Kuvaa wigi au Brazilian Hair Kanisani, Je huwa kuna Mungu anahubiriwa kweli?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,472
8,692
Wigi au nywele za bandia, kucha za bandia na kope za Bandia hivi sio tu kwamba ni urembo bali ni kumsahihisha Mungu alie kuumba.

Nitawaunga mkono hao wamini kama watavaa wigi la nywele za kiafrica au kucha za kiafrica.

Kitendo cha kuvaa sijui Brazilian Hair au Indiani hair ni kwamba Mungu alifanya makosa makubwa mno kukupa nywe za kiafrika au kukupa kucha za kiafrica au kope.

Sasa je walio okoka hasa wachungaji na Manabii wa kike huwa wana manisha nini wanapo Vaaa wigi la nywele za kizungu?

Na huwa wana mhubiri Mungu yupi? Huyo wanaye msahihisha kwa kuwapa nywele ngumu? Au yupi?

Wazungu huwa wanavaa wigi ila tofauti yao na Waafrica ni kwamba wao wanavaa wigi la nywele za za Wazungu wenzao. Hakuna Mzungu anaye vaa wigi la nywele za Kiafrica.
 
nazungumzia kuvaa nywele za bandia za Wazungu au kucha za wazungu au kope za wazungu.
Swali lako liende sambamba na hili,
Je, kuvaa nguo kanisani ni kuficha maungo yako uliyopewa na Mungu?
 
Mbaya zaidi wengine ni Manabii sijui mama wachungaji, wana vaa nywele za Wahindi vichwani huku wanahubili uumbaji wa Mungu
Ndo unakuta mwanamke anajifanya mfia dini lakini kila siku wigi halibanduki, hapo mimi hua naona hamna kitu
 
Haina shida kuvaa wigi za nywele za Wazungu? Je wazungu huvaa za Waafrica? Kwa nini wao wasitamani kuvaa nywele za Waafrica?
Mi Naona haina shida, kupamba nyumba ( housing) provided sipo uchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom