Kuunguruma kwa kongamano la Wanataaluma Dar: Moto wayaka!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kongamano la wanataaluma linakutana kutwa nzima ya ijumaa. Je matarajio yako ni nini hasa? Litakuwa kama makongamano mengine yaliyosifiwa kwa kutoa kauli kali na maazimio yenye vipengele hadi vya herufi za kichina? Tutarajie nini tofauti na kwa nini au ndio yaleyale?

Vyovyote vile.. kongamano hili la wanataaluma wetu chini ya mwamvuli wa TPN ninaliunga mkono na kuwapa benefit of the doubt kwamba watawasha moto wa fikra mpya..
 
Kongamano la wanataaluma linakutana kutwa nzima ya ijumaa. Je matarajio yako ni nini hasa? Litakuwa kama makongamano mengine yaliyosifiwa kwa kutoa kauli kali na maazimio yenye vipengele hadi vya herufi za kichina? Tutarajie nini tofauti na kwa nini au ndio yaleyale?

Kongamano la wanataaluma gani?

Watanzania walio Diaspora Tanzania au Mkutano wa mazingira Copenhagen?

Au wataaluma wa tunguli Bagamoyo?
 
Hii ni social gathering na ubishoo tu/kutafuta headline kwenye press.
 
Kongamano la wanataaluma linakutana kutwa nzima ya ijumaa. Je matarajio yako ni nini hasa? Litakuwa kama makongamano mengine yaliyosifiwa kwa kutoa kauli kali na maazimio yenye vipengele hadi vya herufi za kichina? Tutarajie nini tofauti na kwa nini au ndio yaleyale?

Kutakuwa hakuna jipya...don't hold your breath.
 
Kongamano la wanataaluma linakutana kutwa nzima ya ijumaa. Je matarajio yako ni nini hasa? Litakuwa kama makongamano mengine yaliyosifiwa kwa kutoa kauli kali na maazimio yenye vipengele hadi vya herufi za kichina? Tutarajie nini tofauti na kwa nini au ndio yaleyale?

Binafsi sitarajii kipya kutoka kwenye hilo Kongamano. Tatizo la Tanzania ni la kisiasa zaidi na siyo la kiuchumi. Nimeangalia mada nyingi naona zimejikita kwenye uchumi zaidi ambako wanaenda kuongeza idadi ya middle class ambao siku zote huwa hawana muda na politics.

Baadhi ya Mada zitakazojadiliwa, kuwekewa mikakati ya kiutendaji na ufuatiliaji ni pamoja na:

1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara

2. Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao

3. Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.

4. Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini

5. Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi

6. Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua za Kuleta Mabadiliko Na kwa Vipi?

7. Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka?

Ni hiyo mada ya 6 pekee ndio ambayo naona inaweza kuwa na mwelekeo wa kuleta mabadiliko ambayo tunayahitaji. Lakini je wana ubavu wa kufuatilia na kuhakikisha kwamba kutakuwa na utekelezaji wa maamuzi/maazimio ya hilo Kongamano?

Kwa maoni yangu, pindi tutakapoweza ku-fix tatizo la kisiasa, hayo mengine itakuwa rahisi sana kuya-fix. Kikwete ameishasema kwamba 70% ya wapiga kura wanafuata mkumbo. Ni tusi, lakini ndiyo ukweli kwamba watanzania wengi hatujui tunataka nini na hivyo walio nacho wanatutumia ili waendelee kutuvuna na kupora rasilimali zetu. Hao wana taaluma siku wakija kuamua kupeleka elimu ya uraia vijijini kwa hao 70% ya wapiga kura, hapo ndio nitaona kweli wanataka maendeleo ya kweli.

Kwa mfumo uliopo sasa, hayo yote wanayoya-discuss hayawezi kuisaidia nchi. Ni nani atawekeza mahali ambako hakuna umeme wa uhakika, hakuna barabara nzuri, sheria zipo lakini wasimamiaji wa hizo sheria wanaangalia kwanza nani amekosa, nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe mahakamani. Nani ushahidi wake ukusanywe kwa nguvu zote na nani ushahidi wake uharibiwe. Tukiweza ku-fix tatizo la kisiasa, sheria zitafanya kazi, DPP, IGP na Hosseah wataanza kuwajibika na siyo kufanya kazi kisiasa. Sheria zikianza kufanya kazi hakutakuwa na ufisadi, hela inayoliwa kwa ufisadi itaweza kuwekezwa kwenye vipaumbele vya taifa. Hakutakuwa na mikataba hewa wala uporaji wa rasilimali unaofanywa na wawekezaji mchana kweupe.
 
Kongamano la wanataaluma linakutana kutwa nzima ya ijumaa. Je matarajio yako ni nini hasa? Litakuwa kama makongamano mengine yaliyosifiwa kwa kutoa kauli kali na maazimio yenye vipengele hadi vya herufi za kichina? Tutarajie nini tofauti na kwa nini au ndio yaleyale?
Hawana jipya ni wachovu.utakuja kuniambia.
 
Wengine wanatafuta channel za kutokea hapo

Wengine wanatafuta kuonekana nao wamo

Hamna aliye na kipya, ukiangalia maswali yao tu utaona kama wanataaluma ndio hawa bora labda hao wabeba boksi.
 
Hii ni social gathering na ubishoo tu/kutafuta headline kwenye press.
Umesahau, na ulaji (au Posho) kwa waandaaji pia, yaani kamati ya maandalizi ikiongozwa na mwenyekiti wao(keep change!) Haha hahaa...blah bla blaaa kwa sana!
 
Mh, hii ngumu kweli kwetu watanzania, ni nani tanzania anaweza kuandaa kitu kikapokewa na positive mazee?

Yaani inavunja moyo kweli
 
Mh, hii ngumu kweli kwetu watanzania, ni nani tanzania anaweza kuandaa kitu kikapokewa na positive mazee?

Yaani inavunja moyo kweli
Yaani! Hata kabla ya kuona matokeo yake yakoje tumetangaza wameshindwa. Duuh! Mi naomba jamaa wachukue hii ni kama challenge na kuthibitisha they mean what they say by action.Mtoto kabla ya kuanza kutembea, huwa anatambaa.Siamini kama huu nao ni mkutano kama mikutano mingine unless waandaji wameamua kufanya hivyo.Bado wana chance ya kufanya kitu tofauti.
 
Mimi nina matumaini sana na hawa jamaa. Lakini, tutapima ni maazimio na utekelezaji wake. Wasije wakajikuta wanaitwa majina na kina Makamba!
 
Ni kongamano zuri kwani kihistoria wasomi watanzania hawajwahi kuwa na mwavuli wao binafsi wakujadili mustakabali wa taifa lao.

Waandaaji wazingatie tahadhari mbali mbali zitakazopelekea mwavuli huu kutekwa na wanasiasa au wale wote wenye kutamani zaidi vyeo kwa faida ya nafsi zao..

Mwanzo mzuri TPN tunatarajia maamuzi bora ya kutupeleka mbeleee...
 
Hawa wanaojiita wana taaluma hawana jipya bali wanatumiwa kama front kujaribu kucounter effect za KONGAMANO lililoandaliwa na Mwalimu Nyerere foundation!! Kongamano hili litakuwa ijumaa na jumamosi yamepamgwa maandamano ya kuwalaani wote wanaomkosoa Jakaya kwenye kongamano la mwalimu; sasa kama sio mbinu za kujikosha na kutaka kuhalalisha ufisadi ni nini basi? Wanataaluma wa kweli ni wale waliokuja kutoa maoni yao kwenye kongamano la wazi la Mwalimu Nyerere na sio hawa wanaoweka kiingilio kwenye kongamano ili wale wanaowajua na wenye fikra kama zao ndio waweze kuhudhulia na kupata press coverage!! I will not be surprised kama mwana Mtandao maarufu V.C. wa UDSM Mukandara anatumika katika hizi mbinu chafu za kudhoofisha fikra endelevu!!
 
Binafsi naamini TPN itafika mbali. Ni muhimu tuwe wavumilivu na kutoa ushauri na changamoto za kuweza kuisaidia TPN kufanikiwa katika mipango yake. Naamini wengi wetu humu ni wataalam katika fani mbalimbali, nashauri tuangalie uwezekano wa kujiunga nayo na kuhakikisha inafika mbali kwa maslahi ya taifa letu na watu wake hasa vijana na watoto.
 
Mimi nina matumaini sana na hawa jamaa. Lakini, tutapima ni maazimio na utekelezaji wake. Wasije wakajikuta wanaitwa majina na kina Makamba!

MKJJ, nadhani kuunguruma kwao kutategemea wanaungurumaje. Kukiwa na mwelekeo ama elements za kukosoa utendaji wa Serikali ama kutoa tu ushauri wa nini kifanyike yanaweza yakawa yale yale ya Kongamano la kukumbuka kifo cha Mwalimu. Kongamano hilo litashutumiwa, yatatajwa majina ya waliosema hili na lile.

Kwa 'ujinga' wangu nilidhani yaliyosemwa na Wazee kwenye Kongamano la Mwalimu Nyerere, kwanza yataheshimiwa kwa kuwa yametoka vinywani mwa Wazee wa nchi hii, baadaye yatachujwa, yatachukuliwa ya msingi, na hatimaye yatafanyiwa kazi na Chama (CCM) ama na Serikali kwa manufaa ya taifa letu. Lakini, baada ya matamshi ya Makamba na Rais mwenyewe, na yaliyokuwa yakiripotiwa kwenye vyombo vya habari, ni wazi wananchi wameaminishwa kwamba Kongamano lile lilikuwa likimuandama Rais!

Tusubiri tuone la wasomi kitapokelewaje.
 
Back
Top Bottom