Kuuza mahindi ya njano kwa nchi ya Misri

Mwanza kwetu pia

Senior Member
May 25, 2021
104
150
Habari zenu nyote,

Bila kupoteza muda niende kwenye mada, miezi michache iliyopita nilisikia serikali ikisema ya kuwa nchi ya Misri inataka kuwa inanunua MAHINDI ya njano takriban tani milioni moja kwa mwaka toka Tanzania.

Hivyo wizara ya kilimo ilijitokeza mbele ya wananchi na kuutangazia uma wa watu kuwa tuanze kulima MAHINDI ya njano kwani yamepata soko nchi Misri na ikibidi hata Kama leo yatapatikana ya kutosha waondoke nayo.

Akaendelea kusema kuwa iwapo tutakuwa tayari kulima kilimo hicho basi wao wizara wameshataarifiwa na nchi husika kuwa Kuna aina ya mahindi ya njano ambayo wanayapendelea na ambayo ndo watakuwa wanayanunua hivyo hatuna budi kuchukua mbegu toka kwao,

Swali no, 1; je, watu wamejitokeza kwa wingi kiasi gani kulima hicho kilimo kwa ajili ya kuiuzia Misri

Swali no 2; je hizo mbegu tayari wizara ya kilimo inazo kwa Sasa

Swali no 3: tutakuwa tunamuuzia Misri kwa bei gani ili mkulima kabla hajalima ajue kabisa bei

Swali no 4; hiyo mbegu ukilima heka moja unatoa mavuno kiasi gani au gunia ngapi?

Swali no 5; mazao gani mengine tunahitajika tumuuzie Misri na yuko tayari kununua toka kwetu na kwa bei gani wananunua

Wadau kwa anayeelewa atufungue ili tufahamu au Kama Kuna mtu wa wizarani humu atusaidie kujua kwa hicho nilichokiuliza ili tufahamu.

Uzi tayari;
 
Habari zenu wadau, nakumbushia miezi michache iliyopita serikali ilijitokeza na kueleza kwamba nchi ya Misri imetuma viongozi wake kuja nchini na kuiambia serikali yetu kuwa wanahitaji wanunue mahindi ya njano toka kwetu takriban tani milioni moja kwa mwaka.

Hivyo serikali ilijitokeza mbele ya wananchi na kuwaambia kuwa wachangamkie fursa ya mahindi ya njano kwani tayari soko limepatikana Misri,

Pia serikali ikaongezea Misri wana aina ya mahindi wanayoyapendelea na wapo tayari kutuma mbegu zao hivyo iwapo utahitaji kuanza kulima zao hilo utahitajika uende wizarani ili upewe mbegu hizo.

Swali langu ni je mbegu hizo tayari zipo wizara ya kilimo au Kuna sehemu zinapatikana,

Swali la pili ni utaratibu wa kuiuzia Misri ukoje baada ya mkulima kuivisha mazao yake,

Swali la tatu, Misri wanatununulia kwa bei gani kwa kilo ili mkulima ajue atapata faida kiasi gani kabla ya kulima

Swali la nne, tayari Misri imeshauziwa tani ngapi hadi Sasa,

Swali la tano, heka moja ya hiyo mbegu inayotoka Misri inatoa mazao tani ngapi

Swali la nyongeza, wananchi wamechangamkia fursa kwa kiasi gani

Kwa mliopo wizara ya kilimo mtusaidie kuutulizia huko na mtupe mrejesho,

Nawatakia asubuhi njema nyote
 
Mashaka yanaanzia hapo mbegu uifate wizarani mkuu kama unataka kulima tafuta mazao ambayo soko lake unalijua
 
Back
Top Bottom