Kuunga mkono CCM ni laana. Ushahidi ni kundi la Ze comedy

Chenge mbona haguswi?? Jibu swali


Hana mgogoro wa kimadaraka na wenye nchi. Ni sehemu ya kujenga mfumo CCM .
Sio tishio kwa walioko madarakani na wale wanasaka madaraka.
Ukiangalia kwa haraka Kashfa za Escrow na Lugumi kashfa nyingi za miaka kumi ya utawala wa JK iligusa watu wachache wa ukanda mkubwa. Na hii ilikua ni maandalizi ya uchaguzi ili fedha hizo zitumile kwenye kampeni na kuhakikisha ukanda mkubwa unaipa CCM ushindi.

Hii nchi ina mafisadi wakubwa sana lakini hawaguswi kwa sababu hawana mvuto wa kisiasa na sio wanasiasa.
Ukitaka Chenge ashambuliwe kama mpira wa kona basi aonyeshe nia ya kugombea kwenye nafasi ya urais au uspika.

Hata Kwenye nafasi ya spika wa bunge amekua akijiweka pembeni ili tu asiingie kwenye migogoro ya kuchafuana na kuwhughulikiwa japo Chenge ndiye mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza bunge.

Pia Chenge hakuna mahali alipoiba yeye kama yeye zaidi ya kupewa fungu lake kama mshauri wa kisheria sasa utamshitaki kwa lipi!

Magufuli kama kweli anataka ajue nani ametumia mali za umma kujilimbikizia mali basi afanye sensa ya kuzitambua mali zote zilizopo Tanzania ndani na nje ya nchi ili ijulikane nani anamiliki nini na amevipataje wakati aliku sio mfanyabiashara na hakulipa kodi popote. Hapo atakua ametenda haki.
 
Hiyo sio hoja kufanikiwa ni fikira sio kuwa ccm au chadema

Angalia kwanza elimu za hao watu alafu urudi hapa!!
Umenena mkuu! Hapa sio Orijini Komedi tu Bali ni bongo movies wote na bongo fleva. Elimu zao walio wengi ni f4 failure na std 7. Kumbukia wakati wa kampeni ndipo utajua.
 
wewe ni walewale tuliokuwa tunaambiwa malofa walahi tena. kwa hiyo ulitaka waunge mkono wale watuhumiwa wa ufisadi ili waende ikulu kwa mara nyingine waendelee kuifisadi nchi. hahahah. umekwisha. nakwambia upinzani ungekuwa kwenye ubora wake kama kundi la watuhumiwa wasingepokelewa. haiwezekani watu uliokuwa unawakashifu mafisadi kwa miaka kadhaa na ambao ulikuwa unasema una ushahidi wa kutosha na hawawezi kamwe kusafishika, leo hii umewasafisha ndani ya kipindi cha siku thelathini na tayari ukawaandaa kwenda ikulu. khhaaaaaa. hata mjinga yoyote hawezi kubali upuuzi huo. mliokuwa mumenunuliwa basi ulaji umeshatoweka sasa mnaweweseka tuu
Si mahakama ni zenu? Mnasubiri nini kumsulubisha? Tumia akili wewe, za kuambiwa changanya na zako
 
Ukweli mimi nimiongoni mwatu ambao walipoamia ktk kituo icho ikawa mwanzo namwisho kwakua nasjui kamaipo skuu ambayo kilaludisha imani namimii
 
Usidhani wote waliishia darasa la saba kama ww. Nenda kasome ripoti ya kina Mwakyembe kuhusiana na Richmond utajua Richmond ni nani . Usiwe mvivu wa kusoma.
Mimi niliisoma, lakini hakuna mahali pametajwa Richmond ni ya nani. Ila baada ya Lowassa kujiunga CHADEMA Lissu akiwa kwenye Kampeni Morogoro akasema Richmond ni ya Kikwete, lakini Kikwete akajibu kwa mafumbo kwamba mwenye Richmond ni yule anayezunguka na Lissu kwenye Kampeni. Unadhani ni kwa nini Lissu alikuwa na ujasiri wa kumtaja kwa jina Kikwete lakini Kikwete tena akiwa ni Raisi wa nchi akatumia mafumbo?
 
Hiki kikundi kilikuwa maarufu sana kwa uchekeshaji , hasa kilipokuwa ITV , hujuma zikafanyika kikahamia kule kwenye majanga , kule kusikokuwa na watazamaji TBC 1

Basi baada ya hapo wakaamua kukiingiza rasmi kwenye mustakabali wa CCM , na kwa vile inafahamika kwamba kila anayejiegemeza CCM ni lazima atandikwe kofi la Mungu , hawa vijana ndoto zao zimeyeyuka kabisa, hawaonekani, hawasikiki na hata wakionekana hawajiamini tena, maana ile dhambi ya usaliti inawaunguza .

Hili liwe somo kwa wasanii wengine , kama hujababuka leo basi jua utababuka kesho .
Ni kweli mkuu... Sasa kila mmoja anahangaika kivyake, Sijui Mpoki alikuwa kwenye u Mc lakini kuna siku aliboronga, Masanja kawa mchungaji sijui, Joti maskini ya Mungu amebaki kuigiza Kademu maskini ya Mungu lakin wapi..... Wale wengine sijui wako wapi
Mtoa post umeongea ukweli mtupu
 
hahahah Allen usikariri. unataka kuniambia umeshayasahau matamshi ya makamanda Lissu ,Lema, Dr Slaa, Msigwa, Mnyika, na wengine na bila kumsahau Kubenea na magazeti yake ya mwanahalisi jinsi walivyokuwa wakizungumza skendali ya richmond. unataka kuniambia walikuwa wanatania? usijifanye kufumbia macho bwana. kama ni ukweli yakisemwa tukiri kweli tulisikia. na kama tuliamua kuwasafisha, je kwani sisi ni vyombo vya dola? ?. na je yale maushahidi waliokuwa wanasema wanayo yako wapi
Kesi za ufisadi anayepaswa kuzipeleka mahakamani ni DPP na siyo LISU wala MBOWE.Kuna chama kinahisiwa kuwa kina fisadi lkn kuna CHAMA kinathibitika kabisa kuwa kina MAFISADI.DPP afanye Kazi yake kumaliza huu mkanganyiko.
 
ningeomba kabla ya kuigeuza kwanza tuijadili upande huu tumalizane. then tuhamie upande wa ccm. tusirukeruke mambo kamanda. tusikwepe hoja za msingi. wewe unawazungumzia ccm wakati aliyekuwa mwenyekiti JK hakuwahi kusema yule ni fisadi. alisema mikataba ile ilifanyika chini ya usimamizi wa Lowasa. ila upinzani sasa ndio ukavalia bango na kuchimba maushahidi wanayoyajua na miaka zaidi ya nane wakaendelea kutuhubiria kuwa jamaa ni fisadi. umesahau mara hii. unafanya makusudi tuu

Tuanze vizuri zaidi: Je, wewe binafsi hujui au huamini kuwa Lowassa ni fisadi? Mimi binafsi sikuwahi kuamini kuwa Lowassa ndiye muhusika mkuu wa Richmond. Ndio maana sijawahi kuona JK akiongelea suala hilo kwa kujiamini sawasawa. Kama vile kuhusu Tegeta Escrow account. Anaishia kupiga blabla tu. Hata hao CHADEMA kumshambulia Lowassa kwa nguvu kuhusu Richmond nilichukulia ni mkakati tu wa kisiasa kuigonga CCM. Na kama CCM chini ya Magufuli haitaweza kusimama kidete kuhusu kashfa hizo na nyinginezo, tena baada ya kuanzisha mahakama ya mafisadi, basi isahau kufikia "moral high ground" ya kumnyooshea kidole Lowassa na CHADEMA.
 
Mkuu kuna huyu Msaga sumu kawa maarufu sana by this time
Siku niliposikia jina la Msaga sumu kwa mara ya kwanza ni kutoka kwa kijana aliyekuwa ana msisimko wa ajabu akitaka uwe wimbo wa simu yake (Ring Tone) kisa msaga sumu anasema "ukweli".
 
we unasema hivyo wakati wasanii ndio wanarudi ccm.! hivi karibuni wamerudi wangapi. cheki mwenyewe. usijipe moyo usiokuwa na mashiko yoyote
Ndio maana wanaitwa wasanii! Wanaishi maisha ya kisanii!
Hao wanaokenguaka huku na huko hawafai kuwa kioo cha jamii...
Njaa ndio zinawasumbua hakuna kingine zaidi, na wala hawana impact yoyote kwa mwananchi wa kawaida, wenye akili zao huwapuuza tu!!
 
hiyo waulize wana ccm. mimi niulize habari za chadema asilia. ambao tumeamua kum support Magufuli na sera yake ya hapa kazi tu. ufisadi na mafisadi zika kulee. chadema ya sasa unajua haina ajenda tena. sijui wanadandia ipi


Mkuu nafikiri kila awamu Ina mapungufu yake sio miaka yote ni ufisadi, ndio maana CHADEMA walipiga kelele kuhusu ufisadi na leo magufuli anapinga ufisadi japo ni kwa njia ya kukurupuka, Lakini nikuulize kitu, kama LOWASA asingekuja chadema na wakati huo ufisadi magufuli anaukemea ina maana chadema isingeendelea kuwepo?

Je wewe ungeendelea kuwa chadema au ungehamia CCM?

Kazi ya upinzani ni kuona mapungufu yanayofanywa na serikali na kuyapinga.
Siku njema mkuu
 
Hiki kikundi kilikuwa maarufu sana kwa uchekeshaji , hasa kilipokuwa ITV , hujuma zikafanyika kikahamia kule kwenye majanga , kule kusikokuwa na watazamaji TBC 1

Basi baada ya hapo wakaamua kukiingiza rasmi kwenye mustakabali wa CCM , na kwa vile inafahamika kwamba kila anayejiegemeza CCM ni lazima atandikwe kofi la Mungu , hawa vijana ndoto zao zimeyeyuka kabisa, hawaonekani, hawasikiki na hata wakionekana hawajiamini tena, maana ile dhambi ya usaliti inawaunguza .

Hili liwe somo kwa wasanii wengine , kama hujababuka leo basi jua utababuka kesho .
Hicho Kipindi kwani bado kipogo?

Kinarushwa siku gani? Waliingizwa mkenge ikawagharimu. Ni watatu tu Miongoni mwao wameendelea kufanya vizuri na wenyewe wamebebwa na vipaji vyao ambavyo vimesaidia kuwapatia kazi nyinginezo nye ya kikundi Chao.
 
Back
Top Bottom