tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,796
- 18,218
Mimi nashindwa kuelewa kabisa watu (hasa wanaume) wanaovaa saa enzi hizi za dijitali kama wanafanya hivyo kwa makusudi au ni mbwembwe tu. Kwanini nasema hivyo? Siku hizi yapata 98% ya watanzania wote wanamiliki simu na kwenye simu kuna saa.
Utamkuta mwanamume sharobaro anamiliki simu 3 kwa mpigo na wakati huo huo katupia bonge ya saa kiganjani mwake. Kuvaa saa kwa wanawake inaleta maana kidogo kwa kuwa inachukua nafsi ya bangili &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; ni pambo la kike.
Sikumbuki mara ya mwisho kuvaa saa na sitegemei kuivaa tena labda nikiwa kwenye chumba cha mtihani nitaibeba na kwenda nayo na baada ya kumaliza kupiga paper nitampa demu wangu avae kama bangili. Uvaaji wa saa enzi hizi unawafaa zaidi wanafunzi wa shule za msingi kwa kuwa wengi wao hawamiliki simu. Tujifunze kuishi kulingana na wakati.
:israel:
======
Mada hii ni moja kati ya zilizojumuishwa kwenye kipindi cha Jamii Leo katika chaneli yetu ya YouTube. Kuona habari nyingine zaidi, tazama video hii hapa chini: