Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KONGAMANO la siku mbili lililoandaliwa na asasi ya Concern for Development Initiative in Africa (ForDIA) lilimalizika jana (Ijumaa 8 Mei 2009) jijini Dar es Salaam kwa mafanikio katika maeneo mawili makuu kitaifa na kimataifa:
1. Wadau waliamua kuunda upya tawi la asasi ya kimataifa ya kupigania uwazi na kupambana na rushwa Transparency International (TI) kwa kuipa sura ya kitaasisi na hadhi ya kisheria.
Jina la Tawi la Tanzania litakuwa Tanzania Transparency Forum (TRAFO).
Katika muktadha huu, wadau walichagua Kamati ya Muda ya Utekelezaji ya kusimamia mchakato hadi kusajiliwa kwa tawi katika kipindi kisichozidi miezi sita.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Makamu Nape Mnauye wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Bubelwa Kaiza anayekuwa Katibu Mtendaji. Kaiza ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa ForDIA.
2. Wadau walipokea na kujadili Ripoti ya ForDIA juu ya mtazamo wa wananchi kuhusu rushwa (Mtazamo-rushwa) katika wilaya 35 za Tanzania Bara ambayo ilizinduliwa rasmi jana katika hotel ya Giraffe Ocean View. Ripoti inachambua ifuatavyo:
(i) Halmashauri ambazo hazina kiwango kikubwa cha matukio ya rushwa: Tandahimba (asilimia 95), Mtwara Vijijini (89.55), Ulanga (87.5), Nachingwea (85.2), Liwale (84.9), Shinyanga mjini ( 84.4), Mbinga (83.3) na Ruangwa (77.05).
Nyingine zilizo juu ya asilimia 50 ni Tunduru (76.6), Mbeya Vijijini (75), Rungwe (73.3), Kilosa (66.65), Morogoro Mjini (61.4), Kilwa (60.4.), Kyela (58.35) na Lindo Mjini ( 50.35).
(ii) Halmashauri zinazoongoza kwa kiwango kikubwa cha matukio ya rushwa: Mbozi (asilimia 93.75)), Muleba (93.5), Bukoba Vijijini (87.85), Bariadi (80), Miseny (7, na Newala (70.85), Kishapu (70.1), Meatu (68.35), Mtwara Mjini (65.2), Bukoba Mjini (64.6).
Nyingine zinazoongoza kwa matukio ya rushwa juu ya asilimia 50 ni Kahama (63., Mbeya Mjini (62.5), Namtumbo (61.05), Bukombe (60.4), Mbarali (60.15), Ileje 59.65), Lindi Vijijini (56), Mvomero (55), na Chunya (52.1).
Akizindua Ripoti ya Mtazamo-rushwa, Mkurugenzi Mtendaji wa TAKUKURU, Dk. Edward G. Hosea alisema kazi iliyofanywa na ForDIA ni kubwa na muhimu; na kwamba kazi za aina hiyo huwapa watunga sera ushahidi mwanana wa tatizo husika ili wapate upenyo wa kuanzia katika kukabiliana na tatizo.
Aliwapa changamoto wadau katika eneo hili, wasomi, wanataaluma katika medani ya maendeleo, watafiti na wananchi kwa ujumla, kusoma, kujadili na kutoa maoni juu ya ripoti hiyo yenye kurasa 135.
Bubelwa Kaiza
Mkurugenzi Mtendaji
--------------
Executive Director
Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA)
Secretariat of the Great Lakes Peace and Security Network (PeSeNet)
Off University Road, Survey Area, Kawe/Mlalakuwa Plot # 301-304, House # 250
P.O. Box 32505,
Dar es Salaam -TANZANIA
Tel: +255 22 2701890
+255 22 2701895-6
Cell: +255 784 410 939
Fax: +255 22 2701890
E-mail: bubelwa.kaiza@fordia.org
Website: www.fordia.org

Last edited: