EMMANUEL JASIRI

Senior Member
Feb 2, 2015
127
62
1. Fanya biashara unayo ielewa vizuri zaidi, usiige tu kwa kuona mwingine anafanikiwa. Hakikisha wewe mwenyewe una ujuzi nayo.

2. Hakikisha umeyasoma mahitaji ya wateja wako watarajiwa. Hakikisha umeyaelewa kiundani zaidi mahitaji yao na unaweza kuwatimizia ipasavyo.

3. Amua kujenga mahusiano mazuri na wateja wako watarajiwa. Waelewe ili uweze kuwa sababu ya furaha yao.

BIASHARA YOYOTE IMARA HUJENGWA PALE TU. UNAPO KUWA NA MAHUSIANO MAZURI NA WATEJA WAKO.

1622796297945.png

hasa
1. Fanya biashara unayo ielewa vizuri zaidi, usiige tu kwa kuona mwingine anafanikiwa. Hakikisha wewe mwenyewe una ujuzi nayo

Namba moja iyo mnaanza kulaumiana bure eti haah mtu autaki kunipa connection hata awajui unachofanya mpaka unafanikiwa je labda natembea na mother angu,biashara yoyote ina siri kubwa...IGA UFE
 
1. Fanya biashara unayo ielewa vizuri zaidi, usiige tu kwa kuona mwingine anafanikiwa. Hakikisha wewe mwenyewe una ujuzi nayo

2. Hakikisha umeyasoma mahitaji ya wateja wako watarajiwa. Hakikisha umeyaelewa kiundani zaidi mahitaji yao na unaweza kuwatimizia ipasavyo.

3. Amua kujenga mahusiano mazuri na wateja wako watarajiwa. Waelewe ili uweze kuwa sababu ya furaha yao.

BIASHARA YOYOTE IMARA HUJENGWA PALE TU. UNAPO KUWA NA MAHUSIANO MAZURI NA WATEJA WAKO.
Fanya bei nzuri. Hii inatosha mimi kuwa mteja wako sio lazima uje kufanya stori na mimi eti unajenga uhusiano mzuri
 
hasa

namba moja iyo mnaanza kulaumiana bure eti haah mtu autaki kunipa connection hata awajui unachofanya mpaka unafanikiwa je labda natembea na mother angu,biashara yoyote ina siri kubwa...IGA UFE
Mkuu ukisema tufanye biashara tunazozijua na ujuzi nazo utakuwa huna tofauti na wanaotaka mwajriwa awe na uzoef miaka 3. Lazima kila kitu kina starting point.
 
Dunia tuliyo nayo, imehama. Dunia imehama kutoka katika mfumo wa niambie, Dunia imehamia katika mfumo wa nionyeshe.

Wakati huu ndipo ambapo neno lisemalo, maneno matupu hayavunji mifupa linatimia. Watu hawataki kuambiwa tu kuhusu uzuri wa bidhaa yako na namna inavyofanya kazi. Ila watu wanataka waione ikifanya kazi kama ilivyo elezewa.

Kama haupo tayari kuwaonyesha, utawapa wakati mgumu sana kukuelewa. Watu wanataka kuona si kuambiwa tu.
  1. Waonyeshe leo, upate faida baadaye.
  2. Jifunze kuwasoma kwa haraka wateja wako.
  3. Ni muhimu kukitambua kile kinacho wachukiza wateja wako ili ukiondoe haraka.
  4. Pia ni muhimu kukitambua kile wanacho kipenda ili uwawekee kwa haraka.
 
Kaka fulani ninaye mfahamu mimi. Yeye aliamua kuanzisha duka la mahitaji ya nyumbani mtaani kwake, baada ya kugundua kuwa katika mtaa majirani zake walihangaika sana kupata huduma na bidhaa hizo kwa shida.

Hata waliokuwa wakitoa huduma hizo, walikuwa hawana mitaji ya kuwapatia wateja bidhaa zinazo hitajika kwa wakati muafaka.

Na hata baadhi ya bidhaa za muhimu kwa matumizi ya mwanadamu, katika mtaa huo zilitafutwa bila mafanikio. Ndipo kijana huyu akaja na wazo lakuanzisha duka litakalo timiza mahitaji yote muhimu.

Mahitaji ambayo, wananchi wa mtaa huo wana yahitaji, ila wanayakosa. Huyu kijana baada ya kuleta huduma na bidhaa wanazo hitaji, kiukweli amefanikiwa sana kifedha

Swali naku uliza: Ni nini kinacho kusukuma kuianzisha aina ya biashara unayotaka kuifanya?
 
Kuuza ni kusafirisha hisia kutoka kwako kwenda kwa watu wengine

Hisia inayo wasababisha watu wengine kufanya uamuzi na kuchukua hatua ya kununua kile unacho kiuza

Unaweza kuisafirisha hisia ya kuuza kupitia

Maandishi

Maneno

Na matendo
 
4. Weka ulinzi wa hela, kama ni mcha Mungu fungua biashara yako kwa maombi na kama wewe ni wamataifa tafuta mganga aganye mambo.... Chuma ulete wapo kila sehemu.
Hii comment imenifurahisha na nikiangalia hiyo motion avatar yako inaendana😄
 
Hakika Mkuu

Nina mpango mkubwa sana wa kufungua duka la rejareja + jumla.

Nitawakamata sana hao wateja,kwa sabbu nitacheza nao kwa saikolojia kubwa. Kuna mambo flani flani ukiyaact kwa mtu kamwe hatokaa apindue meza

Hawatonishinda kabisa.
mambo gani ayo mkuu ukiyaect wateja hawtokaa mb ali na wewe
 
Back
Top Bottom