kuwa kuvuja damu kupita kiasi (Mchoro 11.1) Kuvuja damu kupita kiasi hufasiliwa kama kuvuja damu zaidi ya mililita 500. Hata hivyo, kwa wanawake wenye upungufu wa damu, kuvuja damu ya hata mililita 200–250 kunaweza kusababisha kifo. Kwa sababu hiyo, ufasili bora zaidi wa kuvuja damu baada ya kuzaa ni “ kiwango chochote cha kuvuja kinachosababisha hali ya mwanamke kudhoofika na kusababisha dalili za mshtuko unaohusiana na kuvuja damu.”
Uainishaji wa kuvuja damu baada ya kuzaa
Kuvuja damu huainishwa kulingana na wakati wa kuvuja damu baada ya mtoto kuzaliwa, na kisababishi cha kuvuja kwenyewe.
Uainishaji kulingana na wakati wa kuvuja damu:
Kuvuja damu kwa baada ya kuzaa kwa kiwango cha kimsingi(Primary post partum hemorhage) ni hali ya kuvuja damu kupita kiasi inayotokea kati ya tangu kuanza kwa uchungu hadi saa 24 baada ya kuzaa.
Kuvuja damu kwa baada ya kuzaa kwa kiwango cha upili (secondary post partum hemorrhage)(pia huitwa kuvuja damu kwa baada ya mtoto kuzaliwa) hujumuisha kuvuja damu kupita kiasi kwa kati ya saa 24 baada ya mtoto kuzaliwa na wiki 6 baadaye.
Kuvuja damu baada ya kuzaa kunakohusiana na kizazi kutojikaza vizuri
Neno “kutojikaza” linamaanisha “ukosefu wa mikazo ya kimisuli au uwezo wa kujikaza”. Kuvuja damu baada ya kuzaa kunakohusiana na mikazo hutambulika kwa kuvuja damu kupita kiasi kufuatia kizazi kukosa kujikaza vyema baada ya kuzaa, na kuwa laini, legevu na iliyokosa mikazo ya misuli.
Kwa ufasaha zaidi, katika hali ya kuvuja damu inayohusiana na mikazo, misuli ya kizazi haiwezi kujikaza na kuifinya mishipa ya damu ya mama iliyoraruka baada ya kondo la nyuma kutengana na pembezo za kizazi. Mara nyingi kuvuja damu baada ya kuzaa hutokea kwenye sehemu ambapo kondo la nyuma lilikuwa limejibandika hapo awali. Ikiwa misuli ya kizazi haitajikaza kwa nguvu, haitaweza kuifinya mishipa ya damu ili kudhibiti kuvuja damu.
Visababishi vya kuvuja damu kunakohusiana na mikazo
Hali yoyote inayotatiza mikazo ya kizazi huongeza hatari ya kuvuja damu kupita kiasi. (Hali hizi ni kondo la nyuma liliyosalia, mabaki ya tishu za kondo la nyuma, au kuganda kwa damu ndani ya kizazi.) Ikiwa kondo la nyuma limejitenga lakini lingali limebakia kwenye kizazi, hata kama ni kipande kidogo, kizazi hakiwezi kujikaza. Hata kipande kidogo cha kondo la nyuma au donge la damu lililosalia ndani ya kizazi linaweza kufanya kizazi kutojikaza. Kizazi kisipojikaza, mishipa ya damu ya mama itaendelea kuvuja. Mwanamke atapoteza damu haraka.
Tatizo kuu la kuvuja damu baada ya kuzaa ni kuwa huwezi kubashiri ni nani atakayevuja damu kupita kiasi baada ya kuzaa. Hali hii ngumu husababishwa na ukweli kwamba theluti mbili ya wanawake waliokabiliwa na tatizo hili hawana vipengele vya hatari vinavyojulikana. Hivyo basi, wanawake wote wamo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili, Hata hivyo wanawake wenye viashiria vifuatavyo, wanakuwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata hali hii,
Kondo la nyuma lililosalia: Kondo la nyuma au kipande chake kilichosalia kwenye kizazi hutatiza mikazo ya kawaida ya misuli katika sehemu ya plasenta.
Kibofu kilichojaa: Kizazi kimekaribiana na kibofu. Kibofu kikijaa kinaweza kutatiza mikazo ya kawaida ya uterasi katika wakati wote wa leba na baada ya kuzaa.
Usawa wa ujauzito: Mwanamke aliyewahi kupata mimba zaidi ya mara tano. Misuli ya kizazi inaweza kukosa uwezo wa kujikaza kwa udhabiti kwa sababu imejikaza mara nyingi.
Mimba ya mapacha:Ni sharti kizazi kipanuke ili kutoa nafasi ya watoto wawili au zaidi, baada ya kuzaa, kizazii kiliyopanuka sana inaweza kuchukua muda mrefu kabla ya kujikaza kabisa.
Kuwepo kwa maji mengi ya amnion yaliyomzunguka mtoto kuliko kawaida (Polyhydramnios): Kiowevu kingi cha amanioni (zaidi ya lita 3) kinachomzingira mtoto kinaweza kupanua kizazi kupita kiasi kama vile katika mimba nyingi.
Mtoto mkubwa: Mtoto mwenye uzito zaidi ya kilogramu 4.0 anaweza kupanua uterasi kupita kiasi.
Uchungu uliyodumu kwa muda mrefu:Uchungu unapochukua zaidi ya saa 12 , misuli ya kizazi inaweza kuchoka. Muda mrefu wa mikazo hufanya misuli kukosa kujikaza vyema (utepetevu wa kizazi).
Upungufu wa damu kwa mama:Upungufu wa damu unamaanisha ukosefu wa seli nyekundu za damu kufuatia kiwango cha chini cha hemoglobini. Upugnufu wa damu humweka mama katika hatari ya kupata hali ya kuvuja damu baada ya kuzaa, kwa kuwa damu yake haiwezi kuganda haraka kama vile katika mtu asiye na upugnufu wa damu. Kupoteza damu ni hatari mno kwa mtu ambaye tayari ana upungufu wa damu.
Kuvuja damu baada ya kuzaa kunakohusiana na jeraha
Katika kuvuja damu baada ya kuzaa kunakohusiana na jeraha, kuvuja damu kupita kiasi hutokea kufuatia jeraha kwenye njia ya uzazi baada ya mtoto kuzaliwa. Jeraha linaweza kutokea kwenye mlango wa kizazi, uke, periniamu, au kinyeo. Jeraha pia linaweza kuwa kupasuka kwa kizazi .
Kinga
Visa vingi vya hali hii vinaweza kuzuiliwa kupitia utunzaji wa kiustadi wakati wa ujauzito, leba na kipindi kinachofuatia kuzaa.
Wakati wa utunzaji wa kabla ya kuzaa, wanawake wote wajawazito wanafaa kupokea ushauri kuhusu lishe na kinga dhidi ya malaria. Wanawake wote wajawazito wanafaa kupokea matibabu dhidi ya mnyoo. Wanawake hawa pia wanafaa kupokea nyongeza ya virutubishi vya madini ya chuma/foleti ili kuzuia upungufu wa damu.
Vitu vyote hivi hufanywa na wataalamu wa afya katika kliniki za ujauzito. Hivyo basi, ni muhimu sana kwa mama mjamzito kuhudhuria kliniki kadri anavyopangiwa ili kupunguza uwezekano wa kupata hali ya kuvuja damu kupita kiasi wakati au baada ya kujifungua.