Kuvamiwa kwa Ofisi za Mwanahalisi na Polisi

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa gazeti la mwanahalisi limevamiwa muda huu na polisi huku wanaendelea na upekuzi ila hatujui wanataka nini .

Waliwakuta ofisini ndugu Kubenea Said na Ndimara Tegambwagwe pamoja na mlizi ndugu Mayunga.
nitawapa news zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Wanaendelea na upekuzi na itakumbuka kuwa hawa hawa ndio ambao walimwagiwa tindikali na kesi bado inaendelea japo haijulikani nini hatima ya haya mambo , JF members be carefull huenda tunawindana sana na hawa jamaa.
 
Mwana halisi mmiliki ni nani?
RA hana mkono hapo kweli?

Wanaendelea na upekuzi na itakumbuka kuwa hawa hawa ndio ambao walimwagiwa tindikali na kesi bado inaendelea japo haijulikani nini hatima ya haya mambo , JF members be carefull huenda tunawindana sana na hawa jamaa.

Nyie CHADEMA mnaowaambia jf wawe makini na wananchi mtawaambia nini?
Tena jf hapa ambapo watu hata wengi wao hawatumii majina yao?
Ama ni scare tactic?

Hii si ingeunganishwa na hiyo ya Kieleweke ya Mwanahalisi wavamiwa?
Ama macho yangu?

Kabla ya kuwapekuwa hao watu..Je uchunguzi wa shambulizi la kina Kubenea la kumwagiwa tindikali nk polisi wamefikia wapi?

Yani watu washambuliwe na maisha yao yawe hatarini badala ya kulindwa na polisi wanavamiwa na polisi?

Na hao waliowamwagia tindikali si polisi?

Makubwa!
 
Wamechukua computer ambayo anaitumia pamoja na flash na wameondoka naye kwenda kumsachi nyumbani kwake ,na hili lilitokana na kuwa polisi hawa wanatafuta nyaraka fulani na hii huenda ni kwa maelekezo kutoka juu.
 
Do you smell what the rock ic cooking?Kuna habari nadhani hawa majamaa wa Mwanahalisi walitaka kuilipua then mtu akalikisha info.
 
Kuna amri ya mahakama ya kufanya hivyo? la maana ni kuwahi mahakamani (kama inawezekana) nadhani ndio sababu wamevamia late today... lakini kama wana search warrant na kama inawapa uwezo wa kwenda kusearch hadi nyumbani.
 
Upekuzi nyumbani kwake unaendelea na sasa haijulikani nini kinafanyika huko kwani simu yake haipokelewi tena .

Tutawapa yaliyojiri punde.
 
"You can fool some people some time but you can't fool all people all the time", serikali inapaswa kujua hilo!
 
Wamechukua computer ambayo anaitumia pamoja na flash na wameondoka naye kwenda kumsachi nyumbani kwake ,na hili lilitokana na kuwa polisi hawa wanatafuta nyaraka fulani na hii huenda ni kwa maelekezo kutoka juu.

Naweza ku-speculate kwamba Kubenea alitaka kutoa "dataz" za RA ... all the way from Iran.
 
Kuna amri ya mahakama ya kufanya hivyo? la maana ni kuwahi mahakamani (kama inawezekana) nadhani ndio sababu wamevamia late today... lakini kama wana search warrant na kama inawapa uwezo wa kwenda kusearch hadi nyumbani.

Hapo umenena mkuu, na ni hakika kama kweli wamefanya hivyo wametambua kuwa kwa muda huu hakuna uwezo wa kufika mahakamani kwa kazi mwisho saa 9 na kesho ni weekend!! Hali hii mpaka lini? Juzi wameahirisha kesi ya TINDIKALI leo wana m search jamaa tena hadi nyumbani!!! Haki ipo wapi jamani?
Mwenye taarifa zaidi atujuze tafadhali.
 
Kingine cha kujua ni kwamba mara nyingi mtu akishikwa na polisi ijumaa jioni kuanzia saa 11 ni ngumu kutoka kwa dhamana mpaka weekend iishe maana yake watapata muda mwingi zaidi kuhojiana na mtu huyo ambaye atatiwa mikononi mwa vyombo vya dola leo hii
 
Yaani Kwa Tanzania MAFISADI ni Mashujaa huku watetea Haki na Maslahi ya Nchi ndio wanaonekana Wahalifu. Yaani mpaka hivi sasa MAFISADI wanataua mitaani huku wale wanaofichua UFISADI wakinyanyaswa na Polisi.
 
Mbona hawajawapekua akina EL na RA,This is unfair.Extended embarassement
Au hilo jengo la UV-CCM ndo limeleta haya?
VIVA KUBENEA
 
Upekuzi unaendelea nyumbani kwake mpaka sasa maeneo ya Temeke.

Nitawahabarisha baadae naenda eneo la tukio.
 
duh duh duh
wanatuma signal gani kwa jf born again members?? au ndo yale ya zombie??? (RIP - Fela Kuti)
 
Back
Top Bottom