Kuvamiwa kwa Ofisi za Mwanahalisi na Polisi

Mkuu ni mahakama ndio uliyotoa search warant, na hao waliofanya hiyo kazi wamesema wanarudisha mahakamani... huko ndiko... Kubenea and Team, wataambiwa kwa nini wamesearchiwa...

Mkuu Kasheshe,

Heshima mbele, hapa nimekusikia sasa naomba tena kukuuliza one more question, una maana kuwa haya unayosema yamefanyika je ni within sheria na katiba ya Jamhuri yetu?

Meaning mahakama kumauru wananchi wapekulwe majumbani mwao au kwenye makazi yao, kwa amri ya mahakama bila kujua sababu na kwamba sababu wataambiwa baadye huko mahakamani kwenyewe, unasema hii ni within sheria na katiba ya Jamhuri yetu?

Na hakuna kosa la kisheria lililofanyika hapa? au?
 
Mkuu ni mahakama ndio uliyotoa search warant, na hao waliofanya hiyo kazi wamesema wanarudisha mahakamani... huko ndiko... Kubenea and Team, wataambiwa kwa nini wamesearchiwa...

Achana na propaganda za watu kwamba ni GoT

Kasheshe unajua sheria za search and seizure katika Tanzania?
 
Kasheshe unajua sheria za search and seizure katika Tanzania?

Waheshimiwa hili Jambo limewekwa wazi na hao walioenda ku-search, hizi ni taarifa kwenye vituo vya television...

Huenda sijui... sheria... lakini barua iliyosainiwa... na mahakama na mihuri ya mahakama imeonyeshwa leo kwenye vituo vya television....

Namalizia that what I have seen and hear!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kasheshe,

Heshima mbele, hapa nimekusikia sasa naomba tena kukuuliza one more question, una maana kuwa haya unayosema yamefanyika je ni within sheria na katiba ya Jamhuri yetu?

Meaning mahakama kumauru wananchi wapekulwe majumbani mwao au kwenye makazi yao, kwa amri ya mahakama bila kujua sababu na kwamba sababu wataambiwa baadye huko mahakamani kwenyewe, unasema hii ni within sheria na katiba ya Jamhuri yetu?

Na hakuna kosa la kisheria lililofanyika hapa? au?

Mkuu sijui sheria kama ni haki ama sio... lakini nimeona na kusikia kwenye kituo kimoja cha runinga jioni ya leo.
 
Poor us Paparazi...inaelekea ni kutokana na bank statement za Kikwete na Ridhwan ambazo zimechomolewa toka NBC. Ilikuwa iwaanike mwana na mtoto. Anyway, tutaona mwisho wake

PM
Paparazi umeniacha hoi. Umejuaje? I see... Nimekubali kwa mara nyingine wewe paparazi kwelikweli
 
Poor us Paparazi...inaelekea ni kutokana na bank statement za Kikwete na Ridhwan ambazo zimechomolewa toka NBC. Ilikuwa iwaanike mwana na mtoto. Anyway, tutaona mwisho wake

PM

Paparazi hiyo yako kali. Hebu saidia hao waliokupa data kama inawezekana hizo bank stament ziletwe huku JF maana huko kwengine zimeshindikana kupeperushwa.
 
Tanzania hamna rule of law, hata kabla ya statement yoyote kutoka nilikuwa na confidence ya kuandika condemnation ndefu, na inasimama bado.

If at all the bank statement angle is credible, then it follows thta bank statement zako zikivuja ifuate benki yako. Ama sivyo subiri zichapishwe ndiyo ulifuate gazeti. Hapa wanaonyesha kuna mihela wameificha humo, kama siyo kwa nini wanahaha sana na hili?

Na bado, tutawa expose kutoka Channel Islands mpaka NBC.

Ujuha mtupu!
 
Paparazi hiyo yako kali. Hebu saidia hao waliokupa data kama inawezekana hizo bank stament ziletwe huku JF maana huko kwengine zimeshindikana kupeperushwa.
KJ, huu msako umeanza kipindi na wameshakumbwa wengi. Mungu aepushe mbali!
 
Ni kampeni za kuwatisha watu ili waogope kusema au kufuatilia masuala ya watu wanaohusika na ufisadi.
 
Mzee Mwanakijiji anatuzea shere... habari alizoandika kwenye kijiji... na picha hiyo ya mh. mwenye komputa ndio... hiyo iliyoonyeshwa kwenye kituo cha luninga
Na kwenye hio habari ya runinga ndio alipotokea mh. mmoja akasema... wamekwenda kusearch wakiwa na agizo la mahakama... na ripoti watairudisha huko huko mahakamani... sasa sijui kwa nini mzee hakuweka hivi kwenye kijiji na kwenye michango yake hapa kwenye kijiwe
 
Kasheshe... sikuweza kuweka hilo kwa sababu walikataa kutaja mahakama iliyotoa agizo warrant hiyo na walikataa kuelezea kwanini jina la warrant ni la mtu mwingine na upana wake ni "and others".... kwenye Luninga walikuambia ni mahakama gani ilitoa warrant hiyo na ilikuwa na mipaka gani?

Nafahamu sheria sidandii vitu kama hivi. Hakuna cha kesi ya mahakama wala nini. Unless wewe uniambie hapa authoritatively ni mahakama gani na hakimu gani aliyetoa hilo na kwa msingi gani (probable cause).

I'm listening.
 
Mahakama huwa haitoi search warrant nani anawadanganya? Wako wapi wanasheria? Mahakama hutoa amri na sio search warrants ....... mfano kama umeshindwa kulipa deni mahakama inaamuru ufilisiwe n.k. Wanakupa muda na siku ambayo baillifs watakuja kukushughulikia.
 
Am disturbed to lean this shameful act of intimidating our press. Mwanakijiji naomba uisambaze hii taarifa ulimwenguni kote kabisa. ili watu wajue nini kinanendelea.

kitendo cha kumakamata KUbenea ni dhahiri kwamba, serikali iliyopo inafanya mambo mengi mabaya na pindi yanapowekwa hadharani wanakosa cha kufanya badala yake wanaamua kunyanyasa wanaofichua maovu. Serikali badala ya kukamata na kupambana na wale wanaosababisha uovu na ufisadi, inaishia kukamata wale wanaofichua uovu huo.

Kweli nimeshangazwa sana na kitendo cha serikali mpaka leo hii kutokamata mtu yoyote aliyehusika na EPA, wale wakurugenzi wa BoT waliotakiwa kukamatwa na kuchukuliwa hatua, wale walioiba kupitia makampuni hewa, wamesamehewa na kupewa muda wa kurudisha hela, leo hii wanaenda kukamata na kuwapekua hawa wanoatoa taarifa, tena taarifa za ukweli na zenye nia za kulinusuru taifa letu.

Je kuna taarifa ambayo imewahi kuandikwa na gazeti la Mwanahalisi ambayo si ya ukweli? Habari zote zimekua za kweli tena ukweli usiopingika. Leo hii tuankamata watu wanaopenda kusema ukweli na uwazi, je tunakwenda wapi? Tanzania ni taifa gani lisilopenda ukweli?

Kama wamefanya hivo kwa nia ya kummaliza Bw. Saidi Kubenea basi waandike maumivu manake sasa ndio wamempandisha chati haswa.

Nashauri kama kunauwezekano tufanye donation ya kumsaidia Bwana Kubenea kwenye kipindi hichi kigumu. Kama kuna mtu mwenye bank acccount yake aiweke hapa ili tumchangie walau hela kidogo za kununua computer nyingine na ikibidi back up
 
Kasheshe... sikuweza kuweka hilo kwa sababu walikataa kutaja mahakama iliyotoa agizo warrant hiyo na walikataa kuelezea kwanini jina la warrant ni la mtu mwingine na upana wake ni "and others".... kwenye Luninga walikuambia ni mahakama gani ilitoa warrant hiyo na ilikuwa na mipaka gani?

Nafahamu sheria sidandii vitu kama hivi. Hakuna cha kesi ya mahakama wala nini. Unless wewe uniambie hapa authoritatively ni mahakama gani na hakimu gani aliyetoa hilo na kwa msingi gani (probable cause).

I'm listening.

At least you could have said so!!!

By the way za Mahakama hujathibitisha lakini za GoT umedhibitisha... haya... twende mbele!!!
 
Mahakama huwa haitoi search warrant nani anawadanganya? Wako wapi wanasheria? Mahakama hutoa amri na sio search warrants ....... mfano kama umeshindwa kulipa deni mahakama inaamuru ufilisiwe n.k. Wanakupa muda na siku ambayo baillifs watakuja kukushughulikia.

Dua..Hilo lilikuwa ni swali langu la mwanzo kabisa kuwa ni mahakama gani imetowa warrant hiyo.
Kiutaratibu ni lazima waende mahakamani kwa either jaji ama hakimu na kuomba ruhusa ya kwenda ku search.

Na kwa kawaida huwa wanaulizwa na jaji ama hakimu kuwa ni ushahidi gani walionao wa nguvu ili kuweza kumpa yeye mamlaka ya kuruhusu search warrant yao hiyo kui saini ili waweze kwenda kumsachi Kubenea.

Na hivyo ni kazi ya hakimu ama jaji huyo kuhakikisha kama ni kweli hao watu wana ulazima wa kwenda ku search kwa kina Kubenea kwani kwa kutokufanya hivyo(kwenda kusachi) basi either ushahidi fulani utaingia kwenye matatizo na ama kutokamatwa ama kusachiwa kunaweza kuvuruga ushahidi ama kuhatarisha maisha.

Na wakili wa kina Kubenea ana haki ya kuambiwa na mahakama hiyo kuwa ni ushahidi gani uliotumika kumshawishi huyo jaji ama hakimu hadi akakubali kusaini hiyo search warrant.
Kama nimekosea naomba nirekebishwe.

NB: Naona na Mzee MADELA WA MADILU yuko ndani ya Nyumba!
Karibu tena Mkuu kwani nasaba zako tumezikosa sana tu!
 
At least you could have said so!!!

By the way za Mahakama hujathibitisha lakini za GoT umedhibitisha... haya... twende mbele!!!

kasheshe, ungesikiliza show yangu nilipofanya "live" na Meneja Utawala wa Hali Halisi mchana wa leo, kabla ya kurusha shutma za namna hiyo.
 
Back
Top Bottom