Kuungua kwa majokofu na majiko majumbani kwa hitilafu za umeme: Sheria iko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuungua kwa majokofu na majiko majumbani kwa hitilafu za umeme: Sheria iko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Steve Dii, Apr 3, 2009.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kukatika na kurudi kwa kasi kwa umeme kumesababisha fridge na jiko tulilonalo liungue. Nifanyeje kuwa shitaki kwa ajili ya kutulipa fidia hawa Tanesco?! Inauma sana kuona hivi vifaa vinaharibika kwa sababu za hitilafu za umeme. Je, kuna sheria yoyote inaweza kutumika kuwabana hawa Tanesco? Please help.
   
 2. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Pole sana kwa kuwa sheria zetu ni copy/cut and paste, vyuoni ilijulikana kama ku-cram au kumeza, itabidi hapa tuangalie sana waingereza idara yao ya nishati inasemaje wanapokuwa na case kama hizo zinazotokea Tanzania na haswa zikisababishwa na TANESCO the "rabid" company
   
 3. B

  Balingilaki Member

  #3
  Apr 4, 2009
  Joined: Aug 2, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole kwa kupoteza mali zako kwa namna hiyo uliyotaja,,,,,sawa kopi au pesti lakini na sisi pia tunasheria kama hizo hasa katika sheria ya madhara (law of tort) na kama tanesco wanakata umeme ni lazima watoe taarifa kwa kila mdau au kupitia magazeti au vyombo vingine kama tv na redio nk

  Kama uliunguliwa na ilihali ikiwepo taarifa kutoka tanesco na kwa kutojali ukaacha jokofu kwenye umeme itakuwa ngumu kulipwa.

  Na lazima kwenye shitaka uoneshe wajibu wa tanesco kwa mteja ikiwa ni pamoja na kutoa habari
  pia uoneshe kuvunjwa kwa wajibu yaana kutotoa habari kwa mteja na

  pia uoneshe madhara uliyoyapata ikiwa ni kuunguliwa kwa jokofu


  case laws donoghue v.stevenson , benson bezibwa v.cocacola kwanza ltd etc alafu tukikosa kabisa kwetu tunaenda katika JALA s.2(2)
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante mkuu B na pole sana ndugu yetu SteveD. Maelezo hapo juu ni mazuri sana ila kuna mtu aliniambia kuwa kwa hali ya Tz inakuwa ngumu kuwashitaki Tanesco. Kama sikosei, nakumbuka kuwa kuna suala la uwekaji umeme (electrical installation) ambalo jamaa wanatumia kukwepa kulipa fidia. Alinambia kuwa inabidi mambo ya kufunga nyaya na vitu vyote vya ndani yawe yamepitiwa na wataalamu wa Tanesco na kukubaliwa. Sina hakika lakini kama hiyo kweli basi uwezekano wa kulipwa ni mdogo sana endapo ufungaji wa nyaya ulifanywa na mafundi wetu wa mitaani kama wengi tunavyofanya. Yaani kuna kitu zaidi ambacho hawa jamaa hawaweki wazi ila wanakitumia kuruka viunzi.
   
 5. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kuna declaration forms ambazo ni sehemu ya mkataba na TANESCO. Kuna haja ya kuliangalia hilis suala upya na kuleta sheria zitakazomlinda mtumiaji. Sera na sheria zilizoanzisha TANESCO zimepitwa na wakati.

  My Take: to avoid the hasle of the legal system...make sure you insure your properties. It is cheap and more secure than the path to sue TANESCO which is not a guarantee to succeed.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu S,

  Hao insurance wa Tanzania wanaeleweka? Kuna jamaa yangu alipata matatizo ya kuunguliwa na gari lake ambalo aliliwekea comprehensive insurance. Huwezi kuamini aliombwa atoe pesa ili wamsaidie. Sasa hapo kuna kitu kweli? Umepata hasara halafu unatakiwa kutoa pesa nyingine!
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Rushwa imeshakuwa kama desturi Tanzania.Ni wapi utapata huduma unayostahili bila rushwa?

  Unajua Sector ya insurance ina fraud sana.Wafanyakazi wanashirikiana na matapeli/fraudsters ili kubuni namna ya kupata malipo hewa.Wafanyakazi wa insurance nao kwa uzoefu huo hufikiri kila mtu anayedai ni tapeli na ndiyo maana huomba chochote ili wasaidie!
  Tena hao TANESCO ndo usiseme.Watakusumbua weeee mpaka utamani kuwa shoot!
   
 8. I

  Ikena JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 482
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 60
  Nilishawahi kudokezwa eti unatakiwa ku- declare vifaa vyako vyote Tanesco, na pindi kimojawapo au vyote kuungua, wao ndio watakua na wajibu wa kuvilipa baada na kufanyia uchunguzi.

  kuna tetesi kuwa, zamani wasomamita walikua wanatumia idadi ya vyombo vinavyotumia umeme unavyotumia ku-determine bill yako ya umeme, bila wao kwenda kwenye site, na ikapelekea wananchi kutokuorodhesha vifaa vyao.

  Nitafuatilia nione kama kuna ukweli.
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Dark City, akhsante kwa maelezo kuhusiana na vipengele ambavyo wanaonekana kuvitumia hawa Tanesco. Lakini mkuu, iweje wao kama professional public-private company wakubali kuunganisha umeme kwenye nyumba ambayo wanajua haikidhi kuunganishiwa huu umeme? Watanzania tunahitaji mshikamano na kuanza kuonesha kuwa wanapotu shambulia na kutukatia umeme kwa kuchelewesha kulipa bill za matumizi, vivyo hivo tudai haki zetu kama wateja ambao wana deserve better.
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu Shadow, unajua wote tukikimbilia insurance as a way to avoid kuwawajibisha hawa Tanesco hatuchelewi kukuta hata Tanesco wenyewe wanaanzisha biashara ya insurance. Avoidance pahala ambapo tunajua tuna haki yetu kwa kweli sioni kama ni jambo la kuleta solution ya muda mrefu kwa wengi wa watumiaji hapa nchini. Kutaleta ongezeko la kampuni za insurance tu na kushindwa kutatua tatizo la irresponsibility walilonalo Tanesco.

  In fact mimi nafikiria kuanzisha kampeni ya kuhamasisha watu tuanze kuidai hii kampuni, kama moja ya hamasa ya kulifanya shirika hili lifanye kazi zake kiufanisi zaidi, labda hata kupunguza matatizo yetu ya umeme, ambayo naamini chanzo kimojawapo kilichotufikisha sisi hapa ni kule kuzidi kuwaachia achia kwa kero mbalimbali wanazotusababishia sisi wateja. They have become complacent to an extent that they don't even have own strategies to move forward. Of course, to the detriment of the nation as whole economically.
   
 11. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Mimi nafikiri, kisheria kama una back ups za kutosha (e.g. wiring ilikuwa confirmed na TANESCO) and kama kweli tatizo ni uzembe wa Tanesco, kwa mfano kuungua kwa Transformer au kuanguka kwa nguzo, hapo, lazima ulipwe. And I think watanzania tumekuwa wapole sana ndio maana hata hawa Tanesco wamekuwa wakituchezea sana.

  Kwa upande mwingine, kuna maeneo kwa mfano Makumbusho Dar es Salaam, huko kuna transformer moja linaitwa kwa mateja. Halooo, jamaa wanaotumia hili transformer, kuna msimu huwa wanakoma kabisa. Inaweza kufululiza wiki nzima ikifika saa tatu tu, umeme unakatika. Yaani kuna mkazi wa huko aliwahi kuniambia, hawa jamaa wanajua kuna kitu kinacholeta shoti but they are leaving it, ili wapate overtime. Hili transformer limekuwa likipata shoti mara kwa mara, and Tanesco wana taarifa kamili as umeme ukikatika tu, mtu akapiga simu na kusema anatoka makumbusho, utasikia tu, "ni transformer la mateja". Sasa kama Tanesco wanajua kuwa hili transformer ni feki, and they are entertaining it, siku makumbusho ikigeuka makaa kwa nyumba kuungua, wewe unafikiri Tanesco kisheria hawatakuwa held responsible kweli...??

  Nchi zilizoendelea, naamini umeme hata ukikatika kwa masaa machache ndani ya siku 365, basi hapo claims zitakuwa za kumwaga. Bongo, wanakata wanawasha, wanachezesha mpaka TV za walalahoi na wasio walalahoi, zinaungua, but hakuna anayeclaim. I think, watanzania tuunganishe nguvu na kuanza kuwabana hawa watu. Tanesco inaishi kwa kodi zetu, and on top of that, tunawalipa kwa huduma za umeme, then wanatuchezea shere. They must be held responsible.
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kishazi, ile siku tunaunguliwa wala hatukupata chance ya kuzima swichi. Ni kawaida kwamba kila pale umeme unapokatika, tunahakikisha vyombo vyote vya ndani vinakuwa vimezimwa mara moja. Lakini siku hiyo ile tunakimbilia kuzima tu umeme huo umesharudi tena kwa fujo na kuunguza hivi vifaa. Mimi nadhani kuna fundi mmoja alikuwa sehemu sehemu kwenye mamitambo yao ambayo alitakiwa akate umeme pahala lakini akajikuta amekata sehemu isiyo na kuamua kurudisha umeme bila kufata taratibu.

  Kuna ndugu mmoja nimeongea naye amesema wao nyakati za nyuma waliunguliwa na nyumba kabisa, na hamna fidia waliyofanikisha kuipata. Tuungane kuwabana Tanesco, wamezidi.
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Steve,

  Si vibaya kujaribu kuwatimulia vumbi ili ukifanikiwa wengine wafuate mfano wako. Hata hivyo ujue kuna mlima mrefu wa kupanda. Kila kitu kinawezekana kwa hiyo jipige kifua usonge mbele!

  Kwanye post yako nyuma kidogo umeuliza kama Tansco wanaangalia professionalism. Hilo limenichekesha sana. Sina hakika kati ya mashirika yanayoitwa ya umma hapa Tz kama kuna hata moja linaloangalia hicho kitu. Kwa hiyo Tanesco hawawezi kuwa tofauti na wengine. Mambo ya kuangalia kama wire zimewekwa vizuri wala hayaangaliwi kwa sababu kinachofanya kazi hapo ni nguvu ya pase kama mlevi anavyopelekeshwa na dozi ya alcohol.

  Ndiyo maana mimi natamani sana (ingawa najua haiwezekani) kuiona Tanesco imekufa na kufutika katika uso wa dunia. Dawa ya Tanesco ni kama ile iliyotolewa kwa TTCL. Shida hapa ni kuwa mafisadi wanatumia mwanya huo kuhujumu mashirika ya umma ili wapate faida kubwa kwenye makampuni yao. Kama hawa jamaa wangepata wapinzani wa nguvu, amini usiamini siku moja tunaweza kuwa na TiGo au vodafasta kwenye umeme.
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  tatizo kubwa ni kwamba, nyumba nyingi na hasa zinazoungua, huwa ni za walalahoi, ambao wamewachukua vishoka wasojua umeme ili wawaunganishie nyumba zao umeme, pili, nyaya nyingi huwa ni za kichina, hivyo ni rahisi kusababisha moto wakati wowote. liability hii yote iko mikononi mwa mwenye nyumba, na sio tanesco. wewe unapojenga nyumba yako, hakikisha umewatafuta mafundi walosomea vizuri, pili nyaya lazima ziwe imara na genuine, unatakiwa pia kama tanesco wanakatakata incase, zima main switch hadi pale watakapowasha. wewe ndio unatakiwa kutake care of your house. pia, wewe binafsi unao wajibu wa kuiwekea bima nyumba yako. Tanesco wanachofanya ni kuuza umeme kwenye nyumba yako, sio kulinda nyumba yako kwasababu wao hawakai pale. ndo maana ukienda kuomba waje kurekebisha au kufanya chochote kwako, wanakuja kuorodhesha kila kitu ambacho unacho ndani nk ili kujivua liability. nasikitika kuwataarifu kuwa, hata nyumba au kitu chochote kikiungua, hauwezi kupata fidia toka tanesco, labda upate toka kwenye bima yako, au anza maisha upya.

  hapo ndo watu wanaopenda vitu vya bei rahisi(vitu vya kichina hasa nyaya za umeme) watajiju.
   
 15. B

  Balingilaki Member

  #15
  Apr 14, 2009
  Joined: Aug 2, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata kama umeme umefungwa mtaa gani tanesco ndo shirika pekee la kuweka umeme na kila m2 atakaye weka umeme lazima apeleka wiring plan tanesco nao watume m2 wa kukagua jinsi wiring ilivyofanyika.....hivyo tanesco is liable in default.....
   
 16. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tanesco hawako liable for anything other than matatizo ya transformer yao, au kudondoka kwa nguzo yao. ukileta vifaa chakavu kwenye nyumba yako, watakusumbua sana kwenye fidia. tumeona wengi wamekosa hilo. labda kwasababu sheria haina upande wa shilingi, inategemeana, pengine kesi yako wewe ndo itakuwa landmark ya kwanza, kuweka msimamo huo hapa tz, ila kwa kipindi cha nyuma, fidia hiyo ni ngumu kupata na mara nyingi hutapata labda kwa hayo niliyosema hapo juu. tuwe makini na mafundi vishoka, nyaya za kichina nk.bidhaa bandia na vitu vya bei rahisi ambavyo tunavipenda ndo tatizo hapa.
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ubungoubungo, ukisema kama hivyo hapo juu, ya kwamba Tanesco hawako liable na kitu chochote; basi kweli hili litakuwa tatizo letu. Tumekubali vipi kufanya biashara na kampuni isiyokubali makosa pale ikoseapo?! Au Tanesco ni kampuni ambayo haifanyi makosa?!

  Kuhusu nyaya za Kichina na vitu bandia, hapana. Navijua vitu genuine na niko makini navyo. Fridge iliyoungua ni aina ya Miele, kampuni moja maarufu ya Kijerumani. Jiko lililoungua ni make inayotengenezwa Uingereza, HotPoint.
   
 18. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Inabidi kwanza aweze ku-establish causation... Je ni kweli kwamba Tanesco walitoa taarifa kwamba umeme utakatika siku na saa fulani? kama ni kweli basi uzembe wako huwezi kulipwa maana ulijua umeme utakatwa na kurudi muda uliowekwa, kama hapana basi establish kama vitu hivyo vimeungua kwa uzembe wa Tanesco au ubora wa vyombo vyenyewe maana kesi yaweza kufunguliwa kati ya watengenezaji wa vyombo au Tanesco...
   
Loading...