Kuunguruma kwa kongamano la Wanataaluma Dar: Moto wayaka!

Kiongozi na Mzalendo Mushi nimekupa vizuri Mkuu;

Kwa maoni yako, suppose tunataka kuanza kutekeleza maoni yako, nilichopenda kujua tunaenda vipi kimikakati in terms of actions mpaka tufanikiwe? Nadhani hilo ndo kubwa kubwa na muhimu.

Mzalendo Sanctus,

Usipoteze muda wako adimu hapa. Wewe endelea na mikakati yako. Mwishowe nawe utaonekana "kichaa". Kaa chonjo.

Ni ushauri tu. Ila kama unao muda wa kupoteza hapa, basi endelea kujibu ....
 
Kuna wanaosema viongozi wetu/politics ni wala Rushwa hivyo ndio maana Tanzania ni masikini,

sawa ndio lakini hivi duniani kuna nchi kusiko na Rushwa?one of the most succesfull economies are also the most corrupt.

nionavyo mie,we have problems with our system.hii ndio inalea hawa wanasiasa wala rushwa,lets work on fixing the system not leaders/leaders will come and go,the system will be there to stay.

i believe we don't need a kikwete to fix poor services in public offices,do we?
Tunamlaumu sana kikwete,lakini the guy will come and go,even worse leaders than him will come.

swali kwa TPN,mmeandaa any specific solution ya tatizo Lolote lile ili wengine wafuate mfano wenu?

Mzalendo Kimweri;

Unayoyasema ni kweli. najizuia sasa hivi kutoa official statement kwa kuwa Maazimio na notez zote za mkutano bado tunayaweka vizuri. I hope kesho naweza nikazipost as Official Position kama Press Release. Then will be able to respond.

Lakini trust me, mikakati iliyowekwa ni mizuri na inayotekelezeka.
 
Wengine wanatafuta channel za kutokea hapo

Wengine wanatafuta kuonekana nao wamo

Hamna aliye na kipya, ukiangalia maswali yao tu utaona kama wanataaluma ndio hawa bora labda hao wabeba boksi.

Yap! Yap!

Hilo ndo tatizo kubwa kabisa linalowafanya wanasiasa kuwaona 'wanataaluma' kama wana-kujikomba.

Matatizo yooote wanayafahamu kama walivyoyaweka, Tatizo ni jinsi ya kuwaeleza wanasiasa. Wakiwa mbele yao utaona kabisa ni kwa mtindo wa kuwafanya wanasiasa waonekana ndo wanaojua saaana matatizo na suluhu.

Nilidhani, kama wanataaluma walistahili kuwaonyesha wazi kabisa kwamba hapa muko safi, pale muko hovyo. Na solution kwa wa TZ ni hii. Sasa hivi ni jukwaa la kutoa risala na kufahamika ili baadaye watumike kisiasa kama REDET.
 
Kiongozi na Mzalendo Mushi nimekupa vizuri Mkuu;

Kwa maoni yako, suppose tunataka kuanza kutekeleza maoni yako, nilichopenda kujua tunaenda vipi kimikakati in terms of actions mpaka tufanikiwe? Nadhani hilo ndo kubwa kubwa na muhimu.

Mkakati wa kuziamsha fikra za watanzania wote ili wakigunduwa kuwa their fate is on their own hands,basi "hawataridhika na mazingira"

Tusiwaachie wakristo na waislam kuja na waraka...Na ndio maana ninarudia statement yangu kuwa kuna a fundamental way of solving this problem,hata hivyo no one knows how to approach it,na ndio maana ukitazama mazingira unaona mara waraka wa waislam,mara wa wakatoliki,mara kongamano la mwalimu Nyerere,yani hakuna pa kutokea,ni a situation with crubs in a bucket,there have to be some efforts beyond the inside of the basket if we really are to make progress as a Nation.

Kwahiyo utaona kuwa mara baada ya kuzisoma taarifa mbali mbali zenye kuhusiana na mustakabali wa Taifa letu,nimeona kuna struggling,mainly on how to inform people the ways to put themselves in right enviroments in order for the society to progress,na ndio maana kuna hizi nyaraka za kuwaeleza wananchi ni kiongozi gani mwenye kuwafaa,lakini wanasiasa opportunist wanatumia kama kete ya divide and rule,na sasa unasikia ni wakristo vs waislam instead of mafisadi vs wazalendo,ama good enviroments vs bad ones,sasa ushawishi wa mikinzano ya kidini instead of focusing on the mission unakuwa the main obstacle....

And so therefore mikakati ni miwili,kwanza cha muhimu kabla sijamention mikakati,ni lazima tuwe na viongozi ambao ni wazalendo watakaokubali kwamba system ni mbovu na tunahitaji mabadiliko,secondly zifanyike jitihada madhubuti za kuwaelimisha wananchi kuwa uwezo na sababu ama madhumuni wanavyo,wanachohitaji ni nia ya kufanya mabadiliko kwa kushirikiana na viongozi wazalendo,hatuwezi kuwajua kwa majina tu hao viongozi wazalendo,bali tutawajuwa kwa yale wanayosema na kuyafanya....Kushirikiana na wananchi na kuhakikisha kuwa wanaelewa ni kwa namna gani watajijengea mazingira mazuri ya kuweza kujiletea maendeleo.
 
Wakati tumeanza harakati hizi nilikiita hiki tunachokifanya kuwa ni "mapambano ya kifikra".. Natumaini wanataaluma na watu wengine wanazidi kuona ukweli huu na jinsi gani ilivyo vigumu kubadilisha fikra.
 
Mzee mwanakijiji unaonaje sasa na wewe kama mwanataaluma mzalendo uwe wazi sasa hakuna haja ya kuficha nyuma ya majina mengine uwe wazi ujulikane wewe ni nani ili kujenga utamaduni wa kuwajibika miongoni mwetu na kuongea kwa uwazi kama jamii zilizoendelea
 
Mzalendo Sanctus,

Usipoteze muda wako adimu hapa. Wewe endelea na mikakati yako. Mwishowe nawe utaonekana "kichaa". Kaa chonjo.

Ni ushauri tu. Ila kama unao muda wa kupoteza hapa, basi endelea kujibu ....

We Ilongo ondoa longo longo hapa,usiharibu forum,acha kimbelembele huyu ni mtu mzima na hii ni jf usimwalimulie nini cha kufanya ama kusema,kwani maana ya forum ni nini?We una muda wa kupoteza hapa ndio maana umesoma postings na kuijibu hii ya kwake? kwani hakuna "vichaa" wanaokaa kimya tu?Acha ushamba hii ni JF.
 
Wakati tumeanza harakati hizi nilikiita hiki tunachokifanya kuwa ni "mapambano ya kifikra".. Natumaini wanataaluma na watu wengine wanazidi kuona ukweli huu na jinsi gani ilivyo vigumu kubadilisha fikra.

MKJJ;Nguzo kuu ya umasikini Tanzania ni mentality,ni mambo ambayo yanatia huruma ukiafikiria kwa undani zaidi...Mwalimu aliliona tatizo hilo mapema sana,na ndio maana na yeye akaja na siasa za ujamaa na kujitegemea,ile mentality ya kwamba "Hatuwezi" "Sisi ndivyo tulivyo" nk ndivyo vilivyomfanya atake kupambana na ile mentality ya kuomba omba na imani kwamba we can't do nothing,na kwasababu siasa zake zile zilikufa,kukawa na loophole,na sasa siasa zimekuwa kama michezo ya kipuuzi kwasababu as a nation hatuna vision wala mission.

Utani convince vipi kwamba tunaomba ili tuendelee?Kuna kiongozi wetu ambaye ameonyesha kuwa ana nia ya kuwazindua wananchi kwamba they can determine their future and that the can make a difference?kwamba their success is within their capacity?Mentality ya kuomba omba inawapumbaza wananchi na kuona kweli hatuna kitu,na wakati in reality rasilmali zinauzwa kwa bei chee.
Na kwahivyo basi mapambano haya ya kifikra yanahusisha kampeni mahsusi yatakayo ignite mapinduzi ya kijamii na kifikra,wananchi wajuwe kuwa wana uwezo wa kuwawajibisha viongozi wenye ku act against the National interests.Tuna wanasiasa wazalendo lakini hawajui namna ya kudeal na issue hii,mwalimu alikuwa ni mtanzania,na alikuwa ni mpigania uhuru,hilo tu lingetosha yeye kutangaza tu kwamba anagombea na wananchi wampigie kura,lakini haikuwa hivyo,alienda kijiji by kijiji kata by kata,siku hizi hata hao ambao ndio wazalendo wameishia kwenye press conference tu,hakuna massive campaign to reach the people,ile ya ki "uhuru uhuru"na kwasababu ya mixture ya vyombo vya habari vya mafisadi vikiwemo,basi wananchi are totally confused na sidhani kama wanajuwa tofauti wanapoangalia hayo vs ze comedy...Kujua kuwa kipi ni comedy na kipi real...Wafanye kampeni waondoke huko maofisini,kampeni ya kuwaelimisha wananchi,kwamba we need change in direction and in the way we think,and that yes we can....Wananchi hawajui connection ya umasikini na uamuzi wao kwenye sanduku la kura kwasababu si wanaambiwa sisi ni masikini to begini with?Sasa kama kazi yetu kuomba omba unataka wasimchaguwe mtu mwenye personality ya JK?Wananchi hawajui kulinganisha ufanisi wa uongozi na impact yake kwenye maisha yao either a kila siku ama hata ya generation to generation.
 
Jmushi1:

Watanzania na miradi yenu ya kumuinua mtu kifkra (mentality), mnapoteza muda na resources tu. Na ujamaa kilikuwa sio chombo cha kunyanyua fikra za mtanzania.

Kukiwa na incentives za watu kujifunza au kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao, they will do a lot of things on their own.
 
Kwenye kuhusu ujamaa sijasema "Kunyanyua fikra" Nimesema ni jitahada za mwalimu kuwajengea watanzania mentality ya kujitegemea,kwamba they can do it by themseleves,aliliona hilo tatizo,nimefuatilia baadhi ya hotuba zake na nimegundua kuwa hilo lilikuwa tatizo na kuomba omba ama masharti ya kiugandamizaji alipingana navyo sana.Ninacho amini mimi ni the whole system is rotten,na hizo incentives kwa mfano kiuchumi zinzpatikana vipi?Unaweza kuwa na bidhaa za uzalishaji lakini wananchi wasiweze kuafford,hatuwezi kufanikiwa kama incentives tunazotegemea ni nje ya soko letu la ndani,incentive for more innovation ni a successfull marketing,kwamba mwishowe utauza,nijambo la maana umerecognize hilo la incentive,kwasababu lack of incentive ndio mazingira hayo tunayozungumzia yenye kusababisha wataalam legit washindwe ku utilize utaalam wao kwa maendeleo ya Taifa....Na kwa kumalizia tu ni kwamba statement yako haijakamilika unaposema "They will do things on their own" kwasababu if there is incentives invlolved then they just cant do it "on their own"
Kuhusiana na incentive,hilo ni kweli lakini unaonekana dhahiri ku ufavor ubepari zaidi kwa kauli yako hiyo,hata hivyo ku avoid the complexity of the issue,incentive ni lazima iambatane na any kind of innovation
 
Tanzania is among the poorest nations of the world where more than fifty percent of her population live below the poverty line; and that the main cause of poverty is under development which can be expressed in terms of unemployment, underproduction, high rate of illiteracy, low level of Science and Technology and imbalance in its trade balance caused by among others unmanageable external debt and lopsided international trade practices.

Hii preamble hata hivyo inanipa matatizo kidogo - Ni kweli kuwa Tanzanaia ni kati ya nchi masikini duniani lakini umasikini wetu ni mavuno ya zao kutoka shamba tulilolifyeka na tukalilima sisi wenyewe. Baada ya hapo tulipanda mbegu, tukapalilia, tukamwagilia na sasa tunavuna tulichopanda. Kwa kifupi tumeendelea kujenga utamaduni wa kuuona huu umasikini kama jadi yetu kiasi cha kutokuona haya kuwa omba omba. Bado hatuuoni huu umasikini kama adui wa kupigwa vita kwa nguvu zetu zote badala yake tunaona fahari kuendelea kuukumbatia.

Tulipofikia maazimio pekee hayawezi kuleta mabadiliko kwani mfumo ambao umewezesha status quo uko pale pale - intact. Kongamano, semina, warsha na vikao vilivyoota kama uyoga mpaka sasa vime contribute positively nothing katika maendelao ya taifa. Kinachohitajika ni utekelezaji lakini chini ya mfumo wetu, tunajidanganya kama tunafikiri tutafanikisha lolote bila mabadiliko ya msingi - KATIBA. Vyombo vyetu vinaongozwa na wataalamu waliobobea lakini utendaji wao unatawaliwa na maslahi binafsi - kubwa ikiwa kulinda nafasi zao.

Katiba imeweza kumwagilia na kurutubisha mindset ya ubinafsi katika taifa na hivyo kuwalinda waajiriwa(viongozi) wasiweze kuwajibishwa na mwajiri mkuu(wananchi) na hivyo kuwapa kiburi cha ajabu. Wengi wa wanataaluma na wasomi wetu kwa woga na tamaa wakaamua kuvaa miwani nyeusi na kuweka rehani taaluma zao kwa kujiunga na staus quo. Ningefurahi zaidi kama kongamano za aina hii zingejikita zaidi katika kuangalia mapungufu na muundo wa Katiba na kudai iandikwe upya - Shamba lazima lifyekwe kwanza kabla ya kupanda zao.
 
Taifa lisilokuwa na vision pamoja na kutegemea kuomba omba na kuendesha nchi kifisadi ni combination moja hatari sana,product yake ndiyo hii ya kujiona kuwa tuko stuck,leadership vacuum na mengineyo mengi,no mandates...Kama mission ya Taifa towards maendeleo ni kuomba omba,then zipi ndio qualifications za viongozi ama kiongozi mkuu wa nchi?
 
Hii preamble hata hivyo inanipa matatizo kidogo - Ni kweli kuwa Tanzanaia ni kati ya nchi masikini duniani lakini umasikini wetu ni mavuno ya zao kutoka shamba tulilolifyeka na tukalilima sisi wenyewe. Baada ya hapo tulipanda mbegu, tukapalilia, tukamwagilia na sasa tunavuna tulichopanda. Kwa kifupi tumeendelea kujenga utamaduni wa kuuona huu umasikini kama jadi yetu kiasi cha kutokuona haya kuwa omba omba. Bado hatuuoni huu umasikini kama adui wa kupigwa vita kwa nguvu zetu zote badala yake tunaona fahari kuendelea kuukumbatia.

Tulipofikia maazimio pekee hayawezi kuleta mabadiliko kwani mfumo ambao umewezesha status quo uko pale pale - intact. Kongamano, semina, warsha na vikao vilivyoota kama uyoga mpaka sasa vime contribute positively nothing katika maendelao ya taifa. Kinachohitajika ni utekelezaji lakini chini ya mfumo wetu, tunajidanganya kama tunafikiri tutafanikisha lolote bila mabadiliko ya msingi - KATIBA. Vyombo vyetu vinaongozwa na wataalamu waliobobea lakini utendaji wao unatawaliwa na maslahi binafsi - kubwa ikiwa kulinda nafasi zao.

Katiba imeweza kumwagilia na kurutubisha mindset ya ubinafsi katika taifa na hivyo kuwalinda waajiriwa(viongozi) wasiweze kuwajibishwa na mwajiri mkuu(wananchi) na hivyo kuwapa kiburi cha ajabu. Wengi wa wanataaluma na wasomi wetu kwa woga na tamaa wakaamua kuvaa miwani nyeusi na kuweka rehani taaluma zao kwa kujiunga na staus quo. Ningefurahi zaidi kama kongamano za aina hii zingejikita zaidi katika kuangalia mapungufu na muundo wa Katiba na kudai iandikwe upya - Shamba lazima lifyekwe kwanza kabla ya kupanda zao.

Binafsi hii vita wapiganaji wa pande zote wangekua wanalenga hapa ndio ningekua conviced kweli people want to see changes. Kama ulivyosema upandi shamba bila kufyeka kwanza na sababu zingine zinazowafanya hawa wajamaa walinge. KATIBA mbovu iliyo na limitations kwenye ku police accountability.

Zote zilizobaki ni hadithi zenye ukweli fulani lakini hii ndio hatua ya kwanza sijui kwanini wengi hawalioni hili asante sana MKUU.
 
Hivi WATAALUMA ndio kina nani na ni sifa zipi wanazopaswa kuwa nazo ili watambulike hivyo? Isije ikawa mambo ya Wasomi wapinga halafu unakuta ni wanafunzi ambo hata degree moja hawajaipata bado...

omarilyas
 
Sasa unauliza wataaluma ni akina nani alafu unajibu kama lazima wawe na degree hiyo kakufunza nani.

Mfano bill gates hasnt got one lakini anaweza kukaa kwenye body ya washauri kwenye softaware; business; human rights na akatoa mchango mkubwa pengine kuliko wenye Phd.

Branislow Malinowski a mathematician by trade his impact on the social anthropoligist changed the thinking completely ambayo ilikua imechangiwa na scholars waliokua na madgree makubwa.

the list goes on

1.Piaget...a zoologist by trade
2.Freud..... a doctor by trade
3.
4.
etc etc

Read read and read sometimes utajikuta unajua kuliko huyo Professor I know so; if anything ume demonstrate a luck of understanding hapo.
 
Madudu yaliyopo TZ yanafanya na kuratibiwa na hao hao wasomi. I think kama hii network inataka kutuonyesha njia approach yake lazima iwe tofauti. Tumeshachoka na semina na makongamano yasiyokwisha na yasioleta mabadiliko yoyote.Uzuri wa hii semina ni kuwa imeandaliwa bila msukumo wa serikali na agenda zake.Kikubwa ni kujiuliza watahimili ushawishi wa powerful people in the goverment who want to use it as a platform to launch their power ambitions
 
Bwana Sanctus Msimbe,

Hongera kwa kuanadaa kongamano na natumaini umevuna ulichokipanda. Je ule Waraka wa Mchungaji ulishaufanyia kazi kama ulivyoniomba mwaka mmoja uliopita?

La pili, je kama TPN na washihriki wa kongamano hili, mlilijibuje swali hili la kwanza
1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara
?

Je ni nini vipaumbele vya kitaifa kwa mujibu wa TPN au kutokana na maazimio ya kongamano? Je Vipaumbele hivi vimebainika au kubuniwa kutokana na mtazamo gani na wa nani? Je vipaumbele hivi vinamnufaisha nani na vipi?

Kama nikiamua kuweka na kubaini vipaumbele viwili vitatu, kwa ajili ya gumzo hapa kama vile Ubunifu, Juhudi, Ufanisi na Uadilifu, nyinyi kama Wataalamu mliokuwa mnachangua vipaumbele vya kitaifa, mko wapi katika kutambua vipaumbele vya Mchungaji, kuishi katika mtazamo wa Mvhungaji kwa kuwa watekelezaji bora wa vipaumbele vya Mchungaji katika ushiriki wa Vipaumbele vya Taifa vya kujenga Uchumi Imara?

Je katika vipaumbele hivi, ni Uchumi pekee ambao ni mlengwa na mnufaika? je mengine ambayo si ya kiuchumi, TPN na washiriki wanamuachia nani na yatasawazishwa vipi kama hayapo au kama yana kasoro?
 
Back
Top Bottom