Kuundwa kwa kundi la Weusi na kufa kwa kundi la River Camp Soldiers na Nako2nako

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,409
0
Mara nyingi Nikki wa Pili kama msemaji wa kundi la WEUSI amekuwa akinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akidai kwamba weusi si kundi bali ni kampuni ambayo haina uhusiano wowote na kundi la rivercamp soldiers ambalo lilikuwa linaundwa na Joh Makin, Nikki wa Pili, Bonta na wengineo na pia haliingiliani na kundi la Nako2Nako lilikuwa likiundwa na Gnako&Lord eyez na waliojitoa mapema Bu Nako na Ibra da.

Nikki anasema kuwa kuwa makundi ya rivercamp soldier na Nako2Nako hayajafa na bado yanaendelea na shughuli zao, ukweli ni kwamba makundi haya wawili yalishakufa tangu tu pale kundi la weusi lilipoundwa. Toka kundi la weusi limeundwa lini tumesikia kazi ya nako2nako? lini tumesikia kazi ya rivercamp soldier kundi ambalo lilikuwa lipolipo tu halina mbele wala nyuma.

Joh makini na Nikki wa Pili ndio wameyaua haya makundi kwasababu za kimaslahi, kwanini Bonta hayupo kwenye kundi la WEUSI? Walitumia vigezo gani kuunda hiyo kampuni?

Kama wao walihisi wakifanya nyimbo kati ya John Makini, Nikki, G nako na Lord Eyez ndio inakuwa nzuri basi ni vema wakawa wawazi kuwa washajitoa kwenye makkundi yao na waunda kundi jipya kuliko kuwadanganya wenzao na watanzania kwa ujumla.

Kulikuwa kuna umuhimu gani wa kuunda hiyo kampuni ya weusi wakati kundi lenu tu la rivercamp soldiers halijafanya chochote kinachoonekana kwa jamii? Kulikuwa na umuhimu gani wa kuunda kampuni ya weusi wakati kundi la nako2nako lilikuwa bado halijasimama vizuri? ni kipi hasa mlichokuwa mkikitafuta ambacho hakipo kwenye makundi yenu?

MCHAWI WA MSANII, NI MSANII MWENYEWE. OVER
 
Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,603
2,000
Bonta ni dokta proffesional na alikuwa anafanya kazi serikalini so ni ngumu kumanage music kama Nikki,GNako,JMakini na Lord Eyes ambao hawajaajiriwa
 
Kumbuka wakati kundi la weusi linaundwa hata nikki wa pili alikuwa ni mfanyakazi wa ANPPCAN ambayo ni NGO, kumbuka private unabanwa sana kuliko hata huko serikalini unapokuzungumzia wewe
 
privacy

JF-Expert Member
Apr 20, 2014
1,349
2,000
Kazi ya mwisho ya Nako2Nako unayoifahamu wewe ni ipi?? Imefanyika lini??

Turudi kwenye River Camp nitajie wimbo ambao kwenye details zake unaitwa Wimbo wa "River Camp" (Soldiers)

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
believer

JF-Expert Member
Dec 22, 2012
615
250
Kweli imekufa

Hapo mnachanganya habari,mtoa mada moja ya hoja zake ni kua Bonta hayupo kwenye kampuni,weusi inaundwa na bonta,joh makini,nikki wa pili,lord eyez na the kankara himself.Issue ya kutoonekana sana alongside weusi ni majukum yake binafsi yanambana,kufa au kufufuka kwa makundi imategemea na industry imekaaje,bonta yupo weusi.
 
strong ruler

JF-Expert Member
Nov 2, 2013
4,787

Sawa sawa jamaa nimekusoma!!
 
Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,409
0
Hapo mnachanganya habari,mtoa mada moja ya hoja zake ni kua Bonta hayupo kwenye kampuni,weusi inaundwa na bonta,joh makini,nikki wa pili,lord eyez na the kankara himself.Issue ya kutoonekana sana alongside weusi ni majukum yake binafsi yanambana,kufa au kufufuka kwa makundi imategemea na industry imekaaje,bonta yupo weusi.

SI KWELI, Bonta hayupo Weusi. Na hata kama yupo Weusi kwa muujibu wa maelezo yako, utetezi wako kwamba Bonta yupo busy SI KWELI. Mbona track zake anafanya? Ukisema wanashindwa kuonana wapange bado SI KWELI, Kuna wasanii wangapi wa bongo wanafanya track na wasanii wa nje ya nchi. Cha msingi ni kumtumia idea mwenzio then unatuma beat kisha yeye anaenda studio kuingiza Vocal then anawatumia, huu ni ulimwengu wa dijitali mkuu. Weusi kundi la watu wanahisi wao ni bora zaidi ya wenzao na wakaamua kuwasusa wenzao waliotoka nao mbali.
 
appoh

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
4,914
2,000
nako to nako imekaa kisela avi zaidi na river camp soldier imekaa kikauzu zaidi weusi imekaa kibiashara
 
kalagabaho

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,329
2,000
Unataka wavuta bangi waendelee kukaa kwenye makundi?. Sasa tutakuwa na makundi ya wavuta bangi mangapi?
 
Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,603
2,000
Kumbuka wakati kundi la weusi linaundwa hata nikki wa pili alikuwa ni mfanyakazi wa ANPPCAN ambayo ni NGO, kumbuka private unabanwa sana kuliko hata huko serikalini unapokuzungumzia wewe

Inategemea na hiyo kazi,madaktari wanafanya kazi almost week nzima na jamaa yuko mkoani WEUSI muda mwingi wako Dar na wanazunguka mikoani kufanya show.Kuhusu kufanya track zake ni kwamba hata SUGU yuko busy bungeni lakini bado anatoa track but anafanya for fun sio kama zamani
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,415
2,000
Waje watuambie kuwa Nako 2 Nako imekufa na River Camp nayo imekufa,

Tutawaelewa
 
believer

JF-Expert Member
Dec 22, 2012
615
250
SI KWELI, Bonta hayupo Weusi. Na hata kama yupo Weusi kwa muujibu wa maelezo yako, utetezi wako kwamba Bonta yupo busy SI KWELI. Mbona track zake anafanya? Ukisema wanashindwa kuonana wapange bado SI KWELI, Kuna wasanii wangapi wa bongo wanafanya track na wasanii wa nje ya nchi. Cha msingi ni kumtumia idea mwenzio then unatuma beat kisha yeye anaenda studio kuingiza Vocal then anawatumia, huu ni ulimwengu wa dijitali mkuu. Weusi kundi la watu wanahisi wao ni bora zaidi ya wenzao na wakaamua kuwasusa wenzao waliotoka nao mbali.

Mkuu,industry ya music bongo imeshikiliwa sana na Clouds group of companies,hapo kuna sijui prime time promo,cloudsfm,tht nk,hawa jamaa wama influence sana,wanaweza kukuza kibaya,wanaweza kuua kizuri,back to the point,Weusi ni kampuni iliyosajiliwa rasmi,ill mfikie malengo lazima muwe na mitizamo inayofanana thts y wako 5,bonta ndani mkuu,muziki umebadilika,kuna ishu za mikataba,matangazo nk tofauti na makundi hakuna hata MoU,makundi hayo hayajafa.
 
Hiram Abiff

JF-Expert Member
Apr 14, 2013
892
1,000
Mara nyingi Nikki wa Pili kama msemaji wa kundi la WEUSI amekuwa akinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akidai kwamba weusi si kundi bali ni kampuni ambayo haina uhusiano wowote na kundi la rivercamp soldiers ambalo lilikuwa linaundwa na Joh Makin, Nikki wa Pili, Bonta na wengineo na pia haliingiliani na kundi la Nako2Nako lilikuwa likiundwa na Gnako&Lord eyez na waliojitoa mapema Bu Nako na Ibra da.

Nikki anasema kuwa kuwa makundi ya rivercamp soldier na Nako2Nako hayajafa na bado yanaendelea na shughuli zao, ukweli ni kwamba makundi haya wawili yalishakufa tangu tu pale kundi la weusi lilipoundwa. Toka kundi la weusi limeundwa lini tumesikia kazi ya nako2nako? lini tumesikia kazi ya rivercamp soldier kundi ambalo lilikuwa lipolipo tu halina mbele wala nyuma.

Joh makini na Nikki wa Pili ndio wameyaua haya makundi kwasababu za kimaslahi, kwanini Bonta hayupo kwenye kundi la WEUSI? Walitumia vigezo gani kuunda hiyo kampuni?

Kama wao walihisi wakifanya nyimbo kati ya John Makini, Nikki, G nako na Lord Eyez ndio inakuwa nzuri basi ni vema wakawa wawazi kuwa washajitoa kwenye makkundi yao na waunda kundi jipya kuliko kuwadanganya wenzao na watanzania kwa ujumla.

Kulikuwa kuna umuhimu gani wa kuunda hiyo kampuni ya weusi wakati kundi lenu tu la rivercamp soldiers halijafanya chochote kinachoonekana kwa jamii? Kulikuwa na umuhimu gani wa kuunda kampuni ya weusi wakati kundi la nako2nako lilikuwa bado halijasimama vizuri? ni kipi hasa mlichokuwa mkikitafuta ambacho hakipo kwenye makundi yenu?

MCHAWI WA MSANII, NI MSANII MWENYEWE. OVER

bullsh!t
 
Mndengereko

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
7,209
2,000
nako to nako imekaa kisela avi zaidi na river camp soldier imekaa kikauzu zaidi weusi imekaa kibiashara
sio kweli nako to nako ilikuwa juu zaidi ya river camp ila ukosefu wa ubunifu,na lord izy kuwadhulumu wenzzake pesa(maslahi binafsi )ilipelkea kundi kufa nakumbuka kwenye show nyingi tu nako to nako walikuwa wanapata shwngwe za kutosha kuliko hiyo river camp mbayo joh makini ndo alikuwa anatamba peke yake na kwa mbaali niki
 
believer

JF-Expert Member
Dec 22, 2012
615
250
sio kweli nako to nako ilikuwa juu zaidi ya river camp ila ukosefu wa ubunifu,na lord izy kuwadhulumu wenzzake pesa(maslahi binafsi )ilipelkea kundi kufa nakumbuka kwenye show nyingi tu nako to nako walikuwa wanapata shwngwe za kutosha kuliko hiyo river camp mbayo joh makini ndo alikuwa anatamba peke yake na kwa mbaali niki
appoh kasema n2n lilikua kundi la kisela zaidi na rivercamp soldiers lilikua camp la kikauzu zaidi,hajasema river ilikua zaidi ya n2n.
 
Mndengereko

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
7,209
2,000
appoh kasema n2n lilikua kundi la kisela zaidi na rivercamp soldiers lilikua camp la kikauzu zaidi,hajasema river ilikua zaidi ya n2n.
what was he trying to say ni kwamba river camp ilikuw juu ya n2n something that was not right na ndicho nilichokimaanisha hapo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom