Kuunga Mkono kila Hoja: Wabunge wa CCM wanajali chama chao kuliko Tanzania!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
17,871
33,235
Kwa wingi wao bungeni ilitarajiwa maslahi ya nchi yetu yaboreshwe na wabunge wa CCM, lakini badala yake wabunge wa upinzani walio wachache, ndiyo kila siku wanahangaika na hatima ya nchi yetu.

Hadi wakati mwingine najiuliza kama wingi wao ndiyo umewatia upofu wa fikra ama ni mahaba kwa chama chao ndiyo umewafanya wawe kama ndodocha kwa kila liletwalo na Serikali Bungeni.

Wabunge wa CCM Kila siku wakichangia mada bungeni, utawasikia wanalalamika kama vile nchi inasambaratika dakika inayofuatia, lakini muda kidogo baadaye wanaunga mkono kila jambo linaloletwa na serikali bungeni.

Kila siku wanauliza maendeleo yaliyoko kwenye majimbo ya wapinzani kama vile kwenye majimbo yao kuna maendeleo yaliyotukuka. Leo hii Livingstone Lusinde eti anahoji maendeleo ya Jimbo la Iringa mjini wakati jimboni mwake watu wanakunywa maji kwenye bwawa pamoja na Ng'ombe.

Wabunge wa CCM ni hasara kwa taifa kwa kuwa wanalipwa mishahara na posho kwa lengo la kuishauri na kuisimamia serikali, lakini wao kazi yao ni kuisifia na kuipamba hata kwa mambo yanayoumiza watanzania.

Ukitaka kujua uimara wa wabunge wa CCM, gusa chama chao!!
 
JF Kwenu,

Wako Waheshimiwa Wabunge walioishia darasa la saba katika vyama vyetu vya siasa, wengine wanajua kujenga hoja ila wengine, tens wengi ni watu wa kuunga mkono hoja bila kufikiria. CCM inaongoza kwenye orodha.

Hawa ni wa CCM

1.Jaffar Juso-Paje
2.Hussein Nassor Amar
3.Haji Haji
4.Mwantumu Dau
5.Mbaraka Waziri-
6.Deo Sanga-Anapiga kazi
7.Hamis Yahya Machamo.
8.Steven Ngonyani(Prof.Maji Marefu)-Anapiga kazi vizuri
9.Joseph Kasheku Msukuma-Geita, Ana mdomo sana
10.Livingstone Lusinde Kibajaji-Ana mdomo sijapata kuona
11.Mary Chatanda-Alisababisha mtafaruku uchaguzi wa madiwani Arusha.
12.Boniface Mwita Bunda (V)
13.Boniventura Kiswaga -Magu
14.Ali Kesi -Nkasi, Ana domo balaa
15.Lamerck Airo-Rorya
16.Vedastus Mathayo-Musoma(M)
17.Jumanne Kishimba-Ana vijisenti
18.Saul Amon(S.H Amon)-Ana vijisenti
19.Aziz Abood-Ana majisenti, Marafiki wanasema amesoma Forest Hill Sec. Morogoro.

20.Frank Mwakajoka, CHADEMA Tunduma
21.Suleiman Bungara, CUF Kilwa Mjini.

Aidha wabunge wa CHADEMA wa kuteuliwa wana shahada kuliko wengi wa CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafikiri kwann uhakiki haujapita ngazi za juu? Ccm waliogopa kuwapukutisha wanaccm wao. Wanajijua vyema. Huo uhakiki ungefanyika kwa haki hata kairuki leo hasingekuwa waziri. Angekuwa ameshasombwa na maji.
 
Mkuu unadhani yale makofi na kugonga meza Bachelor holder na kuendelea anaweza kufanya ujinga ule.Halafu ndio wakajadili mikataba ya gesi na madini.Hili ndio lile kundi la ndiyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo.
 
Umbumbumbu wa wale wabunge ndio mtaji haswa wa CCM na ndio minyororo ya ujinga na umasikini wa watanzania.
 
Naomba nambie Mbunge gani wa Upinzani anapigania maslahi ya wananchi. Je ushaona ajanda gani zinazogusa wananchi zinazotolewa na Serikali wabunge Wa Upinzani wanapongeza Au kuunga mkono. Hao wanasiasa waache tu.

Kama wewe una yako sema hatuyajui. So unapoamua kudiscuss Watu jirudie mwenyewe kwa kuapply kwako.
 
Naomba nambie Mbunge gani wa Upinzani anapigania maslahi ya wananchi. Je ushaona ajanda gani zinazogusa wananchi zinazotolewa na Serikali wabunge Wa Upinzani wanapongeza Au kuunga mkono. Hao wanasiasa waache tu. Kama wewe una yako sema hatuyajui. So unapoamua kudiscuss Watu jirudie mwenyewe kwa kuapply kwako.
We utakuwa mgeni katika siasa za Nchi hii,hakika nnasema,kwa hiyo ufisadi wote uliosemwa na hata kutikisa Nchi ulisemwa na Ccm?,kwa mfano Escrow,Richmond,Dowans, IPTL na mingine ming Wabunge wa Ccm ndiyo waliifichua?,tutajie Ufisadi ambao Ccm waliufichua ambao unaoujua wewe
 
Kwmy Sakata la kutaka Masha awe Mbunge nami Chadema walikuwa wanasimamia Maslahi ya Nchi?

Tusidanganyane hakuna Upande unaopigania Maslahi ya Nchi kila upande unapigania Maslahi yake

Kwny Posho na Marupurupu ya Wabunge wote huwa kitu kimoja!
 
Kwmy Sakata la kutaka Masha awe Mbunge nami Chadema walikuwa wanasimamia Maslahi ya Nchi?

Tusidanganyane hakuna Upande unaopigania Maslahi ya Nchi kila upande unapigania Maslahi yake

Kwny Posho na Marupurupu ya Wabunge wote huwa kitu kimoja!
Masha na CHADEMA ilikuwa ni mambo yao ya kichama.

Kwa ivo unataka kutambia bunge letu halipiganii maslahi ya watanzania?

Ule msemo wa "asiyefanya kazi na asile" unaelewa mantiki yake? Maana yake anayefanya kazi ale. Posho na Marupurupu kama wanafanya kazi haina shida, tatizo wabunge wa CCM hawana walifanyalo na Posho na marupurupu wanachukua!!

Unajua kama Leone Messi analipwa shilingi Bilioni kumi na nne, milioni mia tisa sabini na tisa, laki tatu themanini na tatu elfu, mia sita sitini na mbili na senti saba (14,979,383,662,07) kwa mwezi? Umewahi kusikia Barcelona wanalalamika?
 
Kama kuna mtu anahisi kuna mwanasiasa anapigania maslahi ya nchi au mtu mwingine basi huyo mtu anataahira ya akili.
Lengo kuu la chama cha siasa ni kushika dola chama sio NGO hata siku moja.
Ukiona watu wanahangaika kututia ganzi tuone kama wanakawema flani lengo kuu ni ukifika uchaguzi tuwape nchi.
Waliopo hawataki kutoka wasiokuwepo wanataka kwa nguvu zote kuingia.
Siwezi kuingia kwenye siasa za nchi hii zinautoto mwingi sana na ujinga wa wanachi umekua mtaji rahisi sana
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom