Kuundwe wizara rasmi itakayokuwa inashughulika na mambo yasiyokuwa ya muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuundwe wizara rasmi itakayokuwa inashughulika na mambo yasiyokuwa ya muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MKWECHE, Nov 30, 2011.

 1. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mie mkweche Mzee wa Igangidungu nimetafakari sana na Kujiuliza kwanini Masuala yasiyo ya Muungano hayana Wizara na Waziri wake?!Manake maswala yasiyoya Muungano manake ni ya Tanganyika,Je kwanini hayo yawe yananing'inia wakati nasisi ni Ardhi ndani ya Muungano.Na yanatamkwa bila woga kwenye Katiba!Mie naona kama hajatiliwa makazo vile
  Wenzetu wamejizatiti wana serikali kabisa yenye bunge kamili(Baraza la wawakilishi),Katiba nzuri kamilifu na Wimbo wa Taifa lao tukufu.
  Kimsingi wao wananafasi 'Faragha' ya kuzungumzia mambo yao kwa Uzuri.Ni vizuri na Ni Haki Yao!
  Upande wa Pili Je kwanini sisi hali ya kutokuwa na mfumo rasmi wa kusimamia mambo yasiyo ya muungano iwe Kawaida laukama kwa jicho la pili naona yananing'inia!
  Kwa Kuanzia mie mkweche ningependa Ndg.Dkt Jakaya ateuage na kuunda wizara rasmi ya kushughulika na majambo yasiyo ya muungano,nasisi tunaoguswa na hayo yasiyo ya muungano tuna mengi ya Kupigania na Kusimamia Jamanii ili nayo yaende sawa sawa!
  Kimsingi Wizara zote zilizopo ni za Jamhuri ya Muungano na Waziri anaweza toka kokote(Kule au huku) ila Je Yasiyo ya Muungano yanakaakaaje nayo waziri aweza toka kokote?!
  Kuna wengine wanasemaga Mie Mkweche eti ni 'Ngumbaru'ila wanasahau mie Tayari ni Mkweche!
  Nawasilisha Kimkweche mkweche munifafanulie Jamanii!
   
 2. i

  iMind JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mfumo wa muungano wetu ni kwamba serikali ya jamhuri ya muungano itasimamia mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika ambayo siyo ya muungano. Na itaundwa serikali ya zanzibar kwa ajili ya kushughulikia mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa zanzibar. Hivyo serikali ya Tanganyika ili deligate powers zake kwa serikali ya muungano halafu ikafa. Huu ni utaratibu tu uliokubaliwa kwa wakati huo, ambao kimsingi una faida nyingi kuliko hasara. Hata hivyo binafsi sioni shida kwa nini wati wasipewe nafasi ya kupitia upya utaratibu huu na aidha kuamua uendelee au kuja na mfumo mpya.
   
 3. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo Waziri wa wizara akiwa Mzanzibari anaendelea kusimamia hata mambo yasiyo ya muungano?
   
 4. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Mkweche hoja yako ni nzito na muhimu. Hicho ni mojawapo ya mambo makuu yanayokera katika ndoa hii ya Tanganyika na Zanzibar. Kwa lugha ya mitaani kwetu ni "changu changu, chako chetu". Wazanzibari wana serikali ya kushughulikia mambo yao. Sisi Wabara (kama wanavyopenda kutuita) kila tunachotaka kufanya ni lazima tupate idhini ya Wazanzibari kwa sababu kila kitu kipitishwe na serikali ya muungano ikiwa ni pamoja na bunge la muungano! Ninaposikia wanalalamikia muungano huwa ninashangaa. Wana nguvu kubwa kuamua cho chote juu ya maisha na mustakabali wa Wabara!!!!
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kabla sija-declare kwamba huijui Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, hebu fafanua usemi wako hapo juu!
   
 6. k

  kicha JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  huu ni mgandano wala si muungano, hata kiongozi wa nchi anashindwa jinsi ya kuulezea, ipi ni haki ya nani na ipi haki ya nani ila ukiulizia utaambiwa wazenji haweshi kulalamika au chadema hawapendi muungano au nyerere aenziwe wakati mambo vurugu mechi
   
Loading...