Kuvamiwa kwa Ofisi za Mwanahalisi na Polisi

Mimi bado nasubiri ukweli zaidi, maana saa hizi wakulu wote wenye dataz wamelala, kwa hiyo kesho hopefully tutakuwa na full dataz ya kilichojiri hasa,

Lakini bado natoa pole kwa Kubenea na Ndimara.
 
Mahakama huwa haitoi search warrant nani anawadanganya? Wako wapi wanasheria? Mahakama hutoa amri na sio search warrants ....... mfano kama umeshindwa kulipa deni mahakama inaamuru ufilisiwe n.k. Wanakupa muda na siku ambayo baillifs watakuja kukushughulikia.

Meneja Utawala wa Mwanahalisi amesema KLH News leo kwamba Wazee walionyesha warrant kutoka Mahakama ya kisutu.

Na sijui kwanini Mwanakijiji anasema Mahakama haikutajwa wakati yeye ndio alimuhoji.

Unless masikio yangu yameota nta lakini nilimsikia Meneja Utawala Yusuf Aboud akisema wamekuja na warrant kutoka Kisutu.
 
Hata kama walikuwa na waranti kutoka Kisutu hii haina maana kwamba mahakama ndiyo iliyoamuru search hiyo. Mahakama kazi yake ni kusikiliza hoja za mtu anayetaka warranti itolewe ama kama ni mwendesha mashtaka au mkuu wa polisi ambaye atatoa sababu za kuomba warranti na mahakama kuridhia ikiona kuna sababu za kimsingi kisheria.
 
Kuhani... nitarusha tena matangazo saa moja, yawezekana mwenyewe nimeyamiss. NItakuwa tayari kuwa corrected. I'm giving you the benefit of the doubt. Nitarusha saa moja.
 
Hivi unajua hapo umekoroga uji?

Kuridhia maombi ya Warrant sio kutoa Warrant?
 
Kuhani... nitarusha tena matangazo saa moja, yawezekana mwenyewe nimeyamiss. NItakuwa tayari kuwa corrected. I'm giving you the benefit of the doubt. Nitarusha saa moja.

Na mimi naomba nidandie "lift" ya huyo unaetaka kumfurahisha kwa kurusha tena mahojiano. Lakini nina tatizo la usikivu wa radio yako, ukianza kudunda muziki naona radio inatoka baruti kwa speed ya 120 mph na sometimes inakata ghafla na ikiibuka ndiyo kwa high speed. Je, tatizo liko kwangu tu ama ni matatizo yanayoanzia studioni kwako?

Natumia media player na niko kwenye high bandwidth.
 
Hata kama walikuwa na waranti kutoka Kisutu hii haina maana kwamba mahakama ndiyo iliyoamuru search hiyo. Mahakama kazi yake ni kusikiliza hoja za mtu anayetaka warranti itolewe ama kama ni mwendesha mashtaka au mkuu wa polisi ambaye atatoa sababu za kuomba warranti na mahakama kuridhia ikiona kuna sababu za kimsingi kisheria.

AMRI ITAKUWA VIPI AMRI BILA YA MAHAKAMA?
I mean kisheria.
Na ndio maana nikasema kuwa hata hiyo mahakama nayo ubanwe ili itowe vigezo vya wao kusaini warrant hiyo.
 
Meneja Utawala wa Mwanahalisi amesema KLH News leo kwamba Wazee walionyesha warrant kutoka Mahakama ya kisutu. Na sijui kwanini Mwanakijiji anasema Mahakama haikutajwa wakati yeye ndio alimuhoji. Unless masikio yangu yameota nta lakini nilimsikia Meneja Utawala Yusuf Aboud akisema wamekuja na warrant kutoka Kisutu.

Ndio maana nimekuwa very slow na hii ishu kwa sababu toka mwanzo nimeiona haijakaa sawa bado, kunahitajika more info zaidi ya nini hasa kilichojiri, maana mimi sijasikiliza anything, lakini ninaamini kuwa hapa kwenye hii ishu kuna something!
 
Na mimi naomba nidandie "lift" ya huyo unaetaka kumfurahisha kwa kurusha tena mahojiano. Lakini nina tatizo la usikivu wa radio yako, ukianza kudunda muziki naona radio inatoka baruti kwa speed ya 120 mph na sometimes inakata ghafla na ikiibuka ndiyo kwa high speed. Je, tatizo liko kwangu tu ama ni matatizo yanayoanzia studioni kwako?

Natumia media player na niko kwenye high bandwidth.

jaribu kusikiliza na Real Audio kama unayo.. au jaribu kwenda Low Bandwidth.. ila sijui kama watu wengine wana tatizo kama la kwako, wanipe feedback.
 
... nitarusha tena matangazo saa moja, yawezekana mwenyewe nimeyamiss. NItakuwa tayari kuwa corrected. I'm giving you the benefit of the doubt. Nitarusha saa moja.

Ahsante.

Bila wewe haya mambo tungekuwa tunasikia magazeti ya crummy press ya Bongo yakitafsiri walivyoelewa wao. Hapa tunasikia maneno ya wahusika wenyewe.

Unawashinda hata kina Mengi na RA wenye ma televisheni na magazeti na majisenti na ma connection na ma staff ya Wahariri chungu mbovu na Chombo chako hicho cha ki mwenyewe wenyewe.

Inabidi tukuunge mkono kwa hali na mali na Radio yako hiyo. Ishakuwa noma mtu wangu. Yani this past week alone, on the biggest news events in the country tumewasikia wahusika, Mtikila na Wahariri wa Mwanahalisi leo, wanakimbilia KLH News kwanza, na hii Radio ndogo inapata habari kabla ya Mengi conglomerate na TBC na wakuja wakuja wengine wa crummy press za Bongo. Wakati watu wenyewe wala hamko jikoni pale.

Tremendous job there.
 
jaribu kusikiliza na Real Audio kama unayo.. au jaribu kwenda Low Bandwidth.. ila sijui kama watu wengine wana tatizo kama la kwako, wanipe feedback. Ninakuwa online mtu anaweza kuwasiliana na mimi hewani kupitia mwanakjj@hotmail.com

Hata mimi ninatumia high bandwidth katika media player ya window na kuna kipidni inatokea hivyo ghsfla bin vuu tuko full blast na baadae tumerudi chini.
 
Ahsante.

Bila wewe haya mambo tungekuwa tunasikia magazeti ya crummy press ya Bongo yakitafsiri walivyoelewa wao. Hapa tunasikia maneno ya wahusika wenyewe.

Unawashinda hata kina Mengi na RA wenye ma televisheni na magazeti na majisenti na ma connection na ma staff ya Wahariri chungu mbovu na Chombo chako hicho cha ki mwenyewe wenyewe.

Inabidi tukuunge mkono kwa hali na mali na Radio yako hiyo. Ishakuwa noma mtu wangu. Yani this past week alone, on the biggest news events in the country tumewasikia wahusika, Mtikila na Wahariri wa Mwanahalisi leo, wanakimbilia KLH News kwanza, na hii Radio ndogo inapata habari kabla ya Mengi conglomerate na TBC na wakuja wakuja wengine wa crummy press za Bongo. Wakati watu wenyewe wala hamko jikoni pale.

Tremendous job there.

Kuhani naomba kutofautiana na wewe kidogo hapo juu kwa kuuliza swali hili...Je unawajuwa THE GUARDIAN na Role yao kwenye mapinduzi haya ya dunia?
Ni kweli michango iko ya tofauti lakini Mengi na yeye ana mchango wake mkubwa sana...Na kama unabisha kamwulize Mkapa.
 
Jamani nchi yetu inaelekea kubaya, naamini kabisa polisi hapa watakuwa wametumiwa kutekeleza matakwa binafsi ya kundi fulani la mafisadi. Nchi yoyote ambako uhuru wa vyombo vya habari unabakwa mchana kweupe namna hii haina tofauti na Zimbabwe na inastahili kuwa treated na jumuia ya kimataifa kama Zimbabwe!

Naam KKN, huo ndiyo ukweli halisi!!! Wanapekua watu wanaofichua uozo unaofanywa na mafisadi wa chama na sirikali kuiangamiza Tanzania na wakati huo huo wakiwaacha mafisadi wakiendelea kupeta na mapesa yao ya haramu. Halafu wanadai kumkemea Mugabe!! Kumbe wao ni Mugabe hakuna tofauti yoyote!!
 
Kwa wanaojua sheria hasa za bongo, je inawezekana kama kesi hii ya mahakama kutoa search warranty kwa public kupewa habari wakitaka kujua kwamba kesi inahusu nini. swali langu ni kwamba kama nitaenda mahakamani monday na kutaka kujua tu Kubenea ana searchiwa kwa kesi gani, hii ni public information au siyo? wengine hizi sheria hatuzijui na sio vizuri kukurupuka tu.
 
Nadhani mwanasheria wake anaweza kufanya hivyo..Ama kama nimekosea wanasheria wanirekebishe hapa.
 
Tumefika mbali na hii serikali ya JK kila fisadi akisimama anasema mwenye ushahidi wakunipeleka mahakamani basi apeleke mahakamani. RA kapiga kifua sana last week kwenye press conference yake ya kuwa mwenye ushahidi ampeleke mahakamani, hata search warranty ya kumfukunyua tu serikali haiwezi kutoa, lakini wapate hata udaku kuwa kubenea ana bank statement basi serikali ghafla inaamka.
 
sijui tatizo ni nini.. labda wakati naswitch toka automated broadcasting na ninapokuwa live studio.. .. sasa hivi niko "live" kama mnapata tatizo hilo basi mtaniambia..
 
Long way we have bado hawa jamaa hawaamini kuwa kumbe walichokuwa wanatafuta hakipo ila wamekosea njia ,kesho utawasikia wakisema walikuwa wanafuatilia mali ya wizi ama kuna taarifa za kulinda taifa......

Lakini sisi tunafahamu kwamba ni usalama wa kulinda mafisadi na siyo kulinda Taifa. Taifa walishashindwa kulilinda miaka mingi tu. Taifa linalolindwa kamwe mafisadi hawawezi kukupua shilingi bilioni 288 wakaendelea kuwa huru zaidi ya miezi sita sasa tangu ripoti ilipotolewa rasmi
 
Back
Top Bottom